Kwanini wanaume ni waoga kiasi hiki

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,072
18,258
WANAUME WENGI NI WAOGA MBELE YA WANAWAKE WALIOSOMA AU WENYE PESA.

UTAKUTA SABABU NYINGI ZINALETWA ETI HOO WALIOSOMA NA WENYE PESA HAWAPENDEKI ETC LAKINI UKIFATILIA CHANZO NI WOGA.

NAFIKIRI BABU WA LOLIONDO ATOE DAWA YA KUTIBU HAKA KAUGONJWA

WEEKEND NJEMA
icon13.png
 
Hawajiamini.
Hawajitambui
Hawataki kukosolewa.

Baadhi wanapenda kunyanyasa, akiwa na mwanamke aliyesoma mwenye kipato anahisi atakua chini, maana hawezi mnyanyasa,au kumtishia arudi kwao.

All in all chanzo ni kutojiamini.
 
Hakuna mwanaume anayemuogopa mwanamke eti kisa kasoma, ana madaraka, fedha au nini!! wanaume wanachoogopa ni ULIMBUKENI unaowakumba wanawake wengi hasa wanapopata vitu hivyo; so they want to play safe. Wanawake wote wenye madaraka, shule, n.k. wana wanaume wanaowapanda kama kawaida. Tatizo kama mwanamke akiwa limbukeni au akiona kuwa madaraka yake, cheo chake, n.k. ndo dili sana akaanza kuonesha dharau, basi Mwanaume husepa mara moja.

Sasa mwanamke akishaona amekimbiwa ataanza kulalama eti kakimbiwa sababu ana shule, fedha au madaraka!! No amekimbiwa sababu ya ulimbukeni wake na si sababu ya vitu hivyo. Hata wanaume wanaozinguliwa na vitu hivyo kiasi cha kuwafanya wawe na dharau sana nao hukimbiwa vile vile na wake au wadada! Huu ni upanga ukatao kuwili.

Kwa hiyo ukiona umesoma, unafedha, cheo au madaraka makubwa, halafu ukaona wanaume wanakukacha, ujue una vijitabia vya kulingia cheo chako, mshiko wako au madaraka yako. Na hiyo tabia ni mbaya tu. Hata ukilingia sana uzuri wako bado wanaume watakukimbia tu!!
 
Naona mtoa mda yamemkuta.....njoo nikuoe mke wa pili (joking)
 
Money is equivalent to power... Waweza kataa ndo ukweli wenyewe huo... iwe katika mahusiano ama maisha ya kawaida with Money waweza geuzwa hata Mungu... Mfano rahisi tu; jiulize ni kwanini kua kuna Maraisi nyuma ya Raisi wetu?? MONEY!

Hivo basi kweli kabisa inapendeza katika mahusiano kama Mwanaume yupo juu kipesa kuliko Mwanamke ili kuepusha vimatatizo vya hapa na pale... Inapotekea mwanamke anapesa kuliko mwanaume - yahitaji mwanamke mwenye busara saana for hata akupende vipi in the long run aweza geuka na kujenga kakiburi fulani ambayo yaweza mfanya mwanaume ajisikie emasculated..... Na if he is in that sorry state, then it means kisha kua weak... Na IMO a man should be stronger than a woman in a relationship. Sisemi amtawale but wanaoelewa you know what i mean....
 
Sababu nyengine ni kuwa mwanamke alosoma na kuwa na pesa mara nyingi hukataa /kutawaliwa na mwanamme...
 
uwoga wao wenyew lakin weng wa wanawake wenye pesa wala cheo si wanyanyasaj ukimtimizia swala la 6x6 hatok nje hata kam ww ni kapuku utakula pesa yake tofaut na wanaume wakiwa nazo wanyanyasaj anafikiria akatongoze dem gan tena yaan hata umpe vp yy anawaza ngono tuuu ili et wamkome kumbe anajimaliza!
 
Sababu nyengine ni kuwa mwanamke alosoma na kuwa na pesa mara nyingi hukataa /kutawaliwa na mwanamme...

Unadhani kwa nini wanakataa 'kutawaliwa' na mwanaume? Btw, hivi 'kutawala' katika muktadha wa ndoa/mahusiano kupoje (kunaambatana na vitendo gani/ishara gani)?
 
Hawajiamini.
Hawajitambui
Hawataki kukosolewa.

Baadhi wanapenda kunyanyasa, akiwa na mwanamke aliyesoma mwenye kipato anahisi atakua chini, maana hawezi mnyanyasa,au kumtishia arudi kwao.

All in all chanzo ni kutojiamini.

Mitazamo hasi kama hii hapa dhidi ya wanaume ndo kinachofanya mwanamke ashindwe kuwa na mahusiano na mwanamme. Hii ni kwa sababu kila mme atakalofanya wewe unaona unanyanyaswa, kumbe wanaume ndivyo walivyo, hakufanyii hivyo eti kwa sababu anakunyanyasa.

Kumbuka tu kuwa mwanaume na mwanamke ni watu tofauti katika baadhi ya mambo na hivyo wana mitazamo inayotofautiana. Wanawake wanaotambua hilo, hata awe amesoma vipi, hata awe millionea bado ataishi na mwanaume wa aina yoyote na watadumu.

Lakini mwanamke anayewachukua wanaume wote na kuwaweka kwenye gunia moja la unyanyasaji, ataishi kweli na mwanaume kinyonge tu kwa kuwa hana kitu!! Akipata kitu tu, basi ndo inakuwa shida.

Rekebisha mtazamo wako tu, mtazamo ndo huumba mazingira yako na kukufanya uwe hivyo ulivyo!
 
Unadhani kwa nini wanakataa 'kutawaliwa' na mwanaume? Btw, hivi 'kutawala' katika muktadha wa ndoa/mahusiano kupoje (kunaambatana na vitendo gani/ishara gani)?

Kutawaliwa nikuonako Mimi labda
1. Kutokubali kuwa mwanamke naye ana mawazo ambayo yanafaa kusikilizwa kwenye masuala ya familia

2. Kuelewa na kumruhusu mwanamke kufanya maamuzi linapokuja suala la pesa alizonazo
(akiamua kumnunulia mdogo wake gari, nyumba,..)

3. Kumpa uhuru Wa kutosha wa kufanya ayapendayo japo kama Mume yeye hayo hayapendi

Na kadhalika :]
 
Hakuna mwanaume anayemuogopa mwanamke eti kisa kasoma, ana madaraka, fedha au nini!! wanaume wanachoogopa ni ULIMBUKENI unaowakumba wanawake wengi hasa wanapopata vitu hivyo; so they want to play safe. Wanawake wote wenye madaraka, shule, n.k. wana wanaume wanaowapanda kama kawaida. Tatizo kama mwanamke akiwa limbukeni au akiona kuwa madaraka yake, cheo chake, n.k. ndo dili sana akaanza kuonesha dharau, basi Mwanaume husepa mara moja.

Sasa mwanamke akishaona amekimbiwa ataanza kulalama eti kakimbiwa sababu ana shule, fedha au madaraka!! No amekimbiwa sababu ya ulimbukeni wake na si sababu ya vitu hivyo. Hata wanaume wanaozinguliwa na vitu hivyo kiasi cha kuwafanya wawe na dharau sana nao hukimbiwa vile vile na wake au wadada! Huu ni upanga ukatao kuwili.

Kwa hiyo ukiona umesoma, unafedha, cheo au madaraka makubwa, halafu ukaona wanaume wanakukacha, ujue una vijitabia vya kulingia cheo chako, mshiko wako au madaraka yako. Na hiyo tabia ni mbaya tu. Hata ukilingia sana uzuri wako bado wanaume watakukimbia tu!!

kweli wewe kipima pembe lol eti wakisoma malimbikeni tena tutake radhi
ni kukosa kujiamini kwenu tu
hamna lolote ..inferiority complex zenu zinawasumbua
 
hela na skonga uleta kiburi sumtimes ....sasa kwa kuogopa matatizo ndio maana wanaume wanawakwepa wanawake wasoi na wenye pesa
 
kweli wewe kipima pembe lol eti wakisoma malimbikeni tena tutake radhi
ni kukosa kujiamini kwenu tu
hamna lolote ..inferiority complex zenu zinawasumbua

Sikatai, wapo wanaume wasiojiamini, wapo wanaume wanyanyasaji na wapo wanaume ambao kuishi kwao na mwanamke wanataka wawe juu siku zote. Hali kadhalika wapo wanawake ambao wakishaenda shule kumzidi mme wake basi tena, tena kwa wanawake ni walio wengi.

Ninachosema ni kuwa si wanaume wote wako hivyo! Hali kadhalika si wanawake wote wako hivyo! Wako wanaume tena wengi tu waelewa wanaoishi na wanawake wenye shule iliyoshiba na/au madaraka na hawana matatizo.

Tatizo ni msimamo wa mwanamke husika. Ikiwa hujakutana na mwanaume wa hivyo usijiwekea kizingiti kwa kusema wanaume wote wanaogopa wanawake walio-soma. Ukishajiwekea hivyo kichwani mwako tayari wewe ndo tatizo.

Kuhusu inferiority complex, sidhani kama umepatia. Wanawake ndo wenye inferiority complex ndo maana akipanda juu anakuwa tatizo. Ungeniambia wanaume wana superiority complex hapo pengine ningekubali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom