Kweli CHADEMA wanapendwa hivi au Macho yangu!?

ni uchochezi tu unaoongozwa na mbowe,lema na komu..hawa jamaa sijui wanampango gani na hii nchi,alafu kuna vijamaa vinawaunga mkono hawa wachaga..kila kitu kwenye chama wanaongoza wao wakaskazini,ata ubunge wa Eac walimpeleka kiraza kisa ni wakwao..kuwa macho mkuu.

Umeamua kuwa punguwani!

They are talking of what's happenning in Mwanza wewe unaleta habari za wachagga
 
Kaah! Hii ya Rocky city nimeipenda sana! nilidhan A-town ndo wako juu kumbe hata mwanza ni zaidi?
 
As from my analysis CDM is over confidence now, but totaly unsure for the presidency position of 2015 unless they form coalition with likeminded Political parties....at the same accepting not to appoint any candidate to areas where otherlikeminded Opposition Parties have got mass support....otherwise MPs and Concellors will increase with no impact to Presidency post...count my lips.
 
Hii M4C ni moto sana, na CDM sio walipata wapi hayo maono kwa kweli.
Na kwa civic educatioin wanayotoa, hapo magamba wanatamani sijui nini kitokee ili wanusurike.
sasa angalia, Mama kasafiri bure, na hela ya faini kapewa (kama alichelewa) na ya kula kapewa na hata nauli za watoto wake kwenda shule, na chenji juu.

We hushangai wananchi kulipa nauli na kutoa mchango juu? Imezoeleka harusi tu kuchangia, sasa magamba ni lazima wahagaike kwa sasa, elimu mliyoiondoa mashuleni sasa inarudi mtaani, mtu ajue kuandika ama asijue, bado wananchi wanaeleweshwa kwa lugha rahisi sana katiba ni nini na ushiriki wao katika demokrasia unatakiwa kuwaje.

Haya, kuna counter attack mnataka ku-suggest? hasa baada ya ile ya kujivua gamba kufeli?
 
Huyo mama ni mfano bora kama rais Joyce wa Malawi; hapa Arusha-Ngulelo nilishuhudia mzozo wa dada mmoja kusongwa kwanini amempiga mwenzako kofi? ugomvi eti alimpigia diwani wa CCM kura Kundi la wasuluhishi liliamua aliyepigwa ni mjinga kwa uzembe wa kumpigia diwani wa CCM. Akina mama hao kwa lafudhi ya kimasai walimalizia na ukome na li-CCM lako.
 
Nimesoma kwa makini sana commemts za wanaJF mwisho nimegundua kwzmba mabadiliko ni lazima. Tupo pamoja.kwamba
 
napendeza sana kuona watu wa kawaida kabisa wameguswa na kiu ya kutaka mabadiliko. Yes something is there na hata hapa kazini kwangu bosi wangu naona kama ameanza kulainika hivi. Bosi kwa hali ilivyo huyu mtu hana shida yoyote eti, anaingia vikao vingi na maposho kibao, lakini juzi hivi nimemwona kama analalamikia sana uongozi wa serikali kwa jinsi hali ya maisha ilivyo;

Wale wanaodai kwamba Dodoma, Morogoro, Kusini au Pwani watu hawataki mabadiliko inawezekana ikawa kweli. Lakini cha kujiuliza ni kwamba hivi hawa watanzania wenzetu wana maana kwamba wao maisha kwao ni mstari na maeneo hayo kumejaa maziwa na asali hivyo mabadiliko siyo ya lazima kwao? Sawa ngoja tuone hawa wenzetu wanawaza nini.
 
La kushangaza jana nilikuwa naongea na ndugu yangu mmoja huko Tabora (ambao waliichagua CCM) akanishangaza kwa kusifia sana CHADEMA, kinyume na nilivyotarajia; kuwa Igunga ilikuwa ni mvua za rasharasha, na itakapofika Tabora mjini basi itakuwa ya mafuriko. Sijui zile kampeini za Igunga zilisaidia kuwaamsha ndugu zangu.
 
Kweli huyu Mungu atabaki kuitwa Mungu, Viva cdm.
Tolerance gives power
solidariry forever..\/
 
4sur cjashangaa kuskia MWANZA na CHADEMA,umenikumbusha mmama mmoja alishushwa kwenye gari na nguo kuchanwa kisa 2 alijifanya anamte2 MASHA alivyidondoshwa na WENJE...........CHEZEA CHADEMA WEWE TENA MWANZA PEPOOOOZ POWEEEEEEER MR PINDA APENDI!
 
Duh, hata mimi ningekuwepo kwenye hiyo Dala dala, ningemchangia huyo Mama! Wao wana Jeshi, Mahakama na Polisi ila sisi tunae Mungu! M4C 4ever.
 
Ni kweli kuna visa vingi vya namna hiyo sema vingine huwa haviripotiwi humui ndani. Kuna msiba ulitokea Mbeya wa fundi cherehani binti ambaye alikuwa m/chama wa CDM. Kwahiyo yale mazishi yalisimamiwa na makamanda wenzake, shughuli ikawa kwenye kupika chakula, dada yangu alikuwa mmoja wa wapishi, unajua kina mama tena, ile kuchukua labda nusu kilo, mafuta kidogo, chakula kidogo ili kuwapelekea watoto nyumbani si unajua umaskini wa Kitanzania. sasa hapo ndipo ilikuwa shughuli wale kina mama wenyewe walianza kuelezana jamani kwenye huu msiba asijidanganye kuiba chochote mtu hapa, hawa CHADEMA wanapingana na wizi kama kuna mwenye shida hiyo awaombe watampa lakini kuiba italeta shida.
Picha ya haraka unaona watu wa chini wanavyoweza kusoma mwenendo wa Chama flani, hivyo CDM haya yanayotokea kazeni kamba hapohapo kitaeleweka tu
 
Back
Top Bottom