Kweli kutesa kwa zamu, nilimdharau leo zamu yake!!

Da Pretty

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
3,059
1,148
Habari wapendwa.
Miaka 12 iliyopita nilikua A'level shule moja DSM.
Kuna binti nilikaa nae hostel. Hatukua tunapatana kabisa na kiukweli nilimpa wakati mgumu sana siku zile kwa sababu nilikua na nguvu kubwa ya kushawishi kuliko yeye, ikamlazimu kuhama pale akatafuta hostel ingine lakini darasani tulikua tunakutana. Tukamaliza shule hatuongei kabisa!
Baadae kila mtu akawa na mambo yake, tukasoma vyuo tofauti katika mikoa tofauti.
Mwenzangu wakati yupo Chuo akapata kazi kwenye NGO moja na baadaye akaajiriwa hapo.
Ninavyoandika hapa, ni kwamba nimemkuta yeye ni Senior na ni Line Manager wangu!!
Ni mwezi wa nne sasa nipo kazini lakini mazingira ni magumu.
Hatusalimiani,nimejaribu kujishusha wala hana mpango.
Mbaya zaidi kila siku nakumbushwa kuwa nipo kwenye probation na anamwambia mwenzangu kama sitaki kazi niseme.
Sielewi ni utumwa na manyanyaso tu,hapa natafuta kazi nyingine.
 
hapo tu ndipo wanadamu huwa wanajisahau lakini na yeye alipaswa kusamehe kama kweli ni mtu anayempenda Mungu alitakiwa akutende wema zaidi ili iwe fundisho kwako na kwa kizazi chako na ingekuwa njia nzuri zaidi ya wewe kuwalea wanao jinsi ya kuishi na watu lakini unyama anao ufanya yeye hata Mungu apendi
 
Mmmmh pole!
Kama vipi tafuta nafasi uongee nae umwombe msamaha!Next time jifunze kuwachukulia watu poa tu...kama mtu hana matatizo na wewe usiyatafute kwa lazima!!

well said dearest,na akiona haelekei kumsamehe,atafute kazi nyingine,kuna watu hawasamehi wala kusahau hata jambo moja,na wanapopata nafasi ya kukomoa,hawaichezei.....pole sana Da Pretty, we learn through mistakes,ila usiteseke kwa makosa yaliyopita,tafuta njia kuondoa tofauti zenu,ukiona haiwezekani,riziki si hapo tu...Mungu atafungua mlango mwingine,tafuta kazi sasa.
 
Mmmmh pole!
Kama vipi tafuta nafasi uongee nae umwombe msamaha!Next time jifunze kuwachukulia watu poa tu...kama mtu hana matatizo na wewe usiyatafute kwa lazima!!
Acha ukome na ukomae.we ulikuwa unaona karibu kama kondoo sasa unateseka nini kama yeye aliama hostel we acha kazi
 
Angekuwa ni mwanaume na wewe ni mwanaume angeweza samehee,lakini mara nyingi Wabejingi huwa hamsamehani katu,so hapo wewe anza tafuta kazi pengine. Hapo umeingia kwenye chaka la simba lazima uliwe
 
Weye ndiye mbaya!
SASA mnasema huyo dada amsamehe Da Prety....Pretty ndiye mwenye jukumu la kwenda kuongea na huyo mdada amwombe yaishe!

Roho Mbaya inakuja kulipwa haki yake somewhere maishani!..Unalo mwaya!
 
haaaaaaaaaa haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

duh.........................hiii ni filam ya kinigeria kabisa lol ...............
 
Huwa nikikutana na stori kama hizi huwa nazidi kuamini kuwa hakuna motoni (jehanam), what comes around goes around they say!

Shukuru Muumba kwa kupata nafasi ya kufanya malipizi, mimi naona njia yako kwenda mbinguni inazidi kuwa nyeupe!
 
teh teh,we bana jikaze mpigie magoti mwombe msamaha km unataka kazi,vinginevyo utaacha kazi utapigwa jua kinoma halafu baadae utatakiwa umwombe yeye tena kurudi kazini maana kapanda cheo,shauri yako chelewa zaidi majuto zaidi:biggrin1:
 
jifanye umesahau uone atafanya nini...

watu wa aina hiyo huwa sio watu wa visasi

tayari yeye ana enjoy wewe kuwa chini yake
na roho yake imeshafurahi na hatakufukuza kazi
bali ata enjoy kukutuma tuma

so wewe now go with the flow uone itakuwaje....
 
Habari wapendwa.
Miaka 12 iliyopita nilikua A'level shule moja DSM.
Kuna binti nilikaa nae hostel. Hatukua tunapatana kabisa na kiukweli nilimpa wakati mgumu sana siku zile kwa sababu nilikua na nguvu kubwa ya kushawishi kuliko yeye, ikamlazimu kuhama pale akatafuta hostel ingine lakini darasani tulikua tunakutana. Tukamaliza shule hatuongei kabisa!
Baadae kila mtu akawa na mambo yake, tukasoma vyuo tofauti katika mikoa tofauti.
Mwenzangu wakati yupo Chuo akapata kazi kwenye NGO moja na baadaye akaajiriwa hapo.
Ninavyoandika hapa, ni kwamba nimemkuta yeye ni Senior na ni Line Manager wangu!!
Ni mwezi wa nne sasa nipo kazini lakini mazingira ni magumu.
Hatusalimiani,nimejaribu kujishusha wala hana mpango.
Mbaya zaidi kila siku nakumbushwa kuwa nipo kwenye probation na anamwambia mwenzangu kama sitaki kazi niseme.
Sielewi ni utumwa na manyanyaso tu,hapa natafuta kazi nyingine.

Mazungumo na record za kiofisi zinakwenda kwa maandishi sio kwa mazungumzo ya mdomo

Wewe anaandika memo mwambie kwa uzoefu wake na kama incharge mzoefu anaonaje utendaji/performnce yako ili ujue kama uko kwenye track sawa au si sawa na nini unaweza kujireebisha kiofisi. ili uwe mfanyakazi mzuri kwenye majukumu yako.

yaani hiyo ni memo ya kuomba ushauri but kama ana akili atagundua na atatofautisha mambo ya ofisi na mambo personal. Na asipkujibu atauwa upata ujumbe kiofisi na somo kalipata.
 
Wanasema malipo ni hapa hapa duniani. Nafikiri utakuwa umejifunza mengi kwenye hii situation. Milima haikutani lakini binadamu hukutana. Kwa kuwa ullimpa wakati mgumu sana siku zile kwa sababu ulikuwa na nguvu kubwa ya kushawishi naona sasa she is on the driving seat. I have always said kuwa wakati mtu unamaliza shule na kuna mtu umemkorofisha ni bora umtafute na kwomba msamaha mapema kabla ya kuingia mitaani. Ukishaingia mtaani inakuwa ngumu.

Unaweza kumwomba msamaha huyo dada kwa vile tuu ni bosi wako. Vipi kama ingekuwa the other way round? Wewe ndio bosi halafu ndio kaja kufanya kazi hapo? Ungemwomba msamaha kwa uliyomtendea? Au tuseme tuu ungekutana naye njiani, ungemsimamisha na kuomba msamaha? Yaani hata akikusamehe sijui kama utaenjoy kufanya kazi hapo. I bet the whole office now know what you did to her. Ushauri wangu omba msamaha akubali asikubali sepa, tafuta kazi nyingine, and learn from your mistakes.
 
Pole sana. Ni vizuri kujifunza kuishi na watu vizuri hata kama kuna mambo mnatofautiana. ni bora kumpuuza mtu kuliko kujaribu kumjengea mazingira magumu kwa vile humpendi.

Vizuri umetambua kosa lako na sasa kwa vile umekubali kujishusha nakushauri umtafute mtu hapo kazini kwenu ambae yuko karibu nae hili hawakalishe pamoja na uweze kuomba msamaha na umuonesha kwamba umetambua kosa lako.

Baada hapo ndio utaweza kuangalia uhusiano wenu kazini unaendeleaje na jitahidi uwe mchapa kazi usimpe nafasi ya kupata sababu ya kujitesea.

Kazi ni ngumu kupata na uamuzi huko juu yako, uvumilivu wako wa kupuuza tofauti zenu ndio utakusaidia kuendelea kufanya kazi,lakini kama huwezi kuvumilia acha kujitesa katafute kazi sehemu nyingine.

Kila la kheri.
 
Duh, unalo..
Hivi kama wewe ndo ungekuwa Bosi wake ungefikiria kujipendekeza kwake au ungeendelea kumnyanyasa?
 
Angekuwa ni mwanaume na wewe ni mwanaume angeweza samehee,lakini mara nyingi Wabejingi huwa hamsamehani katu,so hapo wewe anza tafuta kazi pengine. Hapo umeingia kwenye chaka la simba lazima uliwe
Kama kazi unaipenda itabidi kuvumilia hayo mateso na kufanya kazi hivyo hivyo tu, ukifanya kazi yako sawasawa hatakuwa na la kukufanya zaidi ya kutoongea. Kwa ufahamu wangu juu ya wanawake kukusamehe itakuwa kazi ngumu, wanawake huwa hawasameheani. Ukizingatia kuwa uliyafanya maisha yake kuwa miserable usitegemee msamaha hapo, wewe fanya kazi yako kwa bidii yote ili usimpe nafasi ya kupata ushahidi. Mambo yakiwa magumu tafuta kazi nyingine.
 
hapo tu ndipo wanadamu huwa wanajisahau lakini na yeye alipaswa kusamehe kama kweli ni mtu anayempenda Mungu alitakiwa akutende wema zaidi ili iwe fundisho kwako na kwa kizazi chako na ingekuwa njia nzuri zaidi ya wewe kuwalea wanao jinsi ya kuishi na watu lakini unyama anao ufanya yeye hata Mungu apendi
kwani keshamwambia anamchukia? cha msingi ajitume tu na kama akiondolewa bila sababu ya mmsingi ndio ajue kuwa bado meneja anammaindi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom