Kweli CHADEMA wanapendwa hivi au Macho yangu!?

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,536
2,187
Imetokea jana kwenye Dala dala la Kutoka Airport kwenda Buhongwa (MWANZA), Kama kawaida ya konda ndani ya dala dala anadai chake (Nauli), kabla hajamaliza kudai nauli gali likakata mafuata kiaina (likawa linazimika zimika), ikabidi dereva aingie sheli kuongeza mafuta.

Hatujajua kinachoendelea akainuka mama mmoja kwa asila na kumkoromea konda na dereva, akisema: Mambo ya kutembea na Mafuta ya vidumu mnatuchelewesha kwenye vikao na ntaenda kupigwa faini kwa kuchelewa Tsh. 5,000/=: Mara jirani yake akadakia, Kikao cha nini? Mama akajibu: Kikao cha chama, kwa mshangao wa wengi, kila mmoja alidhani labda kikao cha wakinamama au SACCOS: Mama akadakia tena: Kwenye kikao cha chama cha CHADEMA!

Nkiwa bado nashangaa abiria wote wakadakia: Kama ni kikao cha CHADEMA, tutakuchangia iyo faini, nilidhani kama utani! Kwanza yule konda akamwambia yule mama: wewe ni mjanja, akamrudishaia nauli yake, nkiwa naendelea kushangaa, konda akaanza kukusanya michango kwa ajili ya yule mama. Amini usiamini alichangiwa Tsh. 32,500/=. Chakushangaza zaidi hata watoto wa shule walimchangia yule mama.Nilibaki kushangaa mwanzo mwisho!

Naanza kuisi mabadiliko, kweli hapa Mwanza si mchezo.

Ni mimi nisiyekuwa mwanachama wa chama chochote kwa sasa.
 
Hiyo ni kali na Bado,Kwani watu wameamua kufanya kweli hakuna wa kuwazuia.
 
Mimi naona kasi kubwa imeanza mapema mno, sasa wajipange vizuri kudhibiti usukani kabla ya 2015.
 
Nilishawahi kusoma Comments humu Jamii Forums za Mikaeli Aweda (Mjumbe wa Baraza kuu taifa CHADEMA), aliandika linapokuja suala la utekelezaji wa kazi za Chama Dr Slaa hana mzaha na mtu, na akaendela kusema alichelewesha kuwasilisha report, Dr Slaa alimfokea na kumpa onyo kali(samahani kama nitakua nimenukuu vibaya), kwahiyo kama system ya utendaji wa Chama ipo chini ya Dr Slaa, hili la huyu Mama kusema kwamba akichelewa ataenda kupigwa faini nalikubali moja kwa moja
 
Peoples power. M4c

Yeah...this is good news, you see, things have really changed, citizen of now days are quite different from those in past, that's why ccm MUST GO TO HELL BY 2015....

Measures to eliminate CCM in our country have to be taken seriously, not by our leaders in CDM but by ourselves with our own little money we have and everything little we have......
TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED......YES WE CAN....GOD BLESS CDM...
 
safi sana jamani hii ndo tanzania na mabadiliko yake ndo hayo lazima tuwasaupport chaema watulete maendeleo na mimi ningekuwepo ningetoa zaidi ya hiyo iliyochangwa hapo
 
Dah!!!!!!!!!! Nimefurahije? Mpaka moyo unataka kulipuka kwa furaha. M4C Forever, ili mradi akina mama wameshaamua ndo bac CCM kwishney!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom