Kwanza badilikeni Wenyewe

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Ukitembelea hii mitandao na midahalo mbali mbali inayoendelea haswa sehemu ya afrika ya mashariki utaona kwamba wengi wanaochangia mijadala na midahalo hii ni watu ambao wanaonekana wataka mabadiliko mimi nawaita wana mabadiliko haswa vijana .

Hawa wanabadiliko siku zote za maisha yao wanataka mabadiliko lakini unapoamua sasa tuonane ili tuweze kuunganisha nguvu zetu ziwe moja kwa ajili ya kuandaa rasimu mbali mbali za kuanza mabadiliko haya ndio utashangaa watakaokuja ni wachache tu sio lile kundi la watu 100 waliokuwa wanalilia mabadiliko

Ukiuliza kwanini utaambiwa walikuwa busy na kazi maofisini , wengine wameenda kutembelea jamaa zao huko walipo tena kwa vijana utasikia mimi niko bar Fulani njooni hapo ( anataka mkaongelee mabadiliko kwenye bar ) mwingine utasikia ameenda kwenye vikao vya harusi , mwingine utasikia ameenda kwenye send off mara harusi hizi zote ni sababu

Kesho yake sasa atakuja tena analilia mabadiliko mabadiliko , mimi nawaomba wapenda mabadiliko kwanza wabadilike wenyewe huko walipo kwanza , kuanzia makazini kwao , majumbani kwao , mitaani , mashuleni na sehemu mbali mbali tulivu ambazo wanatembelea kwa ajili ya kukutana na jumuiya kubwa za watu

Kwenye wapenda mabadiliko hawa kuna walimu , wewe mwalimu hakikisha unafundisha wanafunzi wako vizuri waje kuwa wasomo bora na viongozi wazuri huko mbeleni pia na wewe ungana na walimu wenzako kutetea na kuimarisha maslahi yenu kama walimu hatakati hizi fundisha mpaka watoto wako na wanafunzi unaowafundisha

Wewe kama ni mhandisi hakikisha unafanya kazi kwa uaminifu na kwa uzalendo zaidi katika kuleta maendeleo kwenye jamii husika , wanafunzi wanaofundishwa na huyo mwalimu siku moja wanaweza kuja kufanya kazi na wewe , wewe uwe kioo cha jamii kwa yale uliyoyafanya kama mhandisi

Kama wewe ni msanii hakikisha unatumia sanaa hiyo vizuri zaidi jiboreshe kwenye ulimwengu wa sanaa , uwe kioo cha jamii , imba mashairi mazuri na ya kuvutia ya kujenga jamii , mwalimu atakutolea mfano kwa wanafunzi wake , mhandisi anapotaka kufungua jengo lake anaweza kukuita ukatumbuize wageni waalikwa na kuburudisha pia .

Kwa viongozi nao wanajua jukumu lao kwa wale watu ambao waliwachagua kuingia kwenye nafasi hiyo pamoja na wengine ambao wamechomekwa tu kwenye nafasi hizo , wote wanatakiwa kujua kwamba yule mwalimu hapo juu alitumia muda mwingi sana kuwaelimisha wakati wa udogo wao , wahandisi walijenga nyumba zao na barabara zao walizotumia kwenda mashuleni na sehemu zingine walisikiliza wasanii wa muziki kipindi walipokuwa katika burudani au hata wametulia walisoma makala na maandishi mbali mbali za mwandishi

Naamini sasa vijana huko mliko mtaweza kufanya mabadiliko yenu wewe mwenyewe sio lazima tukutane kwenye vikundi na sehemu zingine za wazi , ikilazimika hivyo ni sawa inawezekana lakini mapinduzi anzeni huko majumbani kwenu , mashuleni , makazini , mitaani na katika vyumba vya habari .

Jioni njema
 
Nashukuru sana SHY kwakuliona hili,tunatakiwa badilika kwaajili ya mabadiliko tuyatakayo,sio kupiga mayowe wakati kimatendo tunapwaya,nashukuru kwa kuwaamsha wabadilikaji!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom