Mkuu Luteni,Niliondoka nyumbani na student visa malengo yangu yalikuwa shule kwanza ila sikuwa na tuition fees hata senti tano nilichuma matunda Sweden kwa mwaka mmoja ili nipate fees haikutosha rafiki yangu akaniambia kuna kazi Poland inalipa vizuri tukaelekea huko tukafanya kazi mwaka mmoja kazi zikaanza kupungua bado fees haijatosha tukaona wapolo wameanza kuelekea UK wanakolipa vizuri tukajiunga ndani ya nyumba ya malkia kazi ikakubali recession ikaharibu mahesabu visa ikawa inaelekea ku expire, nikatafuta chuo nikapata visa ikaleta matatizo kwa vile nilikuwa nimelipa kiasi chuo kikanisaidia ku extend nikapiga kitabu kwa mwaka mmoja nikavalishwa joho. Baada ya kumaliza chuo nikaanza kutafuta kazi ya profession yangu huko UK hadi sole ya safety boots ikaenda upande nilichokuwa napata ni zile zile kazi nilizokuwa nafanya kabla ya shule yaani kubeba mabox. Baada ya miezi kama sita hivi nikajiuliza hii shule yangu itanisaidia nini huku uamuzi niliochukua ni kubeba mikoba yangu na kutafuta next flight nyumbaniiiiii kwa baba na mama. Bahati iliyoje nilipofika tu kwa kutumia ujuzi wangu nikapata kazi ya kujiajiri au ya kuajiriwa hiyo ni siri yangu.
Wakati wewe ulikuwa unatafuta kazi ya kuajiriwa, kuna wenzako wengi tu wana create hizo kazi (wanajiajiri).
Nafikiri tukubali tu hapa kwamba kila binadamu ni tofauti na hakuna solution moja kwa matatizo yote ya binadamu.
Wakati wewe unasema ulirudi TZ na kupata kazi, kuna Watanzania wengine wengi tu wanarudi na wanabaki kusota bila kazi.
Ndio maana wengine tunasema, suala la nani anaishi wapi na anafanya nini, ni la mtu binafsi na hakuna haja kuingilia uhuru wa mtu binafsi.
Nyie kama mnaweza basi tengenezeni opportunities nyingi TZ na vijana wa dunia watapima na wakiona kuna mengi ya kuwafaa TZ basi watakuja tu. Hawahitaji kushikiwa mjeredi kurudi kwao; wanachohitaji ni kuona opportunities na mazingira ambayo yanaridhisha nyoyo zao.