mtumwitu, hili la Ukraine ni kilele cha uzembe na kutokuwajibika! Unaweza kupanga vipi kuwasaidia watu milioni 38 wakati watu 29 umeshindwa? Utaweza vipi kujenga mazingira ya kuondoa umasikini wa familia milioni mbili wakati familia 29 umeshindwa? Mtumwitu, kuweza kubuni mbinu za kutatua matatizo makubwa ni lazima uweze kubuni mbinu za kuweza kutatua matatizo madogo. Asiyeweza kusiba ufa, ataweza kweli kujenga ukuta?

Ni jambo moja kusema maneno ya matumaini na ahadi za mbingu, ni jambo jingine kabisa kutenda! Binafsi ningekuwa impressed kweli kwamba kweli Rais ni mtu wa watu kama mara moja angeamua kuingilia kati au kuamuru utatuzi wa jambo hili bila ya kuliacha libishaniwe hadharani.

Asiyeweza kuaminiwa kwa kitu kidogo, anaweza kuaminiwa kwa kitu kikubwa?
 
jamani hivi tunavyopiga kelele kumbe Rais wetu hapati usingizi kwa kufikiria jinsi gani ya kuondosha umaskini wetu, hivi haya ni ya kweli au ndio usanii?

Labda, tumpe muda hadi awamu yake ya kwanza iishe 2010! Hapo tutaweza kusema kama Mkuu wetu anamaanisha au la! Hata hivyo nina mashaka makubwa maana naona kama vile kasi imepungua! TUMPE MUDA!
 
mtumwitu, hili la Ukraine ni kilele cha uzembe na kutokuwajibika! Unaweza kupanga vipi kuwasaidia watu milioni 38 wakati watu 29 umeshindwa? Utaweza vipi kujenga mazingira ya kuondoa umasikini wa familia milioni mbili wakati familia 29 umeshindwa? Mtumwitu, kuweza kubuni mbinu za kutatua matatizo makubwa ni lazima uweze kubuni mbinu za kuweza kutatua matatizo madogo. Asiyeweza kusiba ufa, ataweza kweli kujenga ukuta?

Ni jambo moja kusema maneno ya matumaini na ahadi za mbingu, ni jambo jingine kabisa kutenda! Binafsi ningekuwa impressed kweli kwamba kweli Rais ni mtu wa watu kama mara moja angeamua kuingilia kati au kuamuru utatuzi wa jambo hili bila ya kuliacha libishaniwe hadharani.

Asiyeweza kuaminiwa kwa kitu kidogo, anaweza kuaminiwa kwa kitu kikubwa?


Mkjj,

Mkuu maneno mazito hayo ...

Kwa system ya uendeshaji wa nji hii unavyokwenda, hata akipewa miaka 50 mambo yatakua hivi hivi
 
Mi nadhani haya ni maneno ya mdomoni......kusoma alama za nyakati ili umaarufu usipungue.

Hivi JK sio mchumi? Kama ndivyo, inakuwaje anakuwa na baraza kuuubwa la mawaziri (costly to manage)? Kiongozi anapoonyesha mfano mbovu, asitegemee wasaidizi na wadogo wengine wafanye miujiza. That simple.

Sifa....sifa......sifa zinamwangusha Muungwana.
 
Invicible, inabidi aende refresher course kuweza kuelewa kuwa uchumi umebadilika na dhana za uchumi tuliokuwa tunajifunza miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa tisini nyingi zimepitwa na wakati. Wale ambao tumejifunza political economy ambayo ilikuwa fundamentally ni marxist-leninist ideology leo hii tunatambua muda waliotupotea badala ya kutufundisha the so called "classical economy". Inawezekana bado katika mawazo yake Mchumi-Rais wetu bado ana mawazo ya "Primitive Accumulation of Capital"!
 
Mwanakjj, umenikumbusha mbali sana na hiyo Primitive Capital Accumulation.

JK aende refresher course? Ana tabia ya kujisomea kweli? Sifahamu katika hilo, but I doubt.

On a serious note: Nafahamu JK anataka kutambulika kama mtu wa watu. Lakini wajanja wanautumia udhaifu uliomo katika falsafa hiyo kula (bila kunawa) keki ya taifa.


Time for JK to rethink about his leadership style?
 
"Primitive Accumulation of Capital"!



Indeed, tangie tufakamie huu unyang'au kwa jina la ubepari ama soko huru....political na economic logic ya nchi yetu imekuwa ikitekelezwa kwa msingi huo................utetezi ni kuwa tunahitaji kujenga wazawa wenye uwezo wa kimtaji ile waweze kushiriki kikamilifu katika kujenga sekta "binafsi".

Tanzanianjema
 
On a serious note: Nafahamu JK anataka kutambulika kama mtu wa watu. Lakini wajanja wanautumia udhaifu uliomo katika falsafa hiyo kula (bila kunawa) keki ya taifa


"wajanjawajanja" wamemteka na hata kufikia hatua ya kum-blackmail..na yeye kwa kuwa bado anashindwa kujinasua kutoka katika fikira ya kuwa "CCM ni Tanzania na Tanzania ni CCM" amekuwa anajifunga mikono kwa kile kinachoitwa "busara za urais" na "umuhimu wa continuity"

Manyang'au wakiwemo wale "waliokubuhu" na wale "wanaochipukia" wanatumia huu mwanya kujisimika "kimadaraka" na "kiuchumi" na wengine wako mbioni kununua ufuasi, wakati huohuo wakibomoa mhimili mkuu wa uongozi wake ambao ni "imani ya wananchi"


Tanzanianjema
 
JK ni populist,na lugha za populists ni pamoja na kujifanya wana-sympathise na matatizo ya wanaotaka kuwatumia kufanikisha azma za populists hao.

Hitler na Mussolini walitumia lugha kama hizo ku-win support waliyohitaji kufanikisha azma zao za kishetani.Kitu kimoja ambacho nadhani hata wenzangu mnaweza kukubaliana nacho ni ukweli kwamba nyingi ya ahadi zinazotolewa na Muungwana baada ya kuingia Ikulu ni new versions ya zilezile alizozitoa wakati wa kampeni.

Na kwa wanaofuatilia kwa karibu kauli za huyu binadamu,watamaizi kuwa ile kauli-mbiu ya "Misha Bora kwa Kila Mtanzania Yanawezekana" imeanza kupotea mdomoni mwake na midomoni mwa wasaidizi wake.Who knows,labda baada ya mwaka mmoja wa kuwa madarakani wamebaini kuwa "maisha bora kwa kila Mtz" ni ndoto ya mchana...au pengine yameshawezekana.

Angalia bajeti iliyosomwa leo,ilinganishe na ile ya mwaka jana,na hutoshindwa kugundua kuwa kauli kuwa JK anakosa usingizi kwa namna anavyoguswa na matatizo ya wananchi ni tamthiliya isiyo na mwisho. By the way,who cares kama anakosa usingizi.

Kwani alipoomba kuingia Ikulu hakufanya tathmini kufahamu kuwa kuongoza taifa masikini kama TZ ni suala linaloweza kumnyima mtu usingizi kama kweli mtu huyo ana nia ya kuwasaidia anaotaka kuwaongoza?

Kuna maeneo ambayo tunafahamu yanahitaji muda mrefu kuyashughulikia,lakini kwenye rushwa je?Hadi leo hakuna dalili yoyote inayoonyesha kuwa Muungwana ana nia ya dhati ya kupambana na rushwa.Japo kumbukumbu za utapeli wa Richmond zinaanza kufutika lakini sote twakumbuka kauli ya JK kuwa wala rushwa anawafahamu KWA MAJINA na aliwapa muda wa kujirekebisha.Je wameshajirekebisha?Au deadline ilikuwa indefinite?Na hayo majina alokabidhiwa kayafanyia nini hadi leo.

Moja ya vikwazo vikubwa kabisa vya maendeleo katika nchi zetu masikini ni RUSHWA.Licha ya kuwaza jitihada za ndani za kujikwamua kutoka kwenye lindi la umasikini,rushwa inakwaza pia jitihada za kotoka nje ya nchi kwa vile misaada inayotolewa kwa lengo la kuwasaidia walalahoi inaishia kwenye nyumbandogo za vigogo na kupendezesha mahekalu yao huko Mbezi,Masaki,etc huku "wakitucheka" barabarani wakiwa kwenye mashangingi yao.

Asisingizie umasikini wetu kuwa ndio unamnyima umasikini,labda afya yake....
 
Kwani huu umaskini umeanza leo au JK ndiyo kaingia kwenye 'uongozi' leo? Au alikuwa anangoja hadi awe Rais ndiye auone umaskini, halafu umnyime usingizi!

Pia inategemea umaskini wa 'watu wake wapi' anaouzungumzia!
Wale watu wake wanaopiga risasi wengine au wale watu wake wanopigwa risasi?
Watu wake wanaokula Richmond au watu wake wanaolizwa na madhara ya Richmond?
Watu wake (Msolla & Co) au watu wake (Wanafunzi wa Ukraine, UDSM, etc)?
Watu wake Nchimbi na Chitalilo (elimu fake) au watu wake wa-machinga (bora elimu na si elimu bora).

Kwa wenzangu hapo juu mnaolalamikia u-rais wa JK na kasoro zake, naona mna mantiki kuwa JK aliutaka u-rais ili aweze kuutumia ipasavyo.

Je, hakuna uwezekano kuwa labda JK aliutaka u-Rais just for the sake of kuwa Rais (Wajukuu waseme kuwa babu aliishawahi kuwa Rais wa Tanzania), bila kujua kuwa atafanya nini akiwa Rais?
 
Anapaswa kujua kuwa mafanikio yake hayatapimwa kwa uchungu aliyokuwa nao juu ya umaskini bali kwa kuwaondolea watu huo umaskini!
 
mwenzenu siasa siyo fani yangu hasa, lakini hapa mmenivutia! Sitashangaa aliposema maneno hayo ya kuwa na uchungu na "watu wake" bila ya shaka waliodhania kuwa ni "watu wake" walipiga makofi. Hii kwa kweli ni tungo tata na inafaa kwenda kule kwenye kikweteisms.

Asante.
 
Badala ya kukosa usingizi aje na sera zitakazonyanyua maisha ya Watanzania walio wengi.

Kwanza kwa kuongeza ajira, kuhakikisha Watanzania wanapewa kipaumbele katika ajira badala ya wageni, kuongeza kipato chao kwa kuhakikisha wanalipwa mishahara mizuri, kuhakikisha elimu inaboreshwa kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu, kuhakikisha upatikanaji maji safi kwa watanzania walio wengi pamoja na umeme kwa bei nafuu, kuhakikisha hospitali zetu zinakuwa na madawa na vifaa vya kutosha ili kuwahudumia wabongo vizuri na pia kukipa kilimo ambachi ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania kipaumbele cha hali ya juu ili kuongeza mavuno ya mazao ya biashara na chakula na mwisho kabisa ni kuhakikisha maliasili zetu kama madini na misitu isiwanufaishe wageni tu na Watanzania wachache bali iwanufaishe watanzania walio wengi.

Lakini kukosa usingizi bila kuwa na sera za kupambana na umaskini uliokithiri kwa Watanzania hakusaidia chochote.
 
Dhambi ya unafiki watz ni lazima itutafune,wote mlikuwa mnamfahamu JK kuwa mtu wa totoz na starehe na kujichanganya na mwalimu alisema anafaa kupiga nae stori kwenye kahawa na si uraisi! leo katika uzee huu atabadilikaje ghafla! sana sana anamiss raha za makasino na totos ndo vinavyomkosesha usingizi,na kesi ya dito baada ya mtikila kuianzisha tena.
 
Umaskini wetu unaletwa na viongozi - Anne Malecela

Mbunge wa Same Mashariki (CCM), amesema watu waliopewa dhamana ya kuongoza nchi hii ndio wanaoimaliza kwa kuzidi kuitumbukiza katika janga la umaskini.

Akiongea kwa uchungu bungeni jana, Mbunge huyo, Bi. Anne Kilango Malecela, aliwakemea vikali baadhi ya viongozi serikalini wenye dhamana ya kusaini mikataba kuwa waaminifu kwa kuweka maslahi na uzalendo mbele na kumuogopa Mungu, vinginevyo watalifikisha taifa mahali pabaya.

Hali kadhalika, mbunge huyo amesema hakubaliani hata chembe na hatua ya serikali ya kupitisha moja kwa moja (fast tracking) bila ukaguzi bidhaa zote zinazoingizwa na wafanyabiashara ambao `eti` tayari wameainishwa kama wawajibikaji wazuri katika kulipa kodi.

Bi. Malecela alitoa msimamo huo jana alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha (2007/08).

Hotuba hiyo iliwasilishwa Bungeni Alhamisi iliyopita na Waziri wa Fedha, Bi. Zakia Meghji.

Akielezea suala la mikataba, mbunge huyo alisema, anaamini kwamba Tanzania siyo maskini kiasi hicho lakini kinachochangia kuiangusha, ni mikataba mibovu inayosainiwa na baadhi ya viongozi wenye dhamana hiyo ambao hawazingatii uzalendo na maslahi yaTaifa.

Kwa mujibu wa Bi. Malecela, Tanzania ni nchi ya tano barani Afrika kwa utajiri kutokana na kuwa na raslimali nyingi.

Hata hivyo, alisema pamoja na hali hiyo, bado Tanzania inaonekana kuwa maskini na kwamba umaskini huu ni wa kujitakia kwani unachangiwa na viongozi wenye ubinafsi.

`Kila anayesaini mkataba, amuogope Mwenyezi Mungu? Amtangulize Mungu wake mbele? Nchi hii si maskini kiasi hiki, ni tajiri na yenye raslimali nyingi ambayo inashika nafasi ya tano katika Bara la Afrika,` alisisitiza kwa uchungu.

Alisema Rais Jakaya Kikwete, ameonekana kuwa amedhamiria kuitumikia kwa dhati nchi yake na ndio maana amekuwa akisema mara kwa mara kuwa anakerwa sana na umaskini wa Watanzania walio wengi, lakini baadhi ya watendaji, wanataka kumuangusha.

Alitolea mfano wa Shirika la Ndege (ATC) ambalo aliwahi kulifanyia kazi, kwamba limefikishwa mahala liliko sasa ambako ni mahututi kutokana na mikataba hiyo isiyoangalia maslahi ya nchi yetu.

Alimshauri Rais Kikwete kuwachukulia hatua kali watendaji wa namna hiyo bila kuwaonea huruma. `Ukimwangalia nyani akilia, anatia huruma kuliko hata mjane na ukitaka kumuua nyani anayekula mazao yako shambani, usimwangalie usoni maana utamuone huruma,` alisema akimaanisha kwamba, Rais Kikwete awachukulie hatua kali watendaji wabovu pasipo kuwaonea huruma.

Aliwataka watendaji katika ngazi zote Rais Kikwete kutokana na jitihada zake na kila mmoja ahakikishe
anatimiza wajibu wake.

Kuhusu hatua ya serikali ya kupitisha moja kwa moja (fast tracking) bila ukaguzi bidhaa zote zinazoingizwa na wafanyabishara ambao tayari wameainishwa kama wawajibikaji wazuri katika kulipa kodi, Bi. Malecela alisema hakubaliani hata kidogo.

Alisema anaamini kabisa kuwa kila mfanyabiashara awe mdogo ama mkubwa, hufanya biashara zake kwa kutaka kupata faida kubwa zaidi siku zote.

Aliihoji serikali imenguanduaje uaminifu wa wafanyabiashara hao hata ikaamua kufikia hatua hiyo.

`Tena mmewachagua wafanyabiashara watakaopitisha bidhaa zao bandarini bila kukaguliwa eti wameonyesha kuwajibika, hivi mmeingia mioyoni mwao lini (na kuona kwamba sasa wao ni sawa na malaika?),` Alihoji na kuongeza kamwe yeye hilo hakubaliani na kuitahadharisha serikali kuwa, hatua hiyo itakuja kuleta hatari kubwa kwa Taifa.

`Mimi nasema `No`, tutaimaliza nchi sasa , eti makontena yao yakiingizwa nchini, yanapita bila kukaguliwa? Hapana, hii ni hatari. Serikali inapaswa kuliangalia upya suala hili,` aliongeza Bibi Anne Kilango Malecela ambaye pia ni mfanyabiashara.

Naye Bi. Joyce Machimu (CCM-Viti Maalum), aliitahadharisha serikali kuhusu huo mpango wa kutokagua baadhi ya bidhaa za wafanyabiashara, kwa maelezo kuwa, wafanyabiashara wengine wasiokuwa waaminifu, wanaweza kutumia mwanya huo kuingiza mihadarati nchini.


Chanzo: Nipashe

Hivi huu ushauri wa mama kilango JK atauona na kuufanyia kazi? maana yule mtaalamu aliemualika alimtaka kwanza ajipange na mama anamuonesha mistari iliokaa upande jee atamuua nyani?

Au ndio yasemwayo msanii maana na yeye ni miongoni mwa nyani mwenyewe?

Maana kuna msemo unasema: "mwache angurume simba hamli mwanawe urongo"
 
Naomba tuisomeni hii makala kwa umakini kisha tuangalie ni jinsio gani tutavyoweza kunufaika na mchango wa mtaalamu huyu.


Na Maura Mwingira

WAKATI wowote unapotekeleza mipango yako ya kuwasaidia wananchi wanyonge na maskini, usihesabu wangapi umeshawafikia, bali ni wangapi hujawafikia.

Kisha, jiwekee malengo, mwezi huu unataka uwafikie wangapi, miezi sita ijayo wangapi na miaka mitatu ijayo wangapi. Utaratibu huu ndio utakaowezesha kufanikisha yale unayotaka kuyafanya au kuwafanyia watu. Hivi ndivyo tufanyavyo sisi, tunahesabu wangapi hatujawafikia ndio tunaowafanyia kazi.?


Hayo ni maneno ya mwanauchumi maarufu duniani, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na mwanzilishi wa Benki ya Watu Maskini maarufu, Grammen Bank, Profesa Yunus Mohammed, alipokutana na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam takriban wiki tatu zilizopita.

Mwanauchumi huyo aliyekuwa nchini kwa mwaliko wa Rais Kikwete aliweza pia kufichua mambo mengi yanayohusiana na uwezeshaji wa watu maskini.


Akizungumza kwa taratibu na kwa lugha fasaha ambayo haikuhitaji mtu aliyekuwa akimsikiliza, kuwa msomi au mtaalam wa fani ya uchumi, ilikuwa rahisi kutambua kile ambacho msomi huyo alikuwa akitaka kukisema.


Profesa Yunus, kwa alitumia mifano ya wazi na inayohusu maisha ya kila siku ya mwanadamu. Kwa tafakuri ya haraka, ilikuwa rahisi kutambua kwamba lugha ile nyepesi na iliyoeleweka kwa urahisi ya msomi huyo ndiyo iliyomwezesha kuwasiliana na watu na kufanya kile alichofanya na anachoendelea kukifanya.


Nilipopata taarifa za kuwasili kwa mchumi huyu nchini, nilijawa na mshawasha hasa wa kutaka kumwona, kwa kuwa nimekuwa nikimsoma kwenye vitabu au vyombo vya habari.

Binafsi, nilikuwa mmoja wa Watanzania waliotaka na hatimaye kubahatika kumwona msomi huyo ambaye ametokea kuheshimiwa na wakubwa wa mataifa yote tajiri na maskini, hasa kwa uwezo wake kuwafanya mamia ya watu maskini nchini Bangladesh na hasa wanawake kuondokana na umaskini.

Siku ya siku ilipofika, mchumi huyo aliwasili katika Ikulu, kwa hakika nilishikwa na butwaa kidogo, kwani picha niliyokuwa nayo kichwani mwangu haikuwa ya yule aliyekuwa ameketi mbele yangu.

Nilikuwa na picha ya mtu ambaye kutokana na umaarufu wake angekuwa amevalia suti ya bei mbaya, mkoba wa nguvu na wapambe kadhaa.


Kumbe wapi, aliyekuwa ameketi mbele yangu akimsubiri mwenyeji wake (Rais) alikuwa mtu rahisi kabisa, hakuwa amevaa suti, bali vazi lake maridadi la asili ya kwao, Bangladesh .

Hakuwa na mkoba wa bei mbaya wala wapambe kibao, ila alisindikizwa na watu wawili tu ambao baadaye waligundulika kuwa walikuwa wenyeji wake hapa Tanzania.


Nje ya urahisi huo, Profesa Yunus alikuwa nchini kwa lengo la kubadilishana mawazo na mwenyeji wake, Rais Kikwete, kuhusu kitu gani ambacho anadhani na kwa uzoefu wake, Tanzania ingeweza kufanya ili kuharakisha mchakato wa kuwapunguzia ugumu wa maisha watu wake walio wengi, hususan wale wanaoishi katika maisha ya umaskini ili waweze kuondokana na hali hiyo.


Katika mazungumzo yao, profesa huyo alimweleza Rais Kikwete kwamba, katika nchi anakotoka, kiwango cha umaskini ni cha kutisha na idadi ya watu maskini ni kubwa mno ikilinganishwa na Tanzania.

Akasema kuwa amepata taarifa ya idadi ya watu maskini katika Tanzania, kuwa ni asilimia 39, sawa na kama familia milioni 2.5.

Akaeleza kuwa familia hizo ni chache mno ikilinganishwa na kwao, Bangladesh.


"Hawa mnaweza kabisa kuwaondoa katika umaskini, labda tatizo lenu ni kwamba familia hizi zimetawanyika sana kwa kuwa nchi yenu ni kubwa ambayo Bangladesh inaweza kuingia mara sita.


Kwa tathmini yangu, ninyi katika Tanzania mnayo kazi ndogo sana ya kuwaondoa watu wenu katika umaskini kwa sababu, kwanza idadi ya watu maskini mliyo nayo ni ndogo sana ikilinganishwa na kule ninakotoka."

Katika ushauri wake, profesa huyu akaeleza kuwa tofauti na ilivyo Bangladesh, Tanzania inazo rasilimali nyingi, watu wenye kujituma, serikali madhubuti kinachotakiwa ni kuongeza ubunifu kidogo tu, basi!

"Familia milioni 2.5 ni idadi ndogo sana, mnaweza kuwafikia hawa, ni kweli kwamba wamesambaa nchi nzima, lakini mnaweza, ndiyo inawezekana, kinachotakiwa ni uamuzi tu."

Akasisitiza kuwa licha ya kwamba Tanzania inazo rasilimali nyingi, kuwapo kwa fursa za mikopo nafuu kwa watu wa kawaida, ndio hasa kutakakoweza kuongeza chachu ya watu kuondokana na umaskini.

Anasema benki nchini lazima ziondokane na ile dhana kwamba watu maskini hawalipi... "Sisi tumedhihirisha kuwa watu maskini au wa kipato cha chini wanalipa mikopo. Katika benki yetu ulipaji wa mikopo ni asilimia 98 na tunakusudia kufikia asilimia 100, na nina hakika tutafika huko tunakotaka."

Anatoa mfano kwamba yeye na wenzake walipoamua kuanzisha Grameen Bank, wala hawakuanza na mtaji mkubwa.

Anaeleza kuwa walianza na mtaji mdogo lakini leo hii benki yake inao mtaji mkubwa, ambao unatokana na amana za hao maskini ambao mabenki ya biashara yanasema hawalipi.


"Wanachohitaji watu hawa maskini, wala si kiasi kikubwa cha fedha, ni mkopo mdogo tu wenye masharti nafuu sana au usio na masharti, ili waweze kuongeza tija katika kazi zao ambazo wamekuwa wakizifanya siku zote," anaeleza na kuongeza:


"?Mama anayefuma kikapu kimoja na kukiuza, anahitaji nyongeza ya fedha katika mtaji wake mdogo ili afume vikapu 10 badala ya kimoja cha awali, aviuze na kujipatia kipato, ndicho anachohitaji mtu maskini, nafasi na fursa kujipatia mkopo."


Profesa huyo akamweleza Rais Kikwete kwamba, kila mtu ni mjasiriamali hata yule ombaomba wa mitaani, tofauti iliyopo ni kwamba watu wengine walipata mapema fursa za kuwa kama walivyo (wajasiriamali) na wengine hawakupata fursa hiyo.

Licha ya wanawake wale maskini wa Bangladesh kuwezeshwa kwa mitaji na hivyo kuongeza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa zao, lakini pia anasema profesa huyo kwamba hali ya maisha ya wanawake hao na familia yao imebadilika na kubwa bora zaidi.


"Wale wanawake ambao tuliwatoa kwenye umaskini, leo wana hali bora sana ya maisha, wanazalisha bidhaa zao kwa ufanisi zaidi, wanauza, wanatunza familia zao, watoto wao wamesoma sana kuliko wazazi wao, wana ujuzi wa fani na taaluma mbalimbali.


"Hata ongezeko la watu limepungua kwa sababu sasa akina mama hawa wana shughuli zinazowafanya wajishughulishe na kuwe bize, hawana tena muda wa kupoteza au kufanya kazi ya kuongeza familia."

Kauli hiyo ilimkuna na kumchekesha kila mmoja akiwamo Rais Kikwete.

"Wazazi wao hawajui kusoma wala kuandika, lakini watoto wao, sasa wanapata fursa ya kusoma, na cha kufurahisha zaidi hata umri wa kuishi kwa wanawake umeongezea. Hii yote ni kwa sababu ya uwezeshaji tulioufanya," anaeleza.


Ubunifu huo wa Profesa Yunus wa kuwaondoa wananchi katika umaskini, hauishii kwa wanawake, bali unamfikisha kwenye kundi jingine la kijamii, ombaomba.


"Kama nilivyosema, Rais kila mtu ni mjasiriamali amezaliwa hivyo, kinacho tutofautisha ni kwamba wengine waliipata fursa hiyo mapema na wengine wakachelewa. Hata hao ombaomba wanaweza kuwa wajasiriamali wazuri sana, hilo tumelifanya kwetu na sasa wao ni mfano mzuri.


Anasimulia profesa huyo kwamba waliwakusanya ombaomba kama 100,000 hivi wakakaa nao na kuanza kuwahoji sababu zilizowafanya kuwa katika hali hiyo ya kuombaomba.


"Ombaomba wale kila mmoja alikuwa na simulizi za kusikitisha sana, wapo walioiingia kwenye shughuli ya kuomba kwa sababu ya mazingira wanayoishi. Wengine wanasema kazi hiyo imo ndani ya ukoo wao, alianza babu wa babu akaja baba sasa na yeye na kizazi chake ni kama wameirithi," anasimulia.


Ombaomba hao, Profesa Yunaus anasema kuwa baada ya kuwahoji waliamua kumpatia kila moja wao kitu cha kuuza ili badala ya kwenda kuomba, basi auze na kujipatia fedha yake mwenyewe, tena tukawaelekeza wapite katika nyumba zile zile na kuwauzia wale ambao awali walikuwa wakiomba.


"Huwezi kuamini, kati yao ni 10,000 tu ndio wamebaki wakiendelea na kazi ya kuomba, lakini kati ya hao wako ambao wanafanya biashara ndogo ndogo na wakati mwingine wanakuwa ombaomba. Lakini, wapo wengine ambao wao wameamua kubaki ombaomba kwani ni wataalam wa kazi hiyo na hawapendi kubadilika," anasema.

"Wanaume walipokeaje hatua yako hiyo ya kuwasaidia wanawake maskini, Je, ulipata changamoto gani ningependa kufahamu," akauliza Rais Kikwete."Eehe, Rais haikuwa kazi rahisi, alijibu profesa huyo na kuendelea: "Wanaume, kumbe walichukia, hawakutaka wake zao wawezeshwe, lakini sasa, wanaume wamebadilika sana kwani wamebaini kwamba faida ya uwezeshwaji ule unarudi nyumbani na kuendeleza familia.

Lakini, mwanzoni ilikuwa kazi kweli, sisi kwa upande wetu hatukukata tamaa, tuliamua kuendelea,? anasimulia profesa huyo na kisha kucheka.

Profesa huyo anaongeza kwamba tatizo la wanaume kutopenda wake zao au wanawake kwa ujumla kumiliki kipato chao si la wanaume wa nchi zinazoendelea tu, tatizo hili lipo pia katika nchi zilizoendelea.


Anatoa mfano kwamba alialikwa kwenye mkutano wa nchi tajiri na zenye viwanda, maarufu, G8 uliomalizika hivi karibuni huko Ujerumani.


Anasema kuwa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, katika mazungumzo hayo, alimweleza (Profesa Yunus) kwamba pingamizi alilolipata kutoka kwa wanaume wa Ujerumani, pale alipobainisha mpango mkakati wake wa kuwawezesha wanawake wa nchi hiyo ni kubwa mno.

Akasema kuwa Merkel alipopata uwaziri kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1980, na kuanza kuainisha mikakati ya kuwainua kiuchumi wanawake, wanaume wa Ujerumani walikuja juu kweli.

Anamnukuu Kansela Merkel akisema: ? Wanaume wa Ujerumani walifadhaika sana, unajua wanaume wa Kijerumani wanachotaka ni chakula cha moto mezani, ilikuwa kazi sana kubadilisha fikra na mitazamo yao.?


Profesa Yunus alisema anakerwa na kitu kinachoitwa wataalam, akiongeza kwamba wengi wanaoletwa katika nchi au kusimamia mradi fulani, kwa namna moja au nyingine, ni watumiaji wa fedha ambazo zingetakiwa zitumike kuwasaidia watu maskini.

"Utasikia tunakuletea consultants (mshauri) wa nini huyu? Hivi mama huyu ambaye miaka nenda rudi amekuwa akitengeneza vyungu vyake leo unamletea mtaalam, eti amfundishe anamfundisha nini asichojua, huyu mama anachohitaji ni kuongezewa mtaji, kwangu mimi masuala haya ya consultant ni matumizi mabaya ya fedha tu.


Mtaalam huyo anatoa ushauri kwamba, linapofikia suala la kuwasaidia watu maskini, halipaswi kuwa wa serikali peke yake, anasema ni mchakato unaotakiwa kumshirikisha kila mtu na hasa wale walionacho.

Anafafanua kuwa wale walionacho lazima wawe tayari kuchangia huduma za kijamii au kufanya biashara ya kijamii ili serikali itumie nguvu zake katika kuwasaidia wale wasionacho.


"Mnaweza kufanya biashara ya kijamii, hapa ninamaanisha nini? Maana yangu ni kwamba wale wenye uwezo walipie zile huduma muhimu kama vile afya, maji, elimu na nyinginezo. Kwa kufanya hivyo, watasaidia kuipunguzia kazi serikali na hivyo kujielekeza kuwasaidia watu maskini.

Anasisitiza kwamba hili la kuchangia ni lazima lifanyike, wafanyabiashara nao lazima waonyeshe mchango wao, kwa mfano, mtu anaweza kujenga hospitali yake na kuwatoza watu kwa huduma wanayoipata.

Lakini, kwa fedha ile ile wanayotoa watu wenye uwezo, akatoa huduma hiyo hiyo kwa watu wasio na chochote, hapa huyu atakuwa anafanya biashara sawa, lakini upande mwingine atakuwa anamsaidia mtu maskini asife kwa sababu tu hana fedha,? anaeleza mchumi huyo.


Anaongeza kuwa hili likifanyika kwa ufanisi, mfano huu unaweza pia kusambazwa katika maeneo mengine ya nchi.


Rais Kikwete akamweleza: "Afadhali hilo la uchangiaji, umelisema wewe, maana sisi hapa tumeanzisha utaratibu wa watu kuchangia elimu ya juu, lakini hizo kelele tunazopigiwa ni ajabu ya Mungu.


Tunachosema ni kwamba wale walionacho wachangie ili wengine wasionacho waweze kugharamiwa na serikali, lakini wapi watu hawataki kabisa kuelewa. Natamani kauli yako hii ungeisema hadharani.?


Rais Kikwete pia akamweleza mgeni wake kwamba madhumuni hasa ya kumwalika kubadilishana mawazo na kuchota hekima, busara na maarifa yake.


Akasema kwamba serikali yake imeanza taratibu za kuwawezesha wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia mikopo ya kuendeshea shughuli zao.

Lakini akasema ingawa serikali yake imeanza hatua hizo, bado anadhani michango kutoka kwa wataalamu mbalimbali kama Profesa Yunus inahitajika ili kuboresha mchakato huo.


Anakubaliana na profesa huyo kwamba mabenki na taasisi nyingine za fedha hazina sababu ya kuogopa kumkopesha mjasiriamali mdogo kwa kuwa wameonyesha uadilifu katika ulipaji wa mikopo hiyo.

Akasema anafarijika kwa kusema angalau hivi sasa kumekuwa na mwamko kidogo kutoka baadhi ya mabenki nchini ambayo yameanza kukiri kwamba watu wa kipato cha chini nao wanalipa mikopo tena kwa wakati.

Profesa Yunus akahitimisha mazungumzo na Rais Kikwete kwa kuahidi kwamba yuko tayari wakati wowote, kufika Tanzania na kushirikiana na serikali ili kuratibu mipango mbalimbali itakayoharakisha mchakato wa kuwaondoa wananchi katika umaskini.

Akasema anashukuru serikali kwa heshima kubwa ya kutambuliwa hasa na Rais Kikwete na serikali kwa ujumla kwamba anaweza kuchangia katika maendeleo ya wananchi wa Tanzania.

*Maura Mwingira ni Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais.

Source : mwananchi
 
eti Tanzania watu maskini ni 2.5 million tu? Sasa Raisi alimwita huyo Mbangladesh wa nini wakati tayari Raisi ana mpango ku kutoa ajira million 10?

Ndiyo maana huyu Prof.Yunus akasema kazi iliyopo ni ndogo.
 
Tatizo maneno mazuri yamezidi kila kukicha!

Watu<viongozi>wako half hearted kwenye mambo kama haya,ndio maana utaona yanaanza na si punde yanafifia!

Halafu tuje kwenye ukweli,hivi wajasiriamali wetu wanahitaji mtaji hasa?sawa,lakini tatizo lao kubwa ni masoko ya bidhaa zao.kama utawapa mtaji halafu wakakosa soko si ndo unawatia kwenye madeni?na hivyo umasikini zaidi.

Tuangalie,ni kiasi gani cha bidhaa toka nje ambazo zingezalishwa nchini,tunaziagiza?

Chipboards na jamii yake.

Gypsum boards.

Imported furniture

Alikuja de soto,amekuja prof.yunus....na wengine watakuja,tena sana tu....lakini kama hatutakuwa na moyo thabiti wa kuona hali za wananchi walio na kipato kidogo zinainuka...basi,itakuwa ni furahisha barza tu!

Nadhani hatumuhitaji yeyote kati ya hao...tunachohitaji ni kuwezeshana tu,si kwa pesa,bali kwa kila mtu kutimiza wajibu wake.

Yaani,daktari ahakikishe wagonjwa wanapata matibabu sahihi,hakimu aamue kesi kutokana na ushahidi uliopo,kiongozi awaelekeze watu wake bila kuchoka na awe mvumilivu kwani kulalama hakutasaidia,wanakijiji washirikiane bila kuchoka kujenga barabara na kupata maji safi,pia wahakikishe walimu wanaopelekwa kwenye vijiji vyao wanaishi maisha mazuri iwezekanavyo kwani hao ndio njia ya watoto wao kuondokana na umasikini.

And above all,tuzipende kazi zetu na kuzifanya kwa moyo kama vile wapo<na huwa hivyo>watu ambao maisha yao yako mikononi mwetu!wakifa lawama ni kwetu!

Mwisho,tuache uvivu wa mawazo na vitendo!
 
Maskini milioni 2.5, looh! hawa jamaa yaani wanadanganya kila kitu.

Maskini Tanzania ni zaidi ya milioni 30, wenye unafuu wa angalau kuwa na uhakika na mlo kwa mwaka mzima TZ hawazidi milioni 10
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom