Maskini milioni 2.5, looh! hawa jamaa yaani wanadanganya kila kitu.

Maskini Tanzania ni zaidi ya milioni 30, wenye unafuu wa angalau kuwa na uhakika na mlo kwa mwaka mzima TZ hawazidi milioni 10

Nafikiri ni idadi ya kaya (households) maskini ndo 2.5 million!
 
Mzalendo,
Nami nilielewa hivyo kuwa hiyo 2.5M ni idadi ya familiya maskini na sio idadi ya watu maskini.

Pamoja na yote kuna ya kujifunza kwa huo ushauri wa Prof Yunus.
 
Wana JF,

Kuna ndugu mmoja amenitumia hii makala via e-mail. NAomba tuisome na kuitafakari

WHY IS OUR COUNTRY POOR?

Dear Readers,

Here is a good article sent by Dr. Arsenio Martin of Fort Arthur , Texas .
Enjoy reading.

The difference between the poor countries and the rich ones is not the age of the country:

This can be shown by countries like India & Egypt , that are more than 2000 years old, but are poor.

On the other hand, Canada , Australia & New Zealand, that 150 years ago were inexpressive, today are developed countries, and are rich.

The difference between poor & rich countries does not reside in the available natural resources.

Japan has a limited territory, 80% mountainous, inadequate for agriculture & cattle raising, but it is the second world economy. The country is like an immense floating factory, importing raw material from the whole world and exporting manufactured products.

Another example is Switzerland , which does not plant cocoa but has the best chocolate of the world. In its little territory they raise animals and plant the soil during 4 months per year. Not enough, they produce dairy products of the best quality. It is a small country that transmits an image of security, order & labor, which made it the world's strongest, safest place.

Executives from rich countries who communicate with their counterparts in poor countries show that there is no significant intellectual difference.

Race or skin color are also not important: immigrants labeled lazy in their countries of origin are the productive power in rich European countries.

What is the difference then? The difference is the attitude of the people, framed along the years by the education & the culture.

On analyzing the behavior of the people in rich & developed countries, we find that the great majority follow the following principles in their lives:

1. Ethics, as a basic principle.
2. Integrity.
3. Responsibility.
4. Respect to the laws & rules.
5. Respect to the rights of other citizens.
6. Work loving.
7. Strive for saving & investment.
8. Will of super action.
9. Punctuality.

In poor countries, only a minority follow these basic principles in their daily life.

We are not poor because we lack natural resources or because nature was cruel to us.

We are poor because we lack the correct attitude. We lack the will to comply with and teach these functional principles of rich & developed societies.

If you do not forward this message nothing will happen to you. Your pet will not die, you will not be fired, you will not have bad luck for seven years, and also you will not get sick.

But those may happen because of your laziness, your love for intrigue and politics, your indifference to saving for the future, your stubborn attitude.

If you love your country, let this message circulate for a major quantity of people could reflect about this, & CHANGE, ACT!
 
1. Ethics, as a basic principle.
2. Integrity.
3. Responsibility.
4. Respect to the laws & rules.
5. Respect to the rights of other citizens.
6. Work loving.
7. Strive for saving & investment.
8. Will of super action.
9. Punctuality.


It makes sense. We lack those qualities.
 
....ni uvivu na rushwa tuu.


Uvivu na rushwa nadhani pia ina-fiti ktk hizi principles:
1. Ethics, as a basic principle.
3. Responsibility.
4. Respect to the laws & rules.
5. Respect to the rights of other citizens.
 
Hayo yote yapo ni kweli kwa asilimia zote.
Vipi ya kuzaliana kama kuku? nadhani hiyo tunayo, ameisahau. Utakuta mtu ana watoto 5 hakuna hata mmoja anayweza kumpa maisha ya mazuri au hata kumpeleka shule. Na wengine wanaona hata sifa kuwa na watoto bastards! ni kweli.
 
Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne
1. Watu
2.Ardhi
3.Siasa safi
4.Uongozi bora
 
Hii article pia inaweza kuchangia katika mjadala huu

Ufisadi, rushwa kikwazo cha maisha bora

Dauson Harold
Tanzania Daima


JUZI kambi ya upinzani katika mkutano wao mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam, walitoa orodha ya majina ya vigogo wanaodaiwa kujihusisha na rushwa na ufisadi wakati walipokabidhiwa dhamana ya uongozi.
Sitaki kutaja majina wala kujadili kwa undani suala hilo, lakini jambo lililo wazi na ambalo nataka kulijadili katika makala hii ni suala la rushwa, ufisadi na dhana nzima ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Athari za rushwa na ufisadi katika serikali yoyote ile ni kikwazo kwa maendeleo na hata hapa nchini kadiri siku zinavyozidi kwenda, dhana ya maisha bora kwa kila Mtanzania inazidi kuwa ndoto kutokana na ukali wa maisha kuzidi kuongezeka kila kukicha.

Kila mara nawaza na kuwazua juu ya kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete wakati anaingia madarakani. Nafikiria kama itawezekana, maana kila siku wananchi wanakosa usingizi kutokana na ugumu wa maisha.

Tukiangalia mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali, ni wazi kuwa ukali wa maisha kwa Mtanzania wa kawaida unaongezeka mara dufu hasa baada ya kuanza kwa mwaka mpya wa fedha, sote tunaona jinsi mambo yanavyozidi kuwa magumu.

Ongezeko la bei ya mafuta ni jambo linalofanya wananchi kuhoji, lakini kutokana na uchumi wa nchi kukua kwa kasi ndogo na kupanda kwa gharama za usafirishaji ni wazi kuwa hali ya kipato kwa walalahoi itashuka.

Tukiangalia ongezeko hilo tunazidi kuona jinsi linavyotuathiri wengi, kwani hata Mamlaka ya Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imeruhusu kupanda kwa bei ya nauli kwa asilimia 50, imekuwa mwiba mwingine kwetu wa kipato cha chini.

Tukiangalia mfumuko wa bei ya vitu mbalimbali, tunaona jinsi Watanzania wanavyopoteza ndoto za maisha bora, kwani hii inaonyesha wazi kuwa haijulikani ni lini maisha hayo yatakuwa bora.

Wakati bei za vyakula na bidhaa mbalimbali zinakuwa juu, tunanona Mtanzania huyo kipato chake bado ni kidogo na hakiwezi kumudu gharama za maisha ya kila siku, sasa hapa maisha bora kwa kila Mtanzania yanatoka wapi?


Tunaona maandamano ya wafanyakazi, lengo lao ni kudai nyongeza ya mishahara lakini bado maandamano hayo hayajaleta mafanikio yoyote.

Masuala ambayo yanahitaji kupewa kipaumble ni pamoja na nyongeza ya mishahara ambayo itakidhi mahitaji ya wafanyakazi katika sekta binafsi na wafanyakazi serikalini.

Kutokuwepo kwa mishahara mizuri kimekuwa chanzo kikubwa cha rushwa katika taasisi za umma na binafsi kutokana na mishahara midogo isiyokidhi mahitaji ya mfanyakazi.

Wanachi wenye kipato kidogo wanashindwa kupeleka watoto shule kutoka na gharama zinazohitajika ili mtoto apate elimu ambayo iitamsaidia kuendesha maisha yake na kuondokana na ujinga.

Kwani katika taifa letu maadui wakubwa ni ujinga, maradhi na umaskini, ambapo sasa zaidi ya miaka 45 ya uhuru bado taifa linagubikwa na vitendo hivyo, ambapo watu hawana elimu, maradhi ni mengi na umaskini wa kipato kwa watu walio wengi ni duni.

Tungeona wakati bidhaa zinazidi kupanda na mishahara nayo ingeongezwa ili kukidhi gharama za kuendesha maisha, kama hatufanya hivyo, unafikiri rushwa itakwisha? Unafikiri maisha bora yatapatikana? Tutakuwa tukijidanganya kupambana na rushwa wakati bado kipato ni kidogo.

Tunaona jinsi Watanzania wa kipato cha chini wanavyoishi maisha ya shida, ambayo hata kupata mlo mmoja kwa siku ni ndoto, isipokuwa watu wenye kipato cha juu ndio wanaoweza kuishi maisha mazuri.

Tunaona hata watoto wa watu wenye kipato kikubwa katika nchi yetu ndio wanaosoma katika shule za gharama kubwa, lakini mtoto wa maskini anasoma katika shule zisizokuwa na mahitaji muhimu kwa wanafunzi kama ukosefu wa vitabu, walimu wa kutosha na wanafunzi bado wanaendelea kukaa chini.

Tunaona jinsi vijana wengi wasio na ajira na hata wale waliobahatika kupata ajira, mishahara yao ni midogo, kiasi ambacho hakiwezi kumudu hata kiwango cha mahitaji yao muhimu.

Tukiangalia maisha ya Watanzania wengi waishio mijini na vijijini bado ni duni, pamoja na Rais Jakaya Kikwete kutoa fedha za mikopo kukopesha watu wa kipato cha chini lakini bado hawajafaidika kwa mikopo hiyo.

Pamoja na fedha hizo kutolewa maarufu kama mabilioni ya Kikwete, bado fedha hizo hazikuwafikia walengwa na wengi waliishia kupewa ahadi ambazo kupata fedha hizo kwao zimekuwa ni ndoto.

Serikali ikitaka wananchi wawe na maisha bora kwa kila Mtanzania, lazima ihakikishe Watanzania wengi wanapata elimu ya kutosha, haisaini mikataba mibovu, lazima iwape wanachi kipaumbele katika kuwekeza hapa nchini, na kuongeza uzalishaji viwandani ambao utasaidia wananchi wengi kupata ajira na kuhakikisha wanapata masilahi mazuri.

Ili tufanikiwe, lazima tuwe na uongozi mzuri katika sekta zote za nchi yetu, tulinde rasilimali zetu ili ziweze kuwasadia Watanzania kupambana na rushwa na ufisadi, na tukiweza hilo, dhana ya maisha bora kwa kila Mtanzania, inawezekana.
 
4. Respect to the laws & rules

Nadhani viongozi tulioanao wakifuata hilo kwa makini, ufisadi utaisha, na kama hilo litafuatwa kwa uhakika, naamini maendeleo yatakuja!

Shida kubwa Tz ni kuwa na viongozi Miungu watu, ambao wako above the law, wanafanya watendalo, wasio shaurika na wabinafsi kupindukia! Ambao hutumia mtindo wa 'wagawanye uwatawale'

Mpaka tupate viongozi ambao wapo chini ya sheria ndipo tutajikwamua! Vinginevyo ndege imeshika kasi kuelekea kuzimu!

Poor Tanzanian!
 
Juzi juzi nilikuwa ktk mkutano wa mazingira huko Spain nikiwakilisha nchi fulani, tulikuwa wawili mimi na mwenzangu mzawa wa hiyo nchi, nchi nyingi zilizoshiriki mkutano huo utakuta zilikuwa na wajumbe wawili sana sana watatu, nilipoangalia orodha ya msafara wa nchi yangu Tanzania walikuwepo KUMI NA MMOJA (11), Prof Mwandosya akiwa Kiongozi wa msafara!!!! duuhhh!!

Mungu Ibariki Tanzania
 
Juzi juzi nilikuwa ktk mkutano wa mazingira huko Spain nikiwakilisha nchi fulani, tulikuwa wawili mimi na mwenzangu mzawa wa hiyo nchi, nchi nyingi zilizoshiriki mkutano huo utakuta zilikuwa na wajumbe wawili sana sana watatu, nilipoangalia orodha ya msafara wa nchi yangu Tanzania walikuwepo KUMI NA MMOJA (11), Prof Mwandosya akiwa Kiongozi wa msafara!!!!...............duuhhh!!

Mungu Ibariki Tanzania

Ogah,

Kwanza je, ulimsalimia Prof. Mwandosya na kumpongeza kwa kumshinda Mwang'onda kwenye kinyang'anyiro cha NEC?

Pili, je ulimtambulisha kuwa wewe ulikuwa ni mmoja kati ya watu wawili waliokuwa wanaiwakilisha nchi yako ya ughaibuni, pampja na kuwa wewe ni mbongo? Taarifa ndogo kama hizi zinasaidia sana katika kuwafundisha vibosile wetu.
 
Juzi juzi nilikuwa ktk mkutano wa mazingira huko Spain nikiwakilisha nchi fulani, tulikuwa wawili mimi na mwenzangu mzawa wa hiyo nchi, nchi nyingi zilizoshiriki mkutano huo utakuta zilikuwa na wajumbe wawili sana sana watatu, nilipoangalia orodha ya msafara wa nchi yangu Tanzania walikuwepo KUMI NA MMOJA (11), Prof Mwandosya akiwa Kiongozi wa msafara!!!!...............duuhhh!!

Mungu Ibariki Tanzania

ogah hapo umenichekesha sana;);) Duuh kweli TZ sisi wakali, halafu unaambiwa hata olympics maofisa wa-TZ wanakuwaga wengi kuliko wanamichezo, vitu vidogo kama hivi kama hatuwezi kurekebisha, je tutaweza vitu vikubwa?
 
Mheshimiwa njoo JF upate sababu:

* Asema anajiuliza swali hilo kila siku bila jibu
* Apinga fikra za siasa za ujamaa kuwa tatizo
* Aeleza mikakati ya kuimarisha sekta ya kilimo
*Akiri kuna kipengele katika madini hakimfurahishi



Na Waandishi Wetu (Mwananchi)

RAIS Jakaya Kikwete amesema haelewi ni kwa nini Tanzania bado ni fukara ingawa imejaliwa rasilimali nyingi za asili kuliko nchi nyingi za bara la Afrika.

Rais Kikwete aliyasema hayo Oktoba 4, mwaka huu mjini Paris Ufaransa katika mahojiano na Mhariri wa masuala ya Afrika wa gazeti la Financial Times, William Wallis na Mwandishi wa gazeti hilo,Tom Burgis.

"Hata mimi sielewi. Hili ni swali ambalo hata mimi huwa najiuliza kila siku, ni nini ambacho hatujafanya? Nafikiri tunaongoza barani Afrika katika kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini."

Alisema hata yeye haelewi ni kipi ambacho bado hakijafanywa ili kuifanya Tanzania kuwa katika nchi zenye maendeleo mazuri katika bara la Afrika.

"Lakini bado tunaendelea kuvutia uwekezaji katika sekta nyingine. Labda ujumbe bado haujafika vilivyo," alijibu Rais Kikwete alipoulizwa kwanini Tanzania bado ni masikini.

Alipoulizwa iwapo tatizo pengine bado ni kutawaliwa na mawazo ya kijamaa, Rais Kikwete alisema:

"Sidhani hilo kama bado ni tatizo. Uwekezaji mara nyingi unatoka sehemu moja kwenda nyingine. Labda wakati wetu utafika katika muda mfupi ujao."

Alipoulizwa juu ya utata wa vivutio vinavyotolewa katika sekta ya madini katika miaka ya nyuma, Rais Kikwete alisema hajui kama kuna utata wowote katika sekta hiyo.

Hata hivyo alikiri kuwa kulikuwa na kipengele kilichowaruhusu wawekezaji katika sekta hiyo kuendelea kudai kuwa wanapata hasara hivyo kila wanachozalisha wawekezaji katika sekta hiyo walitumia kipengele hicho kufidia 'hasara' hiyo.

Alisema kutokana na kipengele hicho wawekezaji walikuwa wakichukua chote walichozalisha bila kulipa kodi kwa madai ya kupata hasara na kwamba wenye mali (wananchi) hawakulindwa, na suala hivi sasa linajadiliwa kwa lengo la kurekebisha.

Alisema makampuni yote ya madini yamekubaliana na suala hilo kwa kuwa wameona kuna hoja ya msingi katika kumlinda mwenye mali inapotokea hasara.

Alipoulizwa iwapo anaridhika na malipo ya dola za kimarekani 200,000 kwa mwaka kama kodi kwa halmashauri migodi ilipo, Rais Kikwete alisema anakubaliana ingawa angependa malipo hayo kuongezwa ili kuwanufaisha zaidi wananchi wa maeneo husika.

Katika mahojiano hayo, Rais Kikwete alisema pamoja na kukua kwa michango ya sekta ya madini na utalii katika uchumi, msisitizo wa serikali ni kuibadilisha sekta ya kilimo ili itoe mchango mkubwa zaidi.

Alisema katika mkakati huo mabadiliko makubwa yatafanyika katika sekta hiyo kwa kuongeza kilimo cha umwagiliaji, kuongeza matumizi ya mbegu bora na utumiaji zaidi wa mbolea.

"Matumizi ya kawaida ya mbolea katika kilimo chetu kwa sasa ni ya chini mno ukilinganisha na nchi nyingine. Kwa mfano, sisi tunatumia kilo nane za mbolea kwa ekari moja ukilinganisha na kilo 577 kwa ekari zinzotumiwa nchini Uholanzi," alisisitiza Rais Kikwete.

Alisema katika mpango wa miaka saba wa kuboresha kilimo, mkazo pia unatiliwa katika kuwatumia wataalam wa kilimo kuwafundisha wakulima mbinu za kisasa za ukulima.

Aidha alisema pia kuwa mpango huo unaangalia masoko kwa ajili ya mazao yatakayozalishwa na wakulima na uimarishwaji wa miundombinu hasa barabara vijijini ili iwe rahisi kwa wakulima kupeleka mazao yao sokoni.

Mbali ya mpango huo kwa wakulima wadogo, Rais Kikwete pia alisema wanaangalia mpango wa kuwavutia wakulima wakubwa katika kilimo cha mazao ya biashara kwa kuweka vivutio vya kifedha.

Alisisitiza kuwa sekta ya utalii bado inaweza kuliingizia taifa fedha zaidi za kigeni kwa kuendeleza ujenzi wa hoteli zaidi katika fukwe na mbuga za wanyama ili kuwavutia watalii zaidi.

Katika mahojiano aliyoyafanya akiwa njiani kurejea nyumbani kutoka katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Kikwete alizungumzia masuala mbalimbali ikiwamo rushwa ndani ya CCM, vyama vya siasa nchini na utegemezi wa wafadhili katika bajeti unavyopungua mwaka hadi mwaka.

Pia alizungumzia kwa kirefu matatizo ya Zimbabwe na uhusiano katika mataifa ya Afrika na China na kuonyesha jinsi nchi hiyo ilivyo rahisi katika utoaji wa misaada ambayo haina masharti magumu kama zilivyo nchi za Magharibi na uwekezaji wa nchi hiyo katika Afrika.

Wakati huo huo, Joyce Mmasi anaripoti kwamba Rais Kikwete amesema ifikapo mwaka 2010 migodi yote ya madini nchini itakuwa inalipa kodi kikamilifu.

Rais Kikwete aliyasema hayo alipokuwa akihitimisha ziara yake ya wiki mbili nchini Marekani ambapo alikiri kuwa mikataba ya madini iliyosainiwa zamani ina mapungufu makubwa kutokana na walipa kodi kutolipa kodi ya maana.

Rais Kikwete ambaye aliripotiwa akiyasema hayo kupitia kituo cha Televisheni cha ITV cha jijini Dar es Salaam, alisema kutokana na kuwa mikataba ya zamani ina mapungufu, serikali itahakikisha inabadilisha mikataba mipya ili kuondoa mapungufu ya zamani.

"Wawekezaji wapya hawawezi kupewa mikataba kama ile ya zamani...sasa kama wapya wamepewa asilimia 15, basi hapa hakuna haja ya kuhangaika, huyo atakuwa amekiuka maagizo yangu, huyo mniachie mimi, hiyo ni kazi yangu."

Hata hivyo Rais Kikwete alisema, mipango ya serikali ni kupata asilimia 33 ya faida inayopatikana na akasema, "kama mgodi unapata dola 100, serikali itapata dola 33, hizi ni pesa nyingi na zitasaidia sana" alisema.

Alisema tayari wameanza katika baadhi ya migodi, na kuwa ifikapo 2010, migodi yote tangu ule mdogo mpaka ule mkubwa wa Bulyankulu utakuwa unalipa kodi kikamilifu.

"Tusingebadilisha hiyo mikataba, wenye migodi hiyo wasingelipa kodi mpaka mwisho wa uhai wa migodi hiyo, lakini serikali imeona na kuamua kuipitia upya," alisema.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema lazima tukubali kuwa Watanzania ni wachanga sana katika sekta ya madini na akasema ndio maana serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa haiporwi madini yake.
 
Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema, "lazima tukubali kuwa Watanzania ni wachanga sana katika sekta ya madini na akasema ndio maana serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa haiporwi madini yake."
Oh! My God!
When you have nothing important to say it is always better to keep quiet. No one in Tanzania will agree with this nonsense except few in leadership positions in CCM as well as the government.
 
sqrqmg.jpg


Hapa tuseme mheshimiwa akilia kuonesha uchungu wa kuwa maskini au vipi?
 
Kweli hawana sera how dare can u saw watanzania ni wachanga sana katika suala la madini? ina maana wakati wa nyerere hayakuwepo? alivyoamua kuyaacha kumbe nyerere alikuwa mchanga?

Suala hapa wanaotuwakilisha sisi ndiyo wachanga wapo watanzania kibao na profession zao huko Botswana wanafanya shughuli za madini kwanini wasiitwe?? au wao siyo wanamtandao??

Membe rekebisha statement hiyo la sivyo hatukuelewi.
 
Rais Kikwete ambaye aliripotiwa akiyasema hayo kupitia kituo cha Televisheni cha ITV cha jijini Dar es Salaam, alisema kutokana na kuwa mikataba ya zamani ina mapungufu, serikali itahakikisha inabadilisha mikataba mipya ili kuondoa mapungufu ya zamani.

Kwani huu wa Buzwagi, nao umerihtiwa toka awamu ya tatu, au ni mpya?
 
hapa tuseme mheshimiwa akilia kuonesha uchungu wa kuwa maskini au vipi?

"Ahadi nilizozitoa za ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya pamoja na maisha bora kwa kila Mtanzania hazionyeshi matunda yoyote...sasa sijui nifanye nini?"
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom