Kwanini Zitto na Lowassa wanapotajwa kuhusu urais kelele zinakuwa nyingi?

Ntaramuka

Senior Member
May 2, 2008
169
27
Kwa nini habari yoyote ya ndugu hawa kuhusu kugombea urais hupigiwa kelele sana? Je, hawafai au wanaogopwa na mahasimu wao wa kisiasa?
 
zitto anatamaa sana pamoja na lowasa sisi chadema tulishasema rais ni DR SLAA sasa sijui zito analeta wapi propaganda au katumwa nini na mafisadi kuharibu chadema
 
zitto anatamaa sana pamoja na lowasa sisi chadema tulishasema rais ni DR SLAA sasa sijui zito analeta wapi propaganda au katumwa nini na mafisadi kuharibu chadema

So, kelele kwa Zitto ni nini hasa? Ni kwa sababu ana tamaa au haaminiki Chadema? Lkn ana haki ya kugombea, ndugu!
 
hawa ni viongozi wana maamuzi magumu wanachojali ni maslahi ya wengi na sio kama kikwete ambaye by nature is not a leader at all alichaguliwa kiushabiki tu lakini lowasa akipata uongozi lazima atamtumia zitto na zito akipata urais lazima atamuhusha lowasa ni wachapa kazi wanaakili ya uongozi
kwa nini habari yoyote ya ndugu hawa kuhusu kugombea urais hupigiwa kelele sana? Je, hawafai au wanaogopwa na mahasimu wao wa kisiasa?
 
wote hawa hawawezi kukubali akili ndogo kuongoza akili kubwa sababu wanaona mbali saaana
kwa nini habari yoyote ya ndugu hawa kuhusu kugombea urais hupigiwa kelele sana? Je, hawafai au wanaogopwa na mahasimu wao wa kisiasa?
 
zitto anatamaa sana pamoja na lowasa sisi chadema tulishasema rais ni DR SLAA sasa sijui zito analeta wapi propaganda au katumwa nini na mafisadi kuharibu chadema

Hamna demokrasia nyie..mnatuogopesha namna hii...eti "tumeshasema rais ni dr Slaa"...hawezi pingwa ndani kwa ndani? nini maana ya demokrasia kwenye jina la CDM sasa?
 
si kelele tu hata ngumi, hatuwezi tawaliwa na wabadhilifu wakati watu waadilifu wapo full stop
 
Kwa nini habari yoyote ya ndugu hawa kuhusu kugombea urais hupigiwa kelele sana? Je, hawafai au wanaogopwa na mahasimu wao wa kisiasa?
Haya ndio majembe kabambe yaliyobaki TZ, na wana misimamo ndani ya vyama vyao hawataki upuuzi wa ajabuajabu na ndio maana ndani ya vyama vyao wanapigwa vita sana na kuchafuliwa ila tukimpata mmoja kti ya hawa tutaweza songa mbele ktk nchi yetu. Siangalii chama naangalia Mtu
 
Kwa nini habari yoyote ya ndugu hawa kuhusu kugombea urais hupigiwa kelele sana? Je, hawafai au wanaogopwa na mahasimu wao wa kisiasa?

Heshima kwako mkuu!
Kelele ambazo tunampigia mhe. Zitto kabwe si kutokana eti na yy kugombea urais bali ni imapact za long term effects ambazo Zitto kuna mambo mambo mengi amekuwa akiyafanya na kusababisha kutoaminika kabisa kwa watu sema tu baadhi ya watu wanajifanya hili jambo hawalioni na kuanza kumtetea Zitto.

Lakini kama kweli ww ni mtu makini na umefatilia siasa kwa kipindi cha mda mrefu sasa epecially ktk nyendo za Zitto basi hautapata shida kujua ni kwann Zitto anapondwa sana na wanachama wa CDM kwani matokeo ya yale aliyoyapanda hapo mwanzoni.
 
Hamna demokrasia nyie..mnatuogopesha namna hii...eti "tumeshasema rais ni dr Slaa"...hawezi pingwa ndani kwa ndani? nini maana ya demokrasia kwenye jina la CDM sasa?

hapa ndipo mimi napata shida sana napoona nyie pro-ccm mnampigia debe zitto na kumkataa Dr.slaa.
 
Lowassa yuko makini. Hajawahi kutangaza nia.
You cant compare Lowassa with zitto in political strategies and timings.
 
Kwa nini habari yoyote ya ndugu hawa kuhusu kugombea urais hupigiwa kelele sana? Je, hawafai au wanaogopwa na mahasimu wao wa kisiasa?

Mtu anayefaa kuongoza na mwadilifu huwa hana tamaa ya uongozi na wala hajipigì debe bali hushauriwa na watu wenye hekima kugombea. Kwa bw mdogo Zitto ni wazi kuwa ana tamaa ya madaraka na si muadilifu kama anavyojaribu kuuaminisha umma.

Mtu mwadilifu hafanyi mambo kwa ushabiki wala kwa kuangalia maslahi yake kisiasa au kiuchumi, mtu muadilifu huzingatia utaratibu katika kufanya mambo yake na si kama anavyotangaza nia kabla hata ya muda ambao chama chake hakijatangaza.

Hafai kuwa rais kwani ana jazba na visasi, na mnafiki kama alivyo rafiki yake aliyeko state house kwa sasa. Namkubali kwa nafasi yake ya ubunge na si kwa uwaziri wala urais
 
Ndio lowasa ana uwezo mbali sana zaidi ya zito ila wote wana tamaa ndio wataoiharibu nchi yetu kwa kuleta makundi kwenye vyama vyao,hawatufai kabisa kabisa japo lowasa sasa anajisafisha makanisani na pesa zake na zito anajitafutia umaarufu kwny vyombo vya habari,TUSIPOKAA SAWA RAIS AJAYE ATAKUWA BOYA ZAIDI YA YA BABA LIZI
 
Kuna kitu inaitwa PETERS PRINCIPLE na hii inasema kuwa mara nyingi tunampandisha mtu cheo kuelekea ngazi ya juu kabisa ya UDHAIFU wake,yaani YOU ARE PROMOTED TO THE HIGHEST LEVEL OF INCOMPETENCE!
Waheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na Edward N. Lowassa ni viongozi mahiri lakini kila mmoja wao anahitaji BOSI wa kumwonyesha njia maana kwa kimbelembele na tabia zao za kusaka umaarufu wA rejareja wana uwezo mkubwa wa kuvuka mipaka ya kazi na kusababisha maafa hata hasara.
Kwa nia ya kutoa mfano raisi wa sasa asingejulikana kama ni dhaifu iwapo angeishia kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.Mzee wa Monduli pia angekuwa SAAAFI asingepelekwa nafasi ya WM.Zitto pia akupanda zaidi ya hapo hadi kufikia Mwenyekiti wa CDM andaeni hitima ya CDM!
Nawasilisha nasimama kukosolewa na kufundishwa,maana hii Peters principle ni kitu halisia sana
 
Zitto kwa nini asisubiri muda muafaka wa kutangaza nia kulingana na matakwa ya chama chake? Lowassa haina taabu alishapanga kupokezana kijiti na JK
 
Back
Top Bottom