Kwanini waziri wa elimu na serikali hawataki kiingeleza kisifundishwe toka std one?

Chamkoroma

Senior Member
Sep 6, 2010
186
11
Jamani wana mtandao nisaideni kwanini nchi yetu isibadilike kielimu kurundisha kiingereza toka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu?
Mimi ni moto wa mkulima nilibahatika kupata kazi nchi za nje kweli nimekuta wa kenya wanafanya kazi kila sector hapa nilipo lkn wa TZ ni wachache sn na waliopo aidher wa toto wa Ngasongwa{mfano} na wengineo , nilipata bahati ya kukutana na kiongozi mmoja mkubwa nikamuuliza sababu ya kuacha kiingereza akasema tutaharibu utamaduni wetu, jamani hiyo hoja ya utamaduni ni sahihi? nawaambia ole wao mwana wa mkulima ashike nchi nawaambia tutafaidi wengi, baadhi ya wa unge walianza kulalamika kuwa wa kenya wamezidi sn kwnye hoteli zetu za mbugani je wao kama wa bunge kwa nini wasiamue kuanzaia sasa mitaala yote ya kibongo toa tuingie kwenye ushindani wakielimu?
 
Mimi Mkenya halisi, na kama mnavyojua, sisi hufunzwa kingereza kutoka darsa la kwanza hadi chuo kikuu. Utashangaa kuona wengine wetu ambao tunajuvunia kiswahili sana hadi tungetaka kuondoa kingeereza kama lugha rasmi hapa Kenya na badla yake Kiswahili, maana hatuoni hoja ya kuongea lugha za watu wengine ilihali lugha yetu inaziidi kudhoofika. Siku hizi, wakenya wengi huongea kiswahili kibovu kabisa, bila msamiati na makosa mengi ya lugha (bila shaka naamini nimefanya makosa kadhaa tayari).

Mimi ningeshauri ya kuwa, hata ingawa ni vizuri kuongea lugha kadhaa, tusipoteze mwelekeo na kirithi lugha za wazungu badala ya kutunza lugha yetu. Mwenye anaotaka kukisoma Kiingereza anaweza kufanya hivyo kupitia private tution ama kuhudhuria taasisi zinazoshugulika na mafunzo ya lugha.
 
,
Wewe usingeshauri kwa sababu unaona unajua kuuza nchi yako nje kwa ligha ya wazungu, nakuambia ukikaa nyumba isiyona madirisha utakufa kwa moshi wakupikia chakula chako mwenyewe, TZ c nchi kama China, itachukua muda mrefu sn nakuwa na viongozi wabunifu na wenye uchungu na nchi kuweza kujitegemea, na pia hakuna nchi duniani inayoweza fanya mambo yake yenyewe bila bilateral, mnajua jinsi Kenya inavyopokea hela toka kwa watu wake kujenga uchumi wa nchi yao, nawaambia kuwa bial kukubali kubadilisha mfumo tulionao tujuwe wazi kuwa hatuna sababu yakuingiza ushindani wa kibiashara katika nchi yetu.
Lazima tubadilishe mfumo wetu wa kiswahili sanifu cha chumbani tuongee kiingereza sanifu cha uwanjani kwenye ushindani wa kimaisha.
 
Globalization inatudai tuwe na uwezo mkubwa wa kuwasiliana na watu wa mataifa mbalimbali - vinginevyo tutabaki nyuma.

Kiswahili peke yake sio silaha mashuhuri kwa mawasiliano ya kimataifa. Kiingereza cha kusuasua pia hakisaidii vya kutosha. Inatupasa tulivalie njuga suala la kufundisha vizuri kiingereza, kuanzia mwanzo wa elimu rasmi.
 
Back
Top Bottom