Kweli inasikitisha sana...Kweli wizara husika ya elimu inashindwa kulipia chakula cha walimu siku 1?

Toneradio

Member
Jul 11, 2011
65
5
Katika tukio la kusikitisha sana kamera yetu iliwanasa wanafunzi wa kidato cha saba huko Rudewa wakiwa wameacha masomo na kujiandaa na Mitihani lakini wapo Bize kuvua Dagaa ili wapate Shiringi za kitanzania 600 kama malipo ya chakula cha walimu ambao wanatakiwa kusimamia mitihani hiyo.. nikajiuliza hivi Wizara ya elimu haiwezi kutoa fungu kidogo kwa ajili ya walimu hawa mpaka watoto wateseke kiasi kama hiki? kwa mfano hawa madogo ambao wako na mtumbwi ni hatari sana .... KUWAONA WANAFUNZI HAWA BOFYA HAPAhttp://latestnewstz.blogspot.com/2011/07/wanafunzi-wafanya-hughuli-za-uvuvi-ziwa.html
 
Hivi Ludewa wanasoma hadi kidato cha saba?? Nafikiri ulitaka kuandika darasa la saba!
Ndugu yangu, ukishangaa ya firauni utayaona ya Mussa. Wakati wewe unawashangaa wanafunzi wa Ludewa kushindwa kujiandaa na mitihani kwa ajili ya kutafuta chakula cha mwalimu, kwingineko Tanzania hii hii watoto wameombwa waje na viti kutoka nyumbani ili waweze kukalia wakati wa kufanya mtihani. Haya yanatokea katika nchi ambayo mkuu wa wilaya tu anatembelea shangingi la milioni 200. Kama wangeamua kununua Rav 4 ya milioni 50, halafu hiyo 150 inayobaki wakatumia kuboreshea elimu tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana hapa nchini. Lakini hizi kelele za hapa jukwaani hazisaidii kwakuwa haya yashajadiliwa sana na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali.
 
Katika tukio la kusikitisha sana kamera yetu iliwanasa wanafunzi wa kidato cha saba huko Rudewa wakiwa wameacha masomo na kujiandaa na Mitihani lakini wapo Bize kuvua Dagaa ili wapate Shiringi za kitanzania 600 kama malipo ya chakula cha walimu ambao wanatakiwa kusimamia mitihani hiyo.. nikajiuliza hivi Wizara ya elimu haiwezi kutoa fungu kidogo kwa ajili ya walimu hawa mpaka watoto wateseke kiasi kama hiki? kwa mfano hawa madogo ambao wako na mtumbwi ni hatari sana .... KUWAONA WANAFUNZI HAWA BOFYA HAPA

Hii ya kidato cha saba sina comment.

Child labour iliyorasimishwa na serikali, what a shame.
 
Back
Top Bottom