Kwaya ya CCM yahamia CHADEMA

Uongozi mbaya ndo unaiua CCM, mzee wao yeye kazi kuzurura tu nchi za nje na mawaziri aliowaweka si watendaji sasa anategemea nani atakayesimamia? kweli nimeamini ndo maana mikoa mingi ya Puani haina maendeleo kumbe tatizo ndo hilo. Yahani jamaa anaua chama na nchi pia anaiua. Haya msubiri kuokota mipira kwenye nyavy

Chama cha magamba kilishaingizwa ICU tangu Azimio la Zanzibar. Rushwa, ufisadi, utawala wa kupendeleana ni fimbo za mwisho mwisho ili chama kikate roho.
 
Kesho utasikia na kuona bendi ya ccm ile ya Komba yahamia chadema, mara filikunjombe na mwisho lowasa na jk wahamia chadema! Pipoooooooooooooooz!...
filikunjombe AJE .....KOMBA KUFILIA MBALIIIIIIIII... KWANZA SIO REAL COMBATANT!
 
mmh,kwaya tena?
Si ndo yale yale ya kuanza kuchezewa ngoma kabla ya hotuba
au kukagua maendeleo?

Waingie kama wana chama tu,kucheza ngoma na kuimba imba
kwaya za ajabu hakuna mda sasa,time is money.

Good observation- angalizo jema kabisa! Nchi haihitaji tena ngonjera, tunataka kazi!
 
Tunawakaribisha sana lakini wasitegemee ubwabwa na kanga kwetu. Sisi huku tunachangia Chama tuleta ukombozi, hatupo kwa ajili ya pesa. Natumaini wamekuja kwa moyo wa kukomboa nchi yetu

Kabla ya kuhamia CDM walijua ubwabwa haupo, kwa hiyo wamejiunga kuikomboa nchi.
 
Katika hili mimi sishangai na wala sitashangaa kuona hata viongozi waandamizi wakihama CCM na kujiunga CDM, unajua watu wengi walio ndani ya CCM dhamira inawashtaki kwa maovu wanayoendelea kuwatendea wananchi na hali mbaya iliyoko nchini kutokana na uongozi mbovu wa CCM. Wana JF mimi ni mwana-CCM kwa kadi niliyonayo lakini ndani yangu mimi ni mwana CDM. Ukweli ni kwamba Mtaji mkuu wa CCM ni ujinga wa watanzania lakini kadiri siku zinavyoenda ndivyo tunaona uelewa unaongezeka miongoni mwa watu na matokeo mnayaona. Nashukuru kwa kuanzisha shule za Kata nchi nzima, napenda niwambie ukweli kama kuna watu waliofika kuanzia kidato cha pili na kuendelea ambao ni wana CCM basi si zaidi ya 10%.

Nadhani kwaya hii itasaidia sana maana wamechoka kuimba kwa unafiki sasa wataimba kwa moyo na kwa kumaanisha hebu tuwatie moyo na ikibidi vifaa vyote vya CCM wasichukue hata kimoja alafu waanzishe mfuko tuwanunulie vyombo vya kisasa waanze kazi. Ogopa Nguvu ya UMMA, I Love CHADEMA
 
Jamani huku ughaibuni kuko very stressful. Ila watanzania ni watu wa aina tofauti na watu wa nchi nyingine. Sisi huwa ni watu ambao hatuchelewi kukubwaga ukileta za kuleta. Nimecheka sana!!!!
 
Du nilisema juzi kuwa mfungo wa lema bado haujaisha hadi wiki ijayo

Bado tunasubiri ila matokeo yanmeeanza kuonekana
 
Tunawakaribisha sana lakini wasitegemee ubwabwa na kanga kwetu. Sisi huku tunachangia Chama tuleta ukombozi, hatupo kwa ajili ya pesa. Natumaini wamekuja kwa moyo wa kukomboa nchi yetu

nilikuwa sijafurahi toka jana, umeifanya siku yangu kuwa poa kwa maneno yako
 
Ninaifahamu vizuri sana hiyo kwaya, ndio ilikuwa tegemeo la ccm wilaya ya magu katika kampeni zao. HUU NI USHINDI KWA WANA CDM WILAYA YA MAGU WANAO TAKA MABADIRIKO.
 
Ninaifahamu vizuri sana hiyo kwaya, ndio ilikuwa tegemeo la ccm wilaya ya magu katika kampeni zao. HUU NI USHINDI KWA WANA CDM WILAYA YA MAGU WANAO TAKA MABADIRIKO
 
Chadema ilianza na Mungu harakati za kuing'oa CCM na itamaliza na Mungu.
CCM walianza harakati za kumnyonya Mkulima wakitumia nguvu na ulinzi usioonekana wa Sheikh Yahya Hussein na wanamaliza na mganga Maji Marefu
 
mmh,kwaya tena?
Si ndo yale yale ya kuanza kuchezewa ngoma kabla ya hotuba
au kukagua maendeleo?

Waingie kama wana chama tu,kucheza ngoma na kuimba imba
kwaya za ajabu hakuna mda sasa,time is money.
...naunga mkono hoja...CHADEMA hatuna muda wa kuchekeshana,hapa ni kazi tu mpaka kieleweke...
 
Grraph ya ccm inazidi kushuka kwa kasi....
Wapenda ukombozi wa nchi hii tuzidishe maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu azidi kutusafishia njia ya kuelekea ukombozi.
Kumbuka jinsi Mungu alivyomsimamia Musa kuwaongoza Wana Waisraeli jangwani kwenye shida nyingi kuelekea katika nchi ya ahadi.
Tusisahau katika maombi yetu kumsihi Mungu aisimamie CDM ili iweze kutuongoza vyema katika safari hii ya kuelekea Tanzania yenye neema!
 
Kwaya ijulikanayo kama Kwaya ya Ng'ombe ya Magu Mjini Mkoani Mwanza yenye watu 45 imejiengua CCM na kuhamia CHADEMA jana jioni. Wanakwaya hao wamepokelewa jioni na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Magu ndugu Katinde aliyeongozana na Katibu wa CHADEMA Jimbo la Magu mjini Bahati Simon.

Hii ilikuwa ni Kwaya waliyoitumia sana kwenye kampeni na kwenye kila matukio yao na vifaa vyao vyote vya muziki vilitunzwa kwenye ofisi za CCM wilaya ya Magu. siku mbili kabla ya kuhamia CHADEMA walitafuta kambi ya muda na wakatunga nyimbo za kumsifia Dr. Slaa ambaye atafanya ziara hivi karibuni wilayani Magu

source HAPA
 
Back
Top Bottom