Kwasasa ndio tusemaje?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Wakati naanza shule ya msingi,niliaminishwa na kuamini kuwa wanafunzi wanaosoma Shule za Serikali ndio wenye 'akili' kuliko wale wa shule za binafsi.Nikaendelea kuamini hivyo hata nilipoanza Sekondari hadi kumaliza kwangu.Nilijivuna kwakuwa tangu chekechea hadi Chuo Kikuu nimesoma Shule na Chuo Kikuu cha Serikali.

Wakati huo matokeo ya kidato cha nne au sita yakitoka,mchuano ulikuwa ni Mzumbe,Ilboru,Tabora Boys,Kilakala,Msalato,Kibaha,na shule nyinginezo za Serikali.Sasa mambo yamebadilika. Shule za binafsi(hasa za kidini) zinazifunika za Serikali.Tunaruhusiwa kusema kuwa sasa wanafunzi wenye 'akili' wako shule za binafsi? Tujadili...
 
kweli bora ccm iondoke isiendelee kuiba pesa za wananchi, maana wanafanya mashindani ya kuiba pesa za wanyonge.
 
Back
Top Bottom