Kwanini wanawake wengi siku hizi wanapenda kuingiliwa kinyume na maumbile?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
kwanini wanawake wengi siku hizi wanapenda kuingiliwa kinyume na maumbile?

Naomba mawazo yenu wana JF

------------------------------

Asilimia 26.5 wanawake hufanya mapenzi kinyume na maumbile:


mchoro.jpg

KWA UFUPI

Wakati idadi ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake Tanzania wamebainika kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile. Wakati idadi ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake Tanzania wamebainika kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mfumo wa uzazi unaharibika

Watafiti wanabainisha kuwa kitendo hicho licha ya ukweli hakifai kwa vile kinaharibu mfumo wa uzazi, kina athari kubwa mno kwa mwanadamu, mojawapo ni ikiwemo uwezekano mkubwa wa wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna vilainishi, hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya kuambukiza vijidudu hivyo.

Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR) alitoa ripoti hiyo hivi karibuni hapa jijini Dar Es Salaam. Mremi akiwa na jopo la watafiti kutoka NIMR anasema kuwa wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi na Kuogopa kupata Mimba.

Vilevile alizitaja sababu nyingine za wanawake kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.

Sampuli za utafiti

Utafiti huo ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Tanga, Makete na Siha. Mremi anasema "Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani. Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo.

Imani potofu kwa wanaume

Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maaambukizi ya VVU, kitu ambacho ni uongo, kwani huko ndiko kwenye kuchangia ukimwi kwa haraka zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote. Katika utafiti huo, wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile, licha ya kwamba ni jambo linalokatazwa na dini zote.

Tanga yaongoza

"Tanga ndiyo kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo" anasema Mremi

Fikra za kulinda ubikira

Ilibainika kuwa wasichana wengine walikiri kufanya hivyo kwa ajili ya kulinda ubikira wao na baadhi ni mila na tamaduni za baadhi ya makabila.

Dk Mremi amekaririwa akisema " Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa baa, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani. Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo". Wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo hilo.

Dk Eliza Shayo, ambaye pia alishiriki katika utafiti huo anasema sababu ya kufanya utafiti huo ilikuwa ni kuangalia visababishi vya kusambaa kwa Ukimwi.

"Lakini pia tuliweza kujua tatizo la kufanya mapenzi kwa njia hiyo lina ukubwa kiasi gani" anasema. Dk Shayo pia anasema utafiti huo uliangalia iwapo wanaofanya vitendo hivyo hutumia kondom au la. Wengi walionekana kutotumia kondom wakifikiri hawawezi kupata virusi vya Ukimwi, imani ambayo sio sahihi.

Ni changamoto

Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Kusini mwa Afrika, (GEMSAT) Dominica Haule anasema utafiti huu ni changamoto kwa serikali, watunga sera na vyombo vya sheria. "Ni wakati muafaka wa kujadiliana nini kifanyike kupunguza tatizo hili. Hii ni hatari na haikubaliki," anasema Haule. Anasema wadau wa afya hawana budi kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu na kuweka wazi madhara ya vitendo hivyo.

Mhadhiri wa Masuala ya Saikolojia, Dk Kitila Mkumbo anasema suala hilo linaweza kuwa na athari kiafya.

"Kisaikolojia, kama wao wawili wamekubalina sawa, lakini kiafya lina athari kubwa," anasema

Dk Mkumbo anasema ufanyaji wa mapenzi upo wa aina nyingi wengine hufanyia mdomoni, inategemea na makubaliano, lakini kiafya inaweza kuwa na athari. Dk Meshack Shimwela, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Ndani ya Mwili kutoka hospitali ya Amana anasema mwanamke ambaye hufanya mapenzi kinyume na maumbile huathirika na kuacha kufurahia tendo hilo kwa njia ya kawaida.

"Lakini pia, wengi hujihisi kama wamelaaniwa na wanakosa kujiamini" anasema na kuongeza kuwa hata kama anaweza kufanya kwa mkumbo, baadae hujutia hasa anapojikuta anapata athari kubwa za kiafya kuliko furaha. Dk Shimwela anasema kitendo hicho husababisha bakteria wasiohitajika kuingia katika sehemu ya haja kubwa na kuleta uambukizo.

"Eneo la haja kubwa limeumbwa kutoa na si kuingiza. Hivyo kitendo hicho husababisha uharibifu na kulegea kwa misuli" anasema

Anasema maradhi mengine ambayo hujitokeza katika sehemu ya haja kubwa pindi mtu anapofanya mapenzi kwa njia hiyo hayana tiba. Anaongeza kuwa wanawake hupata madhara wakati wa kujifungua na hatari ya kupata maambukizi ya VVU ni kubwa zaidi.

Hatari kuu Jarida la Havard la afya ya Wanawake (Havard Women Health Watch) linaeleza kuwa ufanyaji wa mapenzi kwa njia ya haja kubwa ni chanzo kikuu cha maradhi ya kuambukiza ukiwemo Ukimwi.Hii ina maana kuwa watu ambao wanafanya vitendo hivyo wana athari kubwa za kupata virusi vya Ukimwi.

Kwanini ni hatari?

Tishu zilizo katika njia ya haja kubwa ni laini na hazina maji maji, hivyo huchanika kwa urahisi wakati wa tendo na kuingiza vijidudu.
Utafiti kama huu ulifanywa nchini Marekani mwaka 2005 na kituo cha Kudhibiti Maradhi ya Kuambukiza (CDCP). Katika utafiti huo asilimia 40 ya wanaume na 35 ya wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 25 na 44 walikiri kufanya tendo hilo kinyume na maumbile.

Wanatumia matambala kuziba kinyesi

Kuna athari kubwa za kufanya kitendo hicho, baadhi ya watu hujikuta wakivaa matambaza ili kuzuia kinyesi kisitoke kwa vile mfumo wa haja kubwa huwa umelegezwa.

Profesa wa Chuo Kikuu cha tiba cha Colombia, Judy Kuriansky anasema "Inashangaza kuona watu wanafanya mapenzi kwa njia hiyo wakidhani wanajikinga na Ukimwi, huko ni kujidanganya, ukweli ni kuwa njia hiyo ndio inayoweza kumfanya mtu kupata virusi kwa urahisi zaidi". chanzo.


Asilimia 26.5 wanawake hufanya mapenzi kinyume na maumbile - mwanzo - mwananchi.co.tz
Sio kwamba nawatetea......
but huwezi sema kwa mfano kwa nini watu wengi wanapenda kuvuta sigara,bila kujua jinsi sigara ilivyo addictive na jinsi ambavyo ni vigumu kuacha.

Sio wanawake wote wanaoingiliwa kinyume na maumbile wanapenda au kujua madhara yake.....
wengine wanaanza utotoni......

Wengine wanafuata mkumbo,wengine wanafundishwa na jamii mfano nyimbo za taarabu, wengine wanalazimishwa na wanaume waliowapenda n.k

Jiulize kama wanaume wengi tungekuwa hatupendi kuwaingilia kinyume na maumbile,nani angewaingilia?

Tusiendeleze utamaduni wa blaming the victims.....

Zamani ilikuwa ni wanawake mashangingi na malaya tu ndo wanaopenda mchezo huo.

But siku hizi ni karibu wanawake aina zote,wanafunzi,waimba kwaya,wake za watu, wasomi, matajiri n.k

Sababu ni nyingi lakini zaidi ni kuwakuna wanaume wengi siku hizi ambao hupenda kuwaingilia wanwake kinyume na maumbile hata kwa nguvu.

Kuchanganyikiwa na mtandao.

Mtandao umekuja wakati waafrika wengi hatujajiandaa, hivyo tunaona kila kitu kinachoonyeshwa ni sahihi kuigwa,n ni cha kistaarabu!

Mi nishawahi kuwakuta akina dada ofisni wanaangalia pornography za hiyo sijui nini(msiseme tigo bana...mi ndo mtandao wangu) ya kunanihii nyuma, basi unaambiwa macho yamewawiva, wamelegea, wanaweweseka, wamechanganyikiwa kiasi ukimgusa na kidole tu, anaanguka chini!

So what does one expect from such a generation?..mtu kama huyo akitokewa na -------- fulani akaombwa huo mchezo si anakubali kuinamishwa hata kwa kudanganywa kidogo tu kuwa ana shingo ya upanga?!!...maana mi sielewi shingo ya upanga inakuwaje, japo najua upanga una makali!

Its this foreign culture that we just swallow without digestion, the result is puking out!

Kwa sababu hawajiamini kuwa/kama anaweza/ameweza kumtosheleza mwanaume wake.

Mfano, Mwanamke akiwa mwingi yaani kutembea na wanaume wengi, tamu yake inalegea. Au akifanya tendo kila siku na wanaume tofauti nani hii yake inalegea.

Nani hii ya mwanamke ni elastic, lakini ikitanuka inahitaji muda isinyae irudi hali yake. Sasa mwanamke akifanya mapenzi kila siku hasa na wanaume tofauti nani hii inalegea. So mwanaume haridhiki na anamwacha, so mwanamke anaweza akamtegea au akamshawishi mwanaume wafanya kinyume na maumbile ili mwanaume aridhike.
 
Sio kwamba nawatetea......
but huwezi sema kwa mfano kwa nini watu wengi wanapenda kuvuta sigara,bila kujua jinsi sigara ilivyo addictive na jinsi ambavyo ni vigumu kuacha.

Sio wanawake wote wanaoingiliwa kinyume na maumbile wanapenda au kujua madhara yake.....
wengine wanaanza utotoni.

Wengine wanafuata mkumbo,wengine wanafundishwa na jamii mfano nyimbo za taarabu, wengine wanalazimishwa na wanaume waliowapenda n.k

Jiulize kama wanaume wengi tungekuwa hatupendi kuwaingilia kinyume na maumbile,nani angewaingilia?

Tusiendeleze utamaduni wa blaming the victims.

Zamani ilikuwa ni wanawake mashangingi na malaya tu ndo wanaopenda mchezo huo.

But siku hizi ni karibu wanawake aina zote,wanafunzi,waimba kwaya,wake za watu, wasomi, matajiri n.k

Sababu ni nyingi lakini zaidi ni kuwakuna wanaume wengi siku hizi ambao hupenda kuwaingilia wanwake kinyume na maumbile hata kwa nguvu.
 
Mitindo ya maisha imebadilika.

Kumbuka asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. maana yate wote waili (mama na ulimwengu) ni walimu. teknolojia inasaidia huyu mwalimu wa pili (ulimwengu) kufundisha watu wengi sana kwa wakati mmoja.

Ukiachilia mbali hayo ya kinyume na maumbile (nadhani unamaanisha anal sex hapa) kuna pia mitindo mbalimbali yamikonyezo, mabusu, michuo na mibinyo ya kimapenzi.

Yote hiyo si ile tuliyofunzwa na mama zetu. ni huyuhuyu mwalimu ulimwengu
 
Chanzo ni mwanaume, akibadilika huyu kiumbe hakutakuwa na huu upuuzi.

Nimeshuhudia mara kadhaa jamaa anambembeleza demu kwa ahadi kede kede ya vitu vya thamani, kwa miezi kadhaa mpaka maskini yule dada akaingia mkenge halafu yule jamaa akaja kutamba kijiweni eti amekata utepe leo. Na naskia siku hizi magari mengi wanayoendesha akina dada ni zawadi baada ya kutoa tigo.

Inasikitisha rafiki yangu wa karibu aliwahi kuwa na uhusiano na mwanafunzi mmoja wa frm six ambaye kwa status ya wazazi wake usingetegemea awe anafanya mambo km hayo, lkn jamaa kila mechi jamaa alipata lawama kuwa hamfikishi, siku akamtolea uvivu akamkalisha akamuuliza nifanye nini nikufikishe.

Alichojibiwa hakuamini, chanzo ni mme wa mtu aliyekua naye yule mwanafunzi miaka miwili kabla aliyemlaghai kwa kumfungulia account nmb na kumwekea laki tano kwa ajili ya kumlaghai mtoto atoe jicho, so yakawa mazoea
 
Kuna mdada amenunuliwa Nadia kwa sababu ya kutoa tigo, kwa mwendo huo ako kamchezo hakataisha!

Ila si tabia njema hasa kwa wanaotarajia kupata watoto kwa mwanamke ni kijambo kwa kwenda mbele wakati wa kuzaa wakati kwa mwaname ni aibu bse uume ulioutumia kwenye tigo ndo wataka zalisha mtoto kwa kutumia uume huo huo na huyo mtoto akiwa bazazi utalaumu si ni mtoto wa tigo.

LAAAAAAAAAAANA
 
Kwa sababu hawajiamini kuwa/kama anaweza/ameweza kumtosheleza mwanaume wake.

Mfano, Mwanamke akiwa mwingi yaani kutembea na wanaume wengi, tamu yake inalegea. Au akifanya tendo kila siku na wanaume tofauti nani hii yake inalegea.

Nani hii ya mwanamke ni elastic, lakini ikitanuka inahitaji muda isinyae irudi hali yake. Sasa mwanamke akifanya mapenzi kila siku hasa na wanaume tofauti nani hii inalegea. So mwanaume haridhiki na anamwacha, so mwanamke anaweza akamtegea au akamshawishi mwanaume wafanya kinyume na maumbile ili mwanaume aridhike.
 
Nadhani swali lingekuwa kwanini wanaume wengi siku hizi wanapenda kuwaingilia wanawake au wanaume wenzao kinyume cha maumbile. Sote tunafahamu kuwa kwa kiasi kikubwa mapenzi yanaongozwa/yanatawaliwa na wanaume hasa katika jamii za kiafrika ambako mfumo dume bado una nguvu sana.
 
...No Mzizimkavu badilisha huo usemi wako, sio wasichana wengi bana ni wachache tu ,wanaopenda kuiga kila kitu kutoka western countries.

Mwanamke kuingiliwa nyuma ni laana, tena wewe msichana ukiona mpenzi wako anataka nyuma hakupendi huyo. Mwanaume anayempenda mke/mpenzi wake hata siku moja hawezi kuomba nyuma.

Wewe msichana ndio kiini cha mabadiliko, mwanaume akitaka nyuma kataa kata kata. Hata akitaka kukuacha ni bora muachane kuliko kutoa nyuma. Tujifunze kuonyesha misimamo yetu kama wanawake.
 
No Mzizimkavu badilisha huo usemi wako, sio wasichana wengi bana ni wachache tu ,wanaopenda kuiga kila kitu kutoka western countries...

naungana na wote wanaopinga ufirauni huu.

lakini hapa nimeona kitu kinataka kukataa ukweli, hivi umpate mtu anakujali mpaka basi, akakukuta used lakini bado akakuhifadhi, unadhani ni rahisi kusema "bora tuachane"? unadhani wote wana kazi kama wewe, fikiria wale ambao hata komputer anaiona kwenye picha tu. wengine wametolewa katika umasikini mkali sana.

nimefurahishwa na mchango wa posti iliyokutangulia kuwa kampeni ya kupinga tigo ni vyema ikaenda sambamba kwa wanawake na wanume kwani mwanumeni muhimu kwani ingawa anakuja kwa kubembeleza, akiruhusiwa ndiye anageuka mtawala wa tendo na mahiusiano mazima
 
Kuchanganyikiwa na mtandao.

Mtandao umekuja wakati waafrika wengi hatujajiandaa, hivyo tunaona kila kitu kinachoonyeshwa ni sahihi kuigwa,n ni cha kistaarabu!

Mi nishawahi kuwakuta akina dada ofisni wanaangalia pornography za hiyo sijui nini(msiseme tigo bana...mi ndo mtandao wangu) ya kunanihii nyuma, basi unaambiwa macho yamewawiva, wamelegea, wanaweweseka, wamechanganyikiwa kiasi ukimgusa na kidole tu, anaanguka chini!

So what does one expect from such a generation?..mtu kama huyo akitokewa na -------- fulani akaombwa huo mchezo si anakubali kuinamishwa hata kwa kudanganywa kidogo tu kuwa ana shingo ya upanga?!!...maana mi sielewi shingo ya upanga inakuwaje, japo najua upanga una makali!

Its this foreign culture that we just swallow without digestion, the result is puking out!
 
kwanini wasichana wengi sikuhizi wanapenda kuingiliwa kinyume namaumbile? Naomba mawazo yenu wana JF

Mkuu;

Nadhani title yako imekuwa misleading;
ukiangalia historia yetu na hata kwenye maandiko, matendo ya kwenda kinyume yalikuwepo tangu enzi na enzi na hata hukumu zake tulizisoma

ukija kwenye wanawake kupenda, la hasha!!! they are really victims of sexual abuse na ningependa kutofautisha wao na wanaume *******! Mwanamke kuingiliwa kinyume ni kwamba alianzishwa bila ridhaa na baadae ndio akazoea

Nachelea kukubaliana na wewe kuhusu wengi kupenda, ila nadhani ni sisi wanaume tunachangia na hayo yote ni kuigaiga!! vilevile siajabu kwamba hawako wengi ila ni wachche lakini habari zao zinaenea kwa kasi na huwa kivutio kwa mabazazi

Kwa maoni yangu naweza kusema kwamba kama mambo ya tIGO yameongezeka, basi ujue ni mwendelezo wa abuse, utandawazi na pia kuiga hasa kwa sisi wanaume kung'ang'ania kudai na hivyo wengine wana-fall victims

Mimi pia nina swali, je wanaume wanaopenda kuingiliwa kinyume nao wameongezeka?? Hauoni labda ni ukuaji wa access to information ndio umemagnify tatizo?
 
Back
Top Bottom