tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,855
- 1,117
Wakubwa shikamoni, wenzangu habari za jioni. Mimi ni kijana ambaye natafuta mchumba ambaye mambo yakienda sawa nataraji awe mke. Katika mizunguko ya kusaka degree nilimuona binti wa 2nd year, alinivutia na nilifanya jitihada nikapata namba yake, niliwasiliana naye kama 2 dayz na akahitaj anione, tulionana na tukaongea machache, baada ya hapo mawasiliano yalikuwa mazuri, na tukawa tunaonana mara chache, kwani tulikuwa busy na maandalizi ya UE. Sikuwa na jinsi, ikabidi nimueleze jins ninavyomhitaji, alinijibu kwamba ana mtu. Nilikubaliana na alichokisema, na nikafanya kautafiti kadogo na kugundua kuwa ana uhusiano na mtu ambaye amemzid sana kiumri, hivyo anaogopa/anaona aibu kumtambulisha kwa wenzake, rafik zake weng anawambia yuko single. Tatizo hapa ni kwamba hataki kunipa muda wa kukaa na kuongea naye, kuna muda huwa nataman kumpotezea, lakini upande mwingine nafsi yangu inambia yeye ndiye anayenifaa. Nishaurini/nipeni mbinu. Asanteni