Kwanini wanaume wengi waliooa hawapendi kuvaa pete ya ndoa?

Mimi ni mbeba zege nikivaa pete naweza nikajisahau kuivua kabla ya kuanza kazi,matokeo yake nitaichubua wakati wa kupokezana makarai matokeo yake haitapendeza tena.Kwa hiyo ni bora niivae jumapili kwenye ibada tu.
 
Uaminifu katika ndoa hauletwi kwa kuvaa pete. Kimsingi uaminifu katika ndoa ni suala la kimaadili, Kiroho na mahusiano binafsi ya mwanandoa na Mungu (Ethical, Moral and Spritual values).

Pamoja na hayo, sheria ya ndoa ya Tanzania hailazimishi mwanandoa kuvaa pete au kutokuvaa. Vile vile baadhi ya madhehebu hawavalishwi pete wakati wa kufunga ndoa.
 
Tatizo ni kutokana na wengi kula vinono na kunenepa vidole so pete inakuwa haitoshi ila wote wanatembea nazo mfikoni
 
Nimechunguza, nimetafiti na nimegundua na kuvumbua kuwa wanaume wengi hawapendi kuvaa pete zao za ndoa kwa visingizio mbalimbali, na kuna kundi lingine ndio huwa linatoka nyumbani wakiwa na pete zao za ndoa na wakifika mitaani huzivua na kuzitupia mifukoni.
Cha ajabu ni kwamba, dada zetu wao wanapenda sana kuvaa pete za ndoa, hata ambao hawajaingia kwenye hiyo taasisi takatifu hujivisha wenyewe pete zao za ndoa na kudundika mitaani.
Nauliza tena wenzangu, kwa nini wanaume wengi walio oa hawapendi kuvaa pete zao za ndoa?

Sio pete tu hata mkanda sivaagi kama suruali inanitosha
 
wapo wanaume wanaoogopa kupeperusha ndege kwa kuvaa pete lakini wapo ambao huwa wanasahau tu, si unajua wakati mwingine unavua! kwa wanaume pete siyo big deal ndo maana wanasahau kuvaa ila kwa kina mama ni heshima kubwa sana zikionekana zile gold zinangaa pale mkononi tena zote mbili ya ingegement na ndoa.
 
wanaume wengi wasiovaa pete umalaya umewazidi,wanapenda wasichana wadogo ambao wanataka wawadanganye kwamba wako single,wanawake tukishaolewa tunapenda kila mtu ajue na ni njia ya kuzuia kutongozwa na kuheshimu ndoa zetu.Hebu msio vaa mvae kwani mlilazimishwa kuoa?
 
Back
Top Bottom