Kwanini wanafunzi wengi wanafeli?unajua kunanini nyuma ya pazia

K-killer

Senior Member
Nov 14, 2011
147
28
Habari zenu wakuu,imekua ni jambo la ajabu sana kua unaweza kuona baadhi ya wanafunzi huwa wanafaulu karibu mihula yote wanayokuaga darasani na vidato mbali mbali lakini inakuaga vigumu sana wanafunzi hawa kufaulu form4 au form6 hata kama wanaakili au hufaulu kwa wastani basi wakifika form4 au form6 unakuta wanapata division4 au zero kabisa,wakati mitiani mingine yakuwapima unakuta wanaweza pata division1 au division2.

Swali linakuja, Je inawezekana kweli mwanafunzi awe anafaulu hiyo mihula minginge lakini akifika finals za form4 au form6 anafeli kabisa kama hana akili? au kuna hujumu flani inafanyika na watendaji wa serikali dhidi ya wanafunzi? je kwanini kama ni kweli hawa watendaji wa serikali wanaodili na mitihani ya hawa wanafunzi huwa wanawafanyia hujuma wanafunzi na kuwafelisha mitihani hii ya form4 au form6?inawezekana kuwa ni kwasababu serikali inajaribu kupunguza idadi ya wanafunzi wanaofaulu ili kukwepa kuongezeka kwa garama wanazotumia kuwapa wanafunzi walofaulu kama hawa wanafunzi wa vyuo ambao kutwa hata wao zile ela wanazopewa haziwatoshelezi na kila siku wanaleta migomo vyuoni.

Tukiangalia kwa upana zaidi tunaona kwenye upande wa elimu serikali haijatilia mkazo katika swala la elimu,imekua haionyeshi jitihada kujitahidi wananchi wetu watanzania kuondokana na ujinga through education,lakini insted tumeshuhudia serikali yetu ikikandamiza sekta ya elimu bila kuisaidia kama inavyotakiwa kwa kujenga majengo mazuri yaa shule,kutoa vifaa na maabara ya kiwango cha juu shule ziwe na vifaa vyakutosha kukidhi na kua katika viwango vinavyoitajika.

Je nitakua nakosea kusema serikali inafanya ivi makusudi ili tubaki kuwa wajinga na tusiendelee kujua lolote linaloendelea nchini kwa kutunyima taaluma ya msingi ya elimu?wanataka tubaki kuwa wajinga kila wasemalo tuone sawa kwakua hatujasoma?je mamilioni ya pesa wanayotumia unnecessarly kwa mapati yao na kadhalika, leo hii wangetumia hizo fedha kwa kujenga shule si tungekua na shule nyingi na karibu ya 80% wangekua wamefuta ujinga na wamesoma.

Hii ni wazi serikali inapenda tuzidi kuwa wajinga na kutu discourage tujione wajinga hatuna akili,ndo maana wengi wanaofeli hata form4 au form6 wanaishia mtaani kama wazee wao hawana uwezo..Nawashilisha hoja,tuchanganue jamani ningependa kujua zaidi pia nanyi wenye michango yenu
 
Kama wanajibu mitihani kwa kuandika kama ulivyoandika wewe no wonder wengi wanafeli!

Sasa ungepangilia hoja zako kwa kutumia aya ingekuwa rahisi hata kufuata kile unachokisema bila kuchoka wala kurudia rudia kusoma.

Unaonaje ukiweka aya kwenye bandiko lako?
 
sababu za kufeli zipo aina mbili kuna za kisiasa na sababu halisi. mimi nitataja sababu halisi
1. kuporomoka kwa maadili "displine" za wanafunzi na waalimu
2. kuenea kwa filamu za kijinga za kibongo na za nchi nyingine ambazo zinawajenge vijaana kuona maisha ni rahisi kama wanavyoona wahusika wakiishi kwenye filamu
3. kupoteza muda mrefu kwenye hizi filamu na miepsode isiyotija
4. wanafunzi kujihusisha na mapenzi
5.kuongezeka kwa mayatima walio na baba na mama yaani wazazi wako hai lakini role yao ni zero katika malezi kazi yao ni kuwapa chakula tu, eti baba anakaa na mwanaye anatazama ze comedi
 
Habari zenu wakuu,imekua ni jambo la ajabu sana kua unaweza kuona baadhi ya wanafunzi huwa wanafaulu karibu mihula yote wanayokuaga darasani na vidato mbali mbali lakini inakuaga vigumu sana wanafunzi hawa kufaulu form4 au form6 hata kama wanaakili au hufaulu kwa wastani basi wakifika form4 au form6 unakuta wanapata division4 au zero kabisa,wakati mitiani mingine yakuwapima unakuta wanaweza pata division1 au division2.
Hakuna hiyo kitu , either hiyo mitihani ni chini ya 'Standards' zinazotakiwa au ,
unatuhadaa ili kuondoa lawama kwa wanafunzi ambao baadhi yao wamejitakia,
Halafu NECTA haifelishi mwanafunzi yeyote...
 
Hakuna hiyo kitu , either hiyo mitihani ni chini ya 'Standards' zinazotakiwa au ,
unatuhadaa ili kuondoa lawama kwa wanafunzi ambao baadhi yao wamejitakia,
Halafu NECTA haifelishi mwanafunzi yeyote...

Acha pumba,alokwambia mitihani inakua chini ya kiwango nani?inakuaga ya standard na mara nyingi huwa wanaangalia region wise mwanafunzi gani kafaulu zaidi kabla hawajafanya NECTA
 
kwa sisi walimu wa sekondari undani wa mambo ni wanafunzi hawana mwamko na elimu kabisa. Sababu nyingine ni elimu ya shule ya msingi imekuwa bora liende form 2 hajui kusoma wa la kuandika. Wao ni bongo fleva na filamu.Tujaribu kizazi kijacho sio hich Tujari
 
Acha pumba,alokwambia mitihani inakua chini ya kiwango nani?inakuaga ya standard na mara nyingi huwa wanaangalia region wise mwanafunzi gani kafaulu zaidi kabla hawajafanya NECTA

Dear friend, those Pre Necta Exams of yours are Neither varid nor reliable. Pia marking zenu zinakuwa biasd kutokana na jinsi gani unafaham performance ya wanafunzi wako. Kamata glasi ya maji kupunguza hasira Mkuu!
 
wanazolewa kiulaini mno darasa la saba, thats why wanajiachia na kwa kuota kwamba historia itajirudia...
 
Hata mi mwenyewe najishangaa nilifeli hivyo hivyo,kwahiyo acha na wao wafeli ili tuwe sawa!!!
 
KwAni ndugu zangu,unataka kuniambia hamna mtu unayemjua ambaye ashuleni kwenu alikua kichwa sana anafaulu au mtu yoyote unamjua,alafu mwisho wa siku kwenye finalas NECTA akafeli?hamna hujuma kweli kwenye kusaishia wanafunzi wetu?
 
Back
Top Bottom