Kweli Nimekubali Jakaya ni Zaidi Ya Mubarak



WANANCHI HATUKO SALAMA TENA WALA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA KUONGEZEKA: KWA HILI SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake.

Yalianza na vifo vya raia kule (1) Pemba, baadaye (2) Unguja, Kisha (3) Mbagala, nako Arusha Mjini, (4) mauaji ya wakulima kule Mashamba ya mpunga kule Mabuki Mbeya na sasa (5) Gongolamboto.

Ajabu ni kwamba licha ya wananchi wengi kuuaua na mali zao kuteketea, hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuwajibika wala kuwajibishwa serikalini. Kote ni kiburi na jeuri tu mbe ya kupotea uhai wa mtu na watoto kubaki miyatima!!!

Jukumu la msingi halijazingatiwa; kuna watu wanasinzia kwenye majukumu nyeti na sasa kutugharimu kiasi hini, wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

Hatutaki tena tume kwani hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????


Gongo1.jpg


Gongo2.jpg

_51307856_munition_ap.jpg

_51307454_bus_ap.jpg

Debris and arms were hurled across the Tanzanian of city of Dar es Salaam on Wednesday night after an accident triggered a series of explosions at Gongola Mboto military base.
_51310264_lostchildren_ap.jpg
Tanzania's Red Cross says about 200 children who lost their parents during the confusion of the blasts are being cared for at the city's stadium.

_51312030_cherehani.jpg



attachment.php
 
Back
Top Bottom