Kwanini wapenzi na mashabiki wengi wa CHADEMA hawamuamini tena Zitto Kabwe?

Mara kadhaa kwenye thread mbalimbali kumekuwa na kundi kubwa la mashabiki na wapenzi wa chadema kuonyesha waziwazi kutokuwa na imani na Zitto Kabwe mtu ambae walimuamini na kumpenda sana kabla hawaja anza kupoteza imani na mapenzi nae.

Sasa hivi usishangae kuona wanachama na wapenzi wa chadema kutokumpa kabisa nafasi ya kumzunguza kwa mema mbunge huyo machachari na matokeo mazungumzo mema yameelekezwa sana kwa John Mnyika, Tundu Lissu, Mdee na wakati mwingine kwa Godbless Lema.
Kautafiti kangu kadogo kamenisukuma kujiuliza na kuamua kuungana nanyi magreat thinker.

Hivi ni kwa nini wapenzi na mashabiki wa chadema hawana tena imani na Zitto Kabwe?
Tafadhari weka sababu huenda zikamsaidia kujirekebisha.

Nawasilisha.

Sijui umefanya wapi utafiti....
 
Ni Mbowe amekutuma? Mbona unahangaika sana kuhamasisha chuki juu ya Zitto? Umeshatoa mada si utulie upate maoni au uchangie unapoona panakugusa? Umeona haitoshi unang'ang'ania wasio na imani ni wengi. Uchambuzi wako unafikiria JF iliyojaa maadui wa Zitto ndio itabadili ukweli wa mazuri yake?
Well, umetaka sababu za watu wengi kupoteza imani juu ya zitto.
1. Sio kweli kwamba watu wengi wamepoteza imani, ila kuna kundi la watu tena ndani ya chama chake kwa kumhofia wanapandikiza mbegu za chuki juu yake na kujitahidi kufanya watu wapunguze imani kwake, ila anayoyafanya yako wazi mbele ya Wote wenye macho na maskio.
2. Zitto yuko huru juu na anachoamini kuwa sahihi, hafanyi siasa za kizee na haoni tabu kumsifia mtu anapofanya jambo jema hata kama si wa chama chake. Mfano rahisi ni ishu ya posho, wameshakubaliana kama chama kwamba posho ya vikao si stahili yao, lakini watu wana tamaa wanaendelea kupokea tu huku wanasema wanapinga, sasa ujinga kama huu ndio Zitto asioweza kuuvumilia, yeye akaamua kutokupokea. Unategemea hapo watampenda?
Nashindwa kuwaelewa nyie mnaomtetea Zito! hivi nyie mnampenda zito au mnataka kumzamisha kabisa? Msijidanganye kuwa kila anaemkosoa Zito ni yule anayemhitaji Mbowe au ni mchaga. Hiyo propaganda ya uchaga haina nguvu kama mnavyoipigia kelele na kimsingi baadhi ya wale tunaomshangaa Zito ni wale tuliokuwa tunamtegemea sana Zito na kosa lake sio kutaka kugombea uenyekiti maana hilo alishauriwa akajitoa. Tatizo la zito ni kuwa amebadilika sana ndugu zangu; tofauti na zamani zito sasa ana mawasiliano makubwa na JK na ambayo ni hatari kwa upinzani, mchezo wake na Kafulila unawaumiza sana wanachadema. Mipango yake ya kugombea urais sio mibaya lakini haraka alizonazo zimemfanya asiaminike tena, CHADEMA haindeshwi kihuni hata mgombea urais anapatikana kwa utafiti wa jinsi anavyokubalika kitaifa ndo maana hata mbowe pamoja na kazi nzuri anayoifanya lakini alishauriwa asigombee urais. Sasa mnaomlinda Zito mbona hamsemi imekuwaje atume polisi kwenye vikao vya NCCR? mbona hamsemi yeye alienda South Sudan na kikwete kama nani? mbona hamjiulizi ni kwanini aliamua kumuunga mkono Kafulila akamwacha mgombea wa CHADEMA? Kinachomwokoa ni busara za uongozi wa CHADEMA angekuwa NCCR nae angetimuliwa.
 
zitto kama binadamu ana mapungufu yake sawa lakini kuna kundi la watu "maalum" waliowekwa kumuharibia! kuna hot issues ambazo zitto amezisimamia hao mnaowaamini wameshindwa.mfano hai ni issue ya posho,amesimamia alichoamini. kuna wengine wanasingiza ohh pesa zinawekwa moja kwa moja kwenye akaunti za wabunge, wanataka kutuaminisha kuwa zitto hana hiyo akaunti?zitto ameibua mijadala mingi pale bungeni na kwingineko ambayo imeleta tija kwa taifa hili.so mpeni heshima yake!
Usiwe mwongo! ishu ya posho ipo kwenye ilani ya CDM kama vipi kasome ilani kwa hiyo zito alikuwa anatekeleza ilani na ndomaana hata mbowe alikataa VX la kiongozi wa upinzani bungeni. Na kuhusu posho kuweka kwenye akaunti za wabunge hata zito mpaka sasa anawekewe maana kimeo makinda alisema watakuwa wanawekewa tu watake wasitake.
 
Mkuu ujue we una point sana, na always una hit to the tagert, ila tu hiyo Avatar yako ndo inanichefua kila nikkiangalia Mkuu, Badilisha Mkuu, haindeni kabisa na points zako,some times nikkiangalia AVATAR Yako, najikuta na scrol down nikihisi utakuwa umeandika Upupu kama hiyo AVATAR yako, kumbe sio Mkuu, itoe Mkuu
Nashaukuru kwa ushauri wako nitaufanyia kazi.
 
Kweli ndiyo maana Turnover ya makampuni yanayochapisha magazeti pendwa ni kubwa sana kulinganisha na magazeti mengine.....! Kwa aina hii ya waso,i , basi tusiwaonee wale ambao hawakuingia madarasani.It's a pity watu wanakuja na udaku juu ya mtu halafu watu wanaunga tela tu.Kuna baadhi ya watu hapa ambao kwa rekodi yao hapa JF wamekuwa analytical lakini walivyochangia wamenichekesha na kunisikitisha....wengine huwa sishangai

Guys let us be serious on issues...tuachane na trivial issues!
 
Sijui umefanya wapi utafiti....

Na mimi nilitaka kujua hako kautafiti kake alifanyia wapi? Hata hivyo ni kama kuna kaukweli unaotokana na kujihusisha kwake kisiasa na akina Rostam kwa kutaka kuivuruga CDM.
 
Zitto ana Ungonjwa wa "Uswaiba"+kujiona yeye ndo Kichwa pekee ndani ya chama so kila anacho kisema basi anataka kifuatwe!!

Kumbukeni huyu jamaa alikataa kufanya wlkout mbele ya JK eti kisa JK alijenga barabara jimboni kwake,so jambo la kujiuliza hapo ni kuwa, hivi PRESIDENT kujenga barabara jimboni kwake ilikua ni favor ambayo ilimlazimu kuilipa kwa style ile kiasi cha kuonyesha utovu wa nidham kiasi kile au ni wajibu wa PRESIdeNT sio tu kwa jimbo lake bali n akwa majimbo mengine!!

Hii inaonyesha kua huyu jamaa USWAIBA unmuathiri sana ktk kufanya maamuzi..ila mi namshauri akae chonjo maake CDM ina shehena ya KUtosha wala ye sio superstar ka anvyofikiri coz yapo majembe ka akina MNYIKA na TUNDULISU etc na ajifunze tu kutoka kwa swaiba wake huyu bw mdogo KAFULIA... ahhh KAFULILA
 
Kweli ndiyo maana Turnover ya makampuni yanayochapisha magazeti pendwa ni kubwa sana kulinganisha na magazeti mengine.....! Kwa aina hii ya waso,i , basi tusiwaonee wale ambao hawakuingia madarasani.It's a pity watu wanakuja na udaku juu ya mtu halafu watu wanaunga tela tu.Kuna baadhi ya watu hapa ambao kwa rekodi yao hapa JF wamekuwa analytical lakini walivyochangia wamenichekesha na kunisikitisha....wengine huwa sishangai

Guys let us be serious on issues...tuachane na trivial issues!
Ben maandishi yako kiasi yanadharau kwa waliokosa opportunity ya kwenda shule kwa sababu ya system mbovu tuliyonayo, kama wewe ulibahatika kupata madarasa shukuru Mungu afterall madarasa ni kitu gani kama hayajakuelimisha.

Kuhusu Zitto ningeshangaa kama ungesema tofauti, Zitto is not the same i used to know in short bila kuficha is an opportunist he is there for himself not for others hata hizo kelele sijui za Buzwangi, Barrick kumbe zilikuwa za nini. Tunamjua Zitto kaanza siasa juzi bado ni kijana sana kwenye nyanja za siasa kusema tu ameingia CDM tangu yuko 16 haitoshi je anaifanyia nini CDM je analipeleka wapi taifa je anawafunza nini vijana kwa vitendo anavyofanya hayo ndiyo ya msingi. Mnaposema watu wanaleta majungu ina maana gani ukweli mnaita majungu, anyway ni jana tu tumeambiwa Zitto kahusishwa na vurugu za NCCR utasema ni majungu je hapo wewe binafsi umejifunza nini kutoka kwake kama role model wako kama si kuwachanganya vijana wanaomwamini ni nini. Nyie watetezi wake msiwe rigid sana kuwa Zitto hawezi kubadilika kwamba alivoingia CDM basi atabaki hivyo hivyo hadi kufa kwake never, watu wakitoa evidence mnasema majungu mnatakiwa kubadilika.
 
Back
Top Bottom