Kwanini waislam wa tanzania wanawachukia ndugu zao wakristo?

Mkuu Mzizi Mkavu, mpiga picha maatufu wa ITV na muumini wa madhehebu ya Ahammadiya. Asante kwa somo lako la leo. Ni kweli mwislamu kamili hawezi kufanya ya kijinga ka yaliooneshwa Mbagala. Ule ni kuudhalilisha uislamu.Mwislamu gani akaibe kanisani, kwa shida ipi?
 
Mkuu Mzizi Mkavu, mpiga picha maatufu wa ITV na muumini wa madhehebu ya Ahammadiya. Asante kwa somo lako la leo. Ni kweli mwislamu kamili hawezi kufanya ya kijinga ka yaliooneshwa Mbagala. Ule ni kuudhalilisha uislamu.Mwislamu gani akaibe kanisani, kwa shida ipi?
Mimi sio mpiga picha

wala Mimi si muumini wa Madhehebu ya Ahmadiyya mimi ni Muislam wa Madhehebu ya Suni ninapinga wanavyofanya

Vijana wa Kiislam kwenda kuwachokoza Majirani zao na marafiiki zao Wakubwa wa Dini ya Kikristo hilo mimi

Sipendi hata kidogo kusikia jambo hilo. mimi ni Mtu ninayependa haki za Binadamu Usawa na Uhuru wa kuabudu

dini Mtu aipendayo pasipo na kumuingilia Mtu na imani yake.Mimi huku nilipo nje nimesha ishi na WaKristo nyumba

moja na nimesha ishi na watu toka Asia wanaabudu Ng'ombe, Budha na hakuna matatizo yoyote yale

niliyoyapata kwa hao wenye imani tofauti na mimi jambo kubwa ni kuheshimiana na kuvumiliana kila mtu na

Dini yake na imani yake huwezi kumlazimisha mtu kufuata imani yako je na wewe akikulazimisha ufuate imani yake utakubali?

Mwenyeezi Mungu anasema hivi katika kitabu kitukufu cha Quran Sura2-256

256. Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Hakuna Ruhusa ya mtu kumlazimisha mtu mwengine aingie katka Dini au imani yako kwa nguvu kila mtu atafuata imani yake apendavyo.
 
546916_479605322061556_1977607752_n.jpg
 
Historia ya Nchi hii Inachangia sana,Kuna watu mpaka leo bado wana makovu...
 
Mkuu Bujibuji hawa waliochoma moto kanisa ni Wahuni Vijana wa Watoto wa kiislam Muislam halisi

hawezi kuchoma moto Kanisa Kwa sababu Eti mtoto Mmoja wa Kikristo kakojolea Quran kwani huko kwetu hakuna Serikali? Serikali

kazi yake ni nini? Serikali inafanya kitu gani kwa hawa wanaoharibu Amani ya nchi yetu?Mambo kama hayo

hayakuwepo wakati wa Enzi ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere iweje yawepo kwa sasa?Serikali haina

uwezo wa kuwathibiti hawa wanaochafua amani ya nchi yetu?Huyo mtoto aliyekojolea Kitabu cha Waislam

angelikamatwa na polisi na kupelekwa kwenye vyomba vya Sheria sio wahuni wachache katka dini ya kiislam

wanataka kuvuruga amani ya nchi yetu Wajichukulie sheria mikononi mwao. Mimi nina laani kitendo cha huyo mtoto kukojolea kitabu cha Waislam Quran na pia nina laani

kitendo cha Wahuni wachache katika Dini ya kiislam kuvuruga amani ya nchi yetu na ninawapongeza ndugu zetu

Wakristo kwa uvumilivu wao wanao onyesha katika kila hali Mungu ndio atakao walipa wema wao.


RAIS JK ATEMBELEA KANISA LILILOSHAMBULIWA NA WAISLAMU MBAGALA




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dar es salaam na Pwani Mkosimonga uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo huko Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

Mawe yametoboa vioo vingi

Ofisi ya Kanisa imechomwa moto


Yote kwa yote Ujumbe Ulifika,Hii haiwezi kurudiwa!! Mpaka sasa kila mtu anaheshimu Dini ya Mwenzake
 
Back
Top Bottom