Kwanini wanawake wengi wajawazito wanakuwa na ugomvi au kauli mbaya?

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Habari za sahizi wapendwa, poleni na weekend na pia nawatakia weekend njema.
Nilikuwa na swali kuhusu wanawake/wamama wajawazito;

Ni kama inatokea mara kwa mara wanawake wajawazito wanakuwa na hasira au ugomvi, au unakuta wanagombeza tu hata bila sababu, tangu nikiwa shule ya msingi, sekondari hata sasa hapa chuoni lecture wangu ana hiyo hali.

Unakuta waalimu wajawazito hata darasani wanachapa bila sababu, sio bongo tu hata hapa nilipo nakereka sana pale anapotutusi na mwanzoni hakuwa hivo, hata manyumbani sometimes unakuta hizo hali zipo kwa mama zetu ingawa sio wanawake wote.

Ni kitu gani hasa linasababisha wawe na kauli mbaya/ugomvi/fujo?
Na je kwa kipindi hicho cha ujauzito nini hasa cha kufanya ili uwezo kuchukuliana nao?
 
wanakuwa na hasira za tabu ya ujauzito
na sometimes wanakuwa na unknowns fear kuhusu baba wa mtoto na mambo mengine
na wengine wanakuwa na regrets na aliempa mimba.....

kama ni hormones tu mbona sio wote?
 
Wanakuwa wamechoka na kwa hiyo hawataki usumbufu. Vile vile kuna wanaochukia mabadiliko ya miili yao na hiyo inawafanya wawe na hasira. Kwa ufupi ni stressfull moment
 
na kweli wengine wanapatia tu sababu ya kujiachia vitabia vyao vibaya! ni attitude pia inachangia japo kwa wale watu wa dini kuna spiritual issues. ukiwa positive,u become @ ur best!

nhh na wengine wanakuwa wamepatia sababu
 
Kuna wengine wakiwa na mimba wanapata lots of complications. Unakuta kuna mtu anatapika from day one mpaka ajifungue; mwingine yeye na kopo la kutema mate tu; bado unategemea mtu kama huyo awe ana smile muda wote? Kila mimba in experience yake ndio maana wengine wanakuwa OK wakati wengine wanakuwa visirani.
 
Huu msemo wa mimba si ugonjwa wanaupenda sana watu wasiopenda ku care wenza wao pale wanapo conceive. I wish mimba ingekuwa inabebwa kwa kupokezana ili watu waongee kwa experience si kwa kufikiri tu.
<br />
<br />
NK ugonjwa uko wapi hapo mpendwa?
 
na kweli wengine wanapatia tu sababu ya kujiachia vitabia vyao vibaya! ni attitude pia inachangia japo kwa wale watu wa dini kuna spiritual issues. ukiwa positive,u become @ ur best!

Labda....
Inawezekana kwa baadhi na kwa wengine, haiwezekani.


Kama unakumbuka, msichana au mvulana wakipevuka huwa pia kuna mabadiliko ya tabia na maumbile. Hii inatokana na kuingizwa kwenye mwili, HORMONES ambazo mwanzoni hazikuwepo.

Kwa kijana wa kiume, akishabadilika hapo baada ya kupevuka, hormones zake hazipungui kwa ghafla, zitapungua kidogo kidogo mpaka uzeeni, na hii inafanya tabia za mwanaume kutobadilika badilika tena.

Kwa mwanamke, mara baada ya kupevuka, hormones zile zinakuwa zinabadilika kwenye mzunguko wake mwezi. Na usishangae mwanamke kubadilika mood (hata kama hana mimba) katika huo mzunguko wa mwezi mmoja.

Mara mimba ikiingia, hormones zingine kabisa zinaanza kuzalishwa na kubadilika viwango na aina, hadi anakuja kujifungua. Kwa hiyo katika kipindi cha mimba, usishange mwanamke kubadilika mood au tabia kadhaa, vitu anavyopenda kula, n.k vyote vyaweza kubadilika. Akisha jifungua, hormones zinarudi kama zamani, na tabia yake ya kila mwezi inajirudi.

Mambo yataendelea hivyo mpaka akifikia menopause. Ambapo hormones nyingi za kike zinakoma kuzalishwa. Hapo tena tarajia mabadiliko makubwa kutokana na hormonal imbalance, mpaka pale mwili utakapozoea baada ya mwaka, au hata miaka.

Hata hivyo, effects kwenye kila stage zinatofautiana kati ya mwanamke na mwanamke. Si lazima wafanane kila kitu. Lakini ni busara, ukategemea mabadiliko na kukubali kuwa mwanamke hasa kipindi cha ujazito na menopause, anatakiwa KUHURUMIWA na si kudhihakiwa...
 
Huu msemo wa mimba si ugonjwa wanaupenda sana watu wasiopenda ku care wenza wao pale wanapo conceive. I wish mimba ingekuwa inabebwa kwa kupokezana ili watu waongee kwa experience si kwa kufikiri tu.

nyumba kubwa kweli mi nisingeweza kuibeba
 
Nikiwa nina mimba mume wangu anatapika wakati mimi niko fresh. Tukienda kwa madokta wanasema anakuwa affected kisaikolojia wala haina uhusiano na mimba yangu. Wazee wao wanasema sijuhi mkeo akikuruka toka kitandani basi unabeba karaa zake za mimba. I have two kids with similar experience. It is so fun. Imeshawahi kuwatokea any of you? Mme wangu hataki kusikia tena maswala ya another kid maanake cha moto anakiona.
 
Hayo yaliyosemwa na wadau waliotoa maoni yao ni ya kweli lakini mie siamini kama mwanamke anaweza kusubiri apate mimba ili agombane na mumewe
 
Niambie kwanza unasomea wapi ndo ntakujibu.:bathbaby::bathbaby::bathbaby:
Nipo Russia,mwalimu wangu wa russian language kwenye lecture anatuzingua sana kisa ana mimba,yaani unaenda class huna amani.
 
Back
Top Bottom