Kweli Tanzania hakuna Pesa?: Huyu ndiye Mtanzania anaemiliki Gari la Tsh Bilioni Moja

Sishangai mtanzania kumiliki gari la thamani hata ya bilioni mia. I know magari mengi ya bei mbaya tunayoyaona mitaa ya bongo ni ya wizi. Anaebisha naomba anitumie chesis no. ya gari ya mosha tumalize fitna. Tutajua mtoto wa bakhresa alinunua wapi.
 



“HII sasa ni kufuru!” Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.


Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.​


Gari analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya njano, linaaminika kuwa miongoni mwa magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania na Afrika, bali duniani kote, kwani hata siku Rooney alipolinunua wenzake wengi hawakutegemea, siyo kwa sababu hana fedha, ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya magari yenye thamani kubwa kama hilo.​


Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.​



Yafuatayo ni maelezo kuhusiana na gari hilo la kifahari kwa kuanzia kiwango cha mafuta na usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko yake.


Ameinunua kwa bei gani?



“Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua kwa mapenzi yangu.



Alipolinunua



“Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.


Spidi ya gari



“Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.



Matumizi ya mafuta



“Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.

Usumbufu anaoupata


“Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au msuguano mara kadhaa.

“Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.


“Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha.



“Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha.












kwani Mtoto wa Bakhresa sio Mtanzania? yawezekana kahongwa shida juu ya nini?
 
Sasa meku (mosha) hili dude unaliendeshea wapi? 360kph hapahapa tz??!!!!

Was asking myself the same question, ukiendesha kidogo shimo, mbele kidogo tuta, hatua chache zaidi foleni! Nafikiri linakuwa zuri zaidi Desembaaaaa.....wakati wa kwenda kuhiji mlimani. Napo litanoga akishafika kwenye ile stretch ya baada ya Chalinze.....
 
Cha ajabu ni kwamba, mtoto wa Bakhesa amekuwa akiliendesha hilo gari bila mbongo yeyote kufahamu kwani hakuhitaji promo, kalichoka akampa meku kama kawaida ya meku walivyo wapenda kujiboost basi anataka kutufanya tuone yeye ndiye mtanzania pekee kuwa na hilo gari, yani limeingia hapa nchini miaka mitano iliyopita na hakuna siku mtoto wa Bakhresa alijiweka kwenye mtandao yeye ndio ajifanye wa kwanza? Mbona watu wana Ferrari F50 kuna mhindi flani anayo nyekundu? Bentley hata yule mbunge wa ifakara mtaalamu Abdul Mteketa alikuwa nayo tatizo watu wanadanganya bei, anaweza kuwa kainunua milioni mia hamsini na wala sio hizo Bilioni, that is pathetic thinking. Otherwise gari ni nzuri ila asitudanganye bei.
 
Ukienda kwenye mnada wa magari used ya Japan utapata hata Bugati kwa bei kama dola laki moja haizidi mpaka lifike hapa yani milioni mia mbili haizidi roghly na kwa wapigaji kama hawa na group yao kina msofe, Ray na wenzie hawashindwi kununua gari hiyo ili wapate. Social climbing status waweze kuwapiga zaidi. Hata mtu mwenye kiwanda cha Asas dairy au Tanga fresh au ALAF anaweza kununua its not a big deal hata wewe unaezindika jam au mango pickle waweza kununua kama utapata soko la uhakika kwa miaka miwili tu na ukaamua kuziinvest pesa zote kwenye hiyo gari. Otherwise ni mateso tu anayajua mwenyewe kwani spea ndogo tu dola elfu kumin ishirini, hata kama unafanya biashara ya kiwanda cha sigara bado ni pesa nyingi unless ndiyo hobby yako yani hata nyumbani wakila manyasi we ni bora Lamborgini itembee uonekane! Otherwise I still believe the coupe is excellent wala sitaki kujua kainunua bei gani kwani anataka kutudanganya, gari kaitembelea mtoto wa Bakhresa miaka zaidi ya mitano yeye aje kujifanya kanunua Bilioni? Basi kama ameuziwa bei hiyo ninaamini kuwa yeye si mjanja aisee dah! Atakuwa kawaaibisha wanakaskazini wenzie wapenda kujibost! Hapo hakuna ujanja ni umbwiga.
 
Naunganisha dots mtoto wa mukulu yanga...davis mosha yanga.....mtoto wa mukulu biashara mafuta ...davis mosha biashara mafuta. Kuna habari za kuaminika kuwa wanafanya biashara na r1, hivyo msishangae sana, hiyo ndiyo bongo zaidi ya uijuavyo.





Sijawahi Kumsikia Huyu Mtanzania... Yuko kwenye SIASA? Kapataje PESA?

Ni mtoto wa Mkubwa? Anawajuwa Wakubwa wa CCM au CHADEMA?

Anatembeaje JIJINI Dar Mpaka anamiliki GARI GHALI kama hilo?

Niamsheni... Hata huku USA kumiliki hilo Gari sio Mchezo, Wengi walionalo hawaliendeshi kila SIKU
 
Achana nae mzushi tu huyo nyumbani kwake hapo
cbk

hizo ni councel flat ambazo zipo moja ya deprived areas in london (mitaa ya dagenham hiyo ndio mitaa wabongo weengi wapo huko).

By the way chilisosi toa post code yako.
Dah!! Umenikumbusha mbali sana..., dagenham east or dagenham heathway.., district line ndo ilikua njia yake hiyo sjui saivi
 
Gari nzuri, nitaomba lift siku moja nitokeleze nayo mitaa ya town. Ila jamaa ana ulimbukeni au, kujitangaza hivyo ili iweje! Mi watu ambao hawana nidhamu ya fedha nawaona washamba na sio wajanja.
 
1 billion for a used lamborghini???? :D changa la macho, mwambieni jamaa aache ushamba!! Atanunua Altezza kwa milioni 30 uyo!
 
Sijawahi Kumsikia Huyu Mtanzania... Yuko kwenye SIASA? Kapataje PESA?

Ni mtoto wa Mkubwa? Anawajuwa Wakubwa wa CCM au CHADEMA?

Anatembeaje JIJINI Dar Mpaka anamiliki GARI GHALI kama hilo?

Niamsheni... Hata huku USA kumiliki hilo Gari sio Mchezo, Wengi walionalo hawaliendeshi kila SIKU


kwani walio kwenye siasa ndio peke yao walio na pesa?
 
Nilliona mara ya kwanza Mjini Kampala mwaka 2004 alikuwa analo Mganda mmoja anaitwa Ezra (wakati huo alikuwa na miaka 33) ambaye alikuwa pia anataka kununua Leeds United
 
Hili ndiyo tatizo la watanzania wengi. Jamaa tayari ana hilo gari na wala hatupaswi kufahamu amepata vipi hizo fedha zake. Kama ameRICHMOND, ameEPA, amePEMBEJEO, ameCHAKACHUA yote sawa coz ndiyo nchi yetu ilivyo mtu akipata mchongo anapiga. La msingi ni kujadili namna ya kuwabana watu tunaodhani wanatufisadi kwa maslahi ya taifa letu.
 
Sikonge sidhani kama kuna matumizi makubwa ya umeme.

Nafikiri watumiaji wakubwa ni Moravian Church Hospital. Kwa watu wa kawaida sanasana ni TV, Frigi SABUFA (Sub Woofer) na vitu vidogo vidogo kama kucharge simu.

Sidhani kama kuna wapikaji wengi wa kutumia umeme. Pia Air Condotion sijui kama zipo.

Sikonge hakuna kiwanda na hapo unapata jibu, kwa nini 500 HP na umeme wa kama 400kw utatosha.
Mmh! H.P. 500? Mh. Sikonge nadhani umekosea! Sasa hiyo Wilaya ya Sikonge itakuwa kama kajiji fulani hivi ambako hakafikishi hata Maximum Load below 1MG (MeggaWatt)?
 
Swali la kijinga:-
Je malipo yalifanyika benki gani?
Au alijitwisha li bilioni lake kwenye gunia na kulipeleka nyumbani kwa Bakhresa?
 
Nimeangalia habari nadhani ilitoka katika magazeti ya Global Publishers, ila pia ilikuwemo humu JF na wengi kuchangia.
Habari yenyewe iko hapo chini.
Nahisi habari hiyo ni uongo mtupu na kutafuta umaarufu.
Ukweli ni kuwa bei ya gari aina ya Lamborghini mpya (sio used kama ya Mosha) ni USD 248,000.
Maana yake ni kuwa hata ukiweka kodi na usafirishaji haiwezi kufika TShs 500M (kwa mpya).

Bei angalia; 2012 Lamborghini Gallardo LP570-4 Spyder Performante Convertible Price, MSRP & Dealer Invoice Pricing | Automotive.com

Habari angalia: https://www.jamiiforums.com/habari-...ania-anaemiliki-gari-la-tsh-bilioni-moja.html
 
Back
Top Bottom