Kweli Tanzania inahitaji Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya?

kazi yao ni kula kodi za wananchi bure! Sisi sera yetu ni majimbo na sii huu upuuzi wa mkuu wa mkoa mkurugenzi wa mkoa mkuu wa wilaya mkurugenzi wa wilaya yaani wizi mtupu
 
Ni makada wa chama cha mapinduzi na wako pale kwa maslahi ya chama japo kupitia mgongo wa ukuu wa mkoa/wilaya usiumize kichwa juu yao kwa sasa time will come
 
Ni makada wa chama cha mapinduzi na wako pale kwa maslahi ya chama japo kupitia mgongo wa ukuu wa mkoa/wilaya usiumize kichwa juu yao kwa sasa time will come

Wishful thinking.

Tomorrow never comes.

Mla, mla leo, mla jana kala nini? kesho unaijuwa weye?
 
Ndugu wana JF kila mara najiuliza hivi ni nini kazi za mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya katika kumletea mwananchi maendeleo. Nimefuatilia sana lakini sioni umuhimu wa hawa wateule wa rais zaidi ya kuwa wapambe na vikwazo vya maendeleo. Kama kuna mwenye kujua anjuze kazi za hawa mabwana tafadhali naomba anisaidie maana nimefuatilia nimeshindwa.

Mkuu wa mkoa ni Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ni Mkuu wa wilaya. Wewe Mkuu wako wa mkoa ni nani? na wa wilaya je?
 
Mkuu wa mkoa ni Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ni Mkuu wa wilaya. Wewe Mkuu wako wa mkoa ni nani? na wa wilaya je?

Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa kwanza ni Wakuu wa Ulinzi na Usalama katika maeneo yao (Wilaya na Mkoa) kwa maana kwamba wanamwakilisha Mhe. Rais katika masuala yote ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yao kwahiyo vyombo vyote vya Usalama ndani ya Mikoa na Wilaya vinavyafa kazi kwa karibu sana na Mkuu wa Mkoa/Wilaya na hivyo ripoti zote za hali ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yao lazima wayapate. Ndiyo wanaotakiwa kuhakikisha kuwa hakuna wizi, ujambazi, uharamia unatokea katika maeneo yao kwa kushrikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Pili, Wakuu wa Mikoa ni wasimamizi wa shughuli za Maendeleo yote katika maeneo yao. Kwa mfano, kama mkoa umepanga kujenga shule za form five katika kila Tarafa au kuchimba bwawa sehemu fulani , Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya husika watakuwa wakifuatilia utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa muda na kwa kiwango kinachotakiwa. Mifano iko mingi lakini kwa ujumla wanatakiwa kusimamia shughuli zote za maendeleo katika maeneo yao.

Tatu, Wakuu wa Mikoa/Wilaya ni wafuatiliaji na wasimamizi wa utekelezaji wa Sera mbali mbali za Serikali katika maeneo yao. Kwa mfano, Serikali ikisema kuwa Mwaka huu wa 2012 ni kuhesabu watu na tunataka kujua kuwa kila Mkoa ina idadi ya Watu kiasi gani, Mkuu wa Mkoa/Wilaya watafuatilia utekelezaji wa watendaji wa serikali ambao wanatakiwa kufanya shughuli za kuhesabu watu katika mikoa/wilaya zao. Hapa utaona kuwa Wakuu wa Mikoa/Wilaya ni wasimamizi wakuu wa Watendaji wa Serikali katika maeneo yao. Wanatakiwa kuhakikisha kuwa mikakati ya serikali inaenda kama ilivyopangwa katika mwaka husika.

Kazi za Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa wilaya ni nyingi na zinachangamoto nyingi sana tofauti na WATU wanavyofikiria kuwa ni kazi ya kula pesa tu ya serikali. Nasema hivi kwa sababu, hakuna kazi yoyote ile ya Serikali na hata isiyo ya serikali ambayo mtu wa nafasi hiyo hatoweza kula pesa. Mambo haya miaka ya nyuma yalikuwa yakifundishwa katika shule za misingi kwenye somo la siasa/Civics/Government (kwa baadhi ya nchi) na sikuhizi hayafundishwi kwa hiyo wengi hawayajui majukumu ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya hata kidogo.

Nadhani nimejaribu kueleza unaweza sasa kupata mwanga kidogo. GONGA LIKE basiiiiiiiiiiiii!!!
 
Hii itakuwa tz tu na lazima uwe umelewa au umevuta kumuelewa huyu tobo lisu
 
akihutubia
mkutano wa chadema huko kilombero mh tundu lisu amesema viongozi wa
wilaya na mikoa wachaguliwe na wananchi ili wawe na kasi ya kuwaletea
maendeleo!!

Hakuna haja ya kuwa na vyeo hivi kwani havina tija na vinadumaza maendeleo ya nchi kutokana na matumizi yake makubwa ya ofisi zao. Kazi za maDC zinaweza kufanywa na District executive directors na kazi za MaRc zinaweza kufanywa na Regional Administrative secretaries. MaDC na MaRC ni mzigo wanaotwishwa wananchi kwa sababu ya kuwapa vyeo wapambe wa wanasiasa!! Kutaka wananchi ndio wawachague MaDC na MaRC ni kuwasumbua wananchi kwani wanachagua madiwani na wabunge kama wawakilishi katika sehemu zao!
 
Poor Governance!

Mtindo wa kuchaguana kwa kujuana huu ndio unaoturudisha nyuma, na wahusika kuwa na hamasa ya kumlinda aliyewaweka madarakani bila kujali wananchi wanaowatumikia. Wenzetu walishaona hilo ndio maana wakaamua viongozi hao wachaguliwe na wananchi. Mawaziri ni kitu kingine kwani ni wasaidizi wa karibu wa Mkulu lakini wanatakiwa wathibitishwe na mhimili wa bunge ambao unawakilisha wananchi.
 
Namuunga mkono Lissu nishasema hapa kuhusi hili kwa upana. Utaratibu wa sasa wa Mkuu wa Mkoa na Wilaya kuchaguliwa ni mbaya na unarudisha maendeleo nyuma kwasababu (1) Wengi wao wanafanyakazi sehemu ambazo hawazipendi (2) Wakuu hawa wakifanya vizuri badala ya kusaidiwa zaidi wanahamishwa kwenye Wilaya kubwa zaidi ambazo nyingi zao zina maendeleo zaidi kitu ambacho ni kinyume kwani sehemu zenye shida ndizo zina shida zaidi ya uongozi mzuri (3) Kwasababu hawa chaguliwi wengi wao hawajali uwekezaji wa muda mrefu badala yake wanatafuta sifa tu ili waamishwe. Hivyo kwa mawazo yangu ni bora uchague watu wanaopenda kuishi kwenye sehemu hizo badala ya kulazimisha. Lakini ni Lazima ni seme hili Serikali ni lazima ifanye utafiti kwanza wa nafasi na idara zote za serikali ili kujua ni zipi muhimu na ni zipi zichanganywe maana huduma nyingi sana zinaweza kuchanganywa. Serikali kwa mawazo yangu itafuta kampuni ya kimataifa ya ufanisi (Productivity) na wafanye research ya idara zote ili waongeze huduma, wapunguze ukubwa wa serikali na waongeza ufanisi kwa kupitia technologia.
 
Hii itakuwa tz tu na lazima uwe umelewa au umevuta kumuelewa huyu tobo lisu

Yawezekana hukubaliani na hoja za Lissu ,lakini kamwe hiyo haikupi uhalali wa kutoa lugha chafu.
Jisikie aibu kutamka maneno yasiyo na staha kwa wanadamu wenzako.
Vinginevyo hapa si mahali mwafaka kwako.
Kama huwezi kuhimili mikiki ya kuwa hapa,kaa barazani ,piga umbea na wambea wenzako.
Ona aibu.
 
Hakuna haja ya kuwa na vyeo hivi kwani havina tija na vinadumaza maendeleo ya nchi kutokana na matumizi yake makubwa ya ofisi zao. Kazi za maDC zinaweza kufanywa na District executive directors na kazi za MaRc zinaweza kufanywa na Regional Administrative secretaries. MaDC na MaRC ni mzigo wanaotwishwa wananchi kwa sababu ya kuwapa vyeo wapambe wa wanasiasa!! Kutaka wananchi ndio wawachague MaDC na MaRC ni kuwasumbua wananchi kwani wanachagua madiwani na wabunge kama wawakilishi katika sehemu zao!

jamani kwa wananchi wa kawaida wanafahamu dadizo la MA-DED na Ma-RAS kwa mfumo wowote ule wa chama kitakachokuwa madarakani madc na marc ni muhimu ni kuliko hao wa halmashauri ambao wengi wao ni wezi waliokubuhu wa mali za umma
 
mkuu ni udhaifu tu wa serikali kuwadhibiti
 
Back
Top Bottom