Kweli kila mjanja ana mjanja wake!!

charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,320
1,369
Hii safu bwana inamambo na vijimambo kibao.Hii sio story ila niliipata kwenye primary source.

Unanjua nini?kuna watu bwana especially wanaume flani flani hawawezi kusafiri mbali na wapenzi wao au wake zao wakalala ugenini kibiashara etc bila kutafuta poza ganzi,milupo,au jina lolote unalolijua wewe ili mradi umeelewa.

Ilikuwa hivi,jamaa katika mishemishe huko huko TZ kapata kasafiri kwenda sehemu fulani.Huyu bwana ni mwanywaji,na huko ugenini alitafuta sehemu ya kuendeleza hiyo fani yake.Akiendelea kupiga kinywaji mara kamwona binti ambaye alimvutia na akili yake ikatamani avunje nae amri ya 6.Jamaa hakusita kamwita huyu binti,binti akaagiza soda na maongezi yakaendelea.Jamaa kaeleza shida yake na akaeleweka na kukubaliwa.

Muda ulipowadia jamaa kaondoka na huyo binti hadi rm alikokuwa amelipia kwa siku hiyo alale ili siku inayofuata aendelee na safari yake.Jamaa kwakuwa ni mzoefu wa kuvunja amri tajwa hapo juu katika mazingira kama yale alipofika ndani kasogeza kitanda mlangoni,yaani kazuia mlango kwa kitanda akihofia kulizwa vijisenti vyake.Amri ikavunjwa binti akapewa ujira wake wakalala.Binti kumbe kweli alitaka kumliza jamaa lakini atatokea wapi sasa?Hakukata tamaa katikati ya usiku kaamka katafuta hela za huyu baba zilipokuwepo kakuta kama laki 8 kazichukua kazichomeka kwenye ventilator juu ukutani yaani yale matundu ya kuingiza au kutolea hewa ndani.Then akarudi kulala.Jamaa muda si muda nayeye sijui alikuwa anaota anafukuzwa na zimwi akastuka usingizini akiwa amelala chali katika kutafakari ndoto, hamadi! kaona vinoti vinachungulia juu.Kapanda aone ni kitu gani kuvuta hivi kumbe ni hela zake.Basi nayeye kimyakimya kazichukua zile hela zake kasachi na pochi ya binti kachukua na hela aliyomlipa.Kavaa jeans yake kaziweka akarudi kulala.Kesho yake asubuhi na mapema kamwamsha binti akidai kuwa amechelewa usafiri aliokuwa anautarajia hivyo anaondoka haraka na kamwambia binti waondoke wote wakaachane huko mbele.Binti kakubali kajiandaa haraka haraka wakaondoka.

Hawajafika mbali binti kajifanya kasahau kitu kule room hivyo anarudi kukifuatilia then atarudi.Jamaa moja kwa moja akajua binti anafuata mzigo wake(hela alizoficha).Jamaa kaongeza hatua ili nayeye atokomee haraka.Binti kufika mle ndani alitafuta na kutafuta asione ile hela.Kwa hasira akakodi pikipiki aende akaugulie nyumbani kwake.Kafika home kwake sasa nauli inatakiwa,kucheki pochi yake hakuamini macho yake,pochi haina kitu kilichooendele hapo misijui.

Ikapita miezi na kwakuwa binti ile kumbe ndio shughuli yake kaenda eneo jingine(mkoa),ikatokea kama bahati sijui mkosi yule jamaa alikuwepo tena hapo mahali kapozi mahala anakunywa.Hakumwona binti.Binti akamkumbuka yule jamaa,akamfuata wakasalimiana vizuri.Binti akiwa na wasiwasi akamwuliza jamaa kuwa siku ile alitumia ujanja gani kumfanyia alicho mfanyia.Jamaa akajifanya wala hajui akamwambia eti yeye ana jini huwa anamsaidia na siku ile alipoteza laki 8 akazikuta zimeshatangulia nyumbani kwake na ziada ya kidogo kama elfu 10 hivi ila hakujua imetoka wapi ile ziada,binti kwa uwoga akaaga na kuondoka.
 
hahahah lol this is funny,alieyeuziwa cheni feki kapewa noti bandia...ni wewe nini mkuu??
 
Kweli hii hadithi tamu....lol!!

Mzima lakini Kaizer?


mzime Keren...nazingatia somo la Miss Judith kuhusu utongozaji, then nitafanya kivitendo soon...kuna mahali nimekutafuta pia kumbe unanisaka hapa....mmm
 
mzime Keren...nazingatia somo la Miss Judith kuhusu utongozaji, then nitafanya kivitendo soon...kuna mahali nimekutafuta pia kumbe unanisaka hapa....mmm

Mhhh...nakuambia baada ya somo ya Judith, hata kusalimia siku tunaona kazi.....!!! Nimekuona kwenye ule mtaa wa pili...! Nafikiri tuhamie huko....
 
Back
Top Bottom