Kwanini waswahili tuko hivi?

na samtaimu utaliona jibaba lina waifu na watoto tisa linakamatwa limebaka kuku. inakera sana.why yu repu chikeni? why yu repu awa fevoraiti vijitebo? why bana?.
aaaargh! ndo mana nafkiria kuomba uraia poland.
hapa greti thinka nipo veri disapointedi!
 
Waswahili huwa tunatema mate kwenye mabasi,
tunapenga na kukojoa hovyo barabarani,
tukiwa tunahama tunang'oa hadi silingi bodi licha ya kuwa tumelikuta, na pia huwa tunaharibu vitasa vya milango,
tukienda kwenye pati tunaiba misossi na kuondoka na chupa,
jamani hivi kwa nini tuna tabia za ajabu?
Tabia zetu mbaya ni nyingi mno kiasi kwamba nikiandika zote hapa wino utaisha kwenye monitor yangu,
lakini kikubwa cha kujiuliza, kwa nini leo tusiachane na tabia hizo?

Walezi wengi weusi ni walezi wasiojali, wanaswaga watoto utafikiri ng'ombe wa ranch. Pia ktk mila nyingi za weusi kuna taboo nyingi na hatupendi kubadili mazingira yetu, hebu nenda baa yeyote pale Dar City uone watu wanavyoshirikiana na inzi kula nyama choma bila tatizo kabisa. Ukiwauliza, wanacheka tu kama vile hamna tatizo. Hata mawaziri mawaziri wetu ndio maisha hayo. Msimu wa masika nenda sehemu yeyote TZ utakuta ni inzi, inzi, inzi, lakini watu wala hawaoni wala hawajali. Product: Ni taifa la tusiojali wala kuwajibika kwa chochote. Hata kwa wasimamiaji wa sheria zetu, mali zetu, nk ndio hivyo hivyo, nao hawajali.
 
We africans lack the so called 'Social Capital'. Early socialization begin at home then carried forward by other social Instituitons (i.e. educational, political, economical institutions). Aims of socialization is to internalized social values, norms, traditions and good culture to members of a family/society. These Institutions are supposed to teach people social life i.e. how to value and safeguard properties in their surroundings, how to behave before others,what is right or what is wrong.What we're witnessing today is the total failure of social institutions to invest in people (Social capital). that is why tunaona watanzania wanaharibu daraja la mto Rufiji ili wapate vyuma chakavu wakauze (Failure of economical institution), Wengine hawana heshima mbele za watu wanaowazidi umri au wanakunya na kukojoa barabarani (Failure of family institution), wengine kwa kukosa ufahamu wanakata mikono ya albino ili wapate kuwa matajiri 'ignorance' (failure of education institution). Na bado tutegemee kuona mengi
 
Nafikiri waswahili ustaarabu wao wameukalia na ****** ndio maana hawajuni maana ya neno ustaarabu. yaani ni uchafu uchafu tu kila mahali ukiwauliza mbona mnashindwa hata kusafisha maeneo yanayowazunguka utasikia oh city hawajaja kuzibua mifereji, site hawajafagia soko, city hawajazoa matakataka. wakati wenyewe ndio wachafuzi wakubwa , ndio wanasababisha mifereji kuziba, ndio wanasababisha hata miji yetu inanuka vinyesi. hii yote kwa sababu ya ustaarafu wa ******.

imagine mtu anakojoa kwenye sink la kunawia na pengine hao ndio wamevaa suti na tai wakiwa nje lakini akiingia ****** anachamibia ukutani. loh! mimi nafikiri hizi TV na redio kungekuwa na kipindi kinaitwa ustaarabu na kufichua mambo kama hayo na mtu akikamatwa anafanya vitendo visivyo vya kistaarabu picha yake ibandikwe hadharani kuwa huyu ni mmojawapo wa aliyekosa ustaarabu na mchafuzi wa mazingira.
 
Hayati Nyerere aliyaona haya zamani sana na ndio maana alisema kuwa tuna maadui watatu wakubwa, na ili tuendelee inabidi tupambane nao, hawa ni ujinga,maradhi na umaskini. Akajitahidi akaanzisha kisomo cha watu wazima,wajifunze kusoma kuandika,maarifa n.k Lakini watu wote walimwona chizi! Sasa kama wewe si mjinga,kwanini ung'oe kiti ambacho kesho ukirudi uwanja wa Taifa utataka kukikalia? Na usipokikuta unadai serikali haijali,ikujalije? Na bila ya ujinga kuisha,ni vigumu kukomesha kitu chochote,kwani unakuwa huwezi ku-reason. Au mkoloni arudi tu tuchapwe viboko,tupate akili! Banza stone aliwahi kuimba akisema.'bora ukose mali upate akili......!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom