Kweli CCM hakuna mbunge

Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,328
955
Nimemsikia mh. Livingstone akihojiwa akasema anashangaa mama ntilie kuwa na laini nne wakati yeye ni mbunge na ana laini moja, akasema tuishi kulingana na kipato, je kwa kauli hiyo amezingatia maisha halisi ya mtanzania?
 
Mh. Lusinde, kuwa na laini nne, si kuongeza matumizi! wanaofanya hivyo wanataka kubana matumizi. Kwa taarifa yako ukimpigia mwenye laini ya tigo kwa tigo, gharama ni nafuu zaidi kuliko kutumia laini tofauti hivyo hivyo kwa laini nyingine. Ila kwako wewe mwenye kipato "kikubwa" ndiye usiyeliona hilo!
 
Nimemwona kwanza alikuwa anaogopa hata hiyo microphone, hajaongea kitu zaidi ya kubwabwaja kama kawaida yake, kidogo aseme kudadadeki.
 
Huyo ndiye mbunge tunayemsubiri achangie bajeti yetu ya mwaka 2012/2013
 
Nimemsikia mh. Livingstone akihojiwa akasema anashangaa mama ntilie kuwa na laini nne wakati yeye ni mbunge na ana laini moja, akasema tuishi kulingana na kipato, je kwa kauli hiyo amezingatia maisha halisi ya mtanzania?

Hayo ni matatizo ya kufikiria kwa kutumia masaburi hajui mama ntilie lazima awe na laini zaidi ya moja ili iwe rahisi kuwasiliana na wateja wake wanaotumia mitandao tofauti,hao ndo wabunge wanapiga meza bila sababu za msingi
 
Kabisa maana anachokifikiria ni ***** tu, cha ajabu kati ya wachangiaji wa bajeti na yeye atakuwa mmoja wao
 
Back
Top Bottom