Kweli serikali yetu ni sikivu?

EL MAGNIFICAL

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
938
125
ni juzi tu kwenye vikao vya bunge kabla halijaairishwa mh. John cheyo alipotoa ripoti kuonesha ni jinsi gani serikali inavyoingia hasara kwa kuwa na matumizi yasiyo ya lazima akatoa mfano jinsi kodi za watanzania zinavyomalizwa ktk maandalizi ya sherehe mbalimbali mfano 7 saba, nane 8 sijui miaka 50 ya uhuru, mei mosi nk.
Sasa kilichonishangaza kwa leo ni ktk sherehe iz za miaka 48 ambapo naona wamerudia mambo yale yale.
Mfano kuna kundi kubwa la watu wamevishwa nguo nyeupe na kofia na ni dhahili inaonesha kuna chochote wamepewa pamoja na usafiri wa kwenda na kuludi, pia kuna ngoma, show itayofanywa na watoto. Ndg wanabodi kama serikali inashauriwa kufanya jambo flani kwa namna flani yenyewe inazidisha ndio usikivu huu tunaousikia wanajisifu.......!
 
Huyo Cheyo ni mnafiki tu, ni mchumia tumbo tu, anauma na kupuliza ili ccm wasiache kumpanga kwenye ziara mbalimbali za rais nje ya nchi. Mwanzoni nilimwamini sana kumbe mtu mzima hovyooooo.
 
Huyo Cheyo ni mnafiki tu, ni mchumia tumbo tu, anauma na kupuliza ili ccm wasiache kumpanga kwenye ziara mbalimbali za rais nje ya nchi. Mwanzoni nilimwamini sana kumbe mtu mzima hovyooooo.
huwezi amini mkuu japokuwa yeye ndio aliyetoa ushauri lakini yupo naye ndani ya nyumba
 
Yetu macho. masikio yamezibwa nta. Serikali inamsikiliza nani? Lowasa, Rostam, Chami, Ngeleja, Malima, Nundu au yule Ngw'anamalundi?

:rolleyez:
 
duh ivi kweli tumefikia hapa kweli !
Mkuu, na bado. Tutafikishwa mbali zaidi. Sauti zetu ni kelele za madebe.
Nyimbo zetu tamu ni kelele za budi kwao. Ukimya wetu ni sawa na maiti. Kwao ule usemi wa "kimya kina kishindo" ni usemi wa wakosaji na wagonjwa wa akili.
Nundu, chami, maige, na wanaofanana na hao kwao wao mwendo mdundo. Twafwa
 
mungu ibariki TZ hali si shwari.
 
Back
Top Bottom