Kwanini waislam wa tanzania wanawachukia ndugu zao wakristo?

Eeeh!
:what:
389478_10151098399902843_503993324_n.jpg
 
Sasa wewe unaejua zaidi ni nani aliekusudiwa????????? Na nikuulize hivi wewe kweli ni Muislamu au ndio Muislamu kama mashehe wa BAKWATA?
 
Ndio hakuna Urafiki utaokuwepo baina ya Kafiri na Muislamuuuuuuuuuuuuu mbona bichwa gumu weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Mkuu Idimi Waislam wa huko Uswahilini ndio wanaoleta fujo kutokana wengi wao hao Waislam

hawakuenda shule watoto wa Masikini walala hoi Umasikini ndio chanzo kikubwa cha hao watoto wa Kiislam

wa Uswahilini kufanya fujo zisizokuwa na msingi wowote si unajuwa Matatizo ya ajira nchi mwetu. Tofauti na

Waislam wa kutokea Sehemu Masaki,mbezi beach,Oysterbay ni Sehemu za watu Matajiri kuna waislam Matajiri

na watoto waliosoma Kielimu ya Dini na Dunia sio rahisi kufanya mambo hayo ya fujo Mkuu.Usifananishe Sehjemu za

uzunguni na sehemu za Uswahilini hapo Dar ni Tofauti kabisa mji mmoja lakini kila sehemu ina daraja yake.

Mkuu MziziMkavu, kwa hao wa Mbagala na Temeke tuchukulie hawajasoma, sawa, wasiosoma wapo mpaka mikoani pia. Iwapo kitabu kilichonajisiwa kinamhusu kila Muislamu, mbona wale wa mikoani hawaja andamana? Hili nalo linataka jibu! Au hawa wa Mbagala ni Waislamu zaidi kuliko wale wa mikoani. Tofauti iko wapi hapa?
 
Last edited by a moderator:
Thanks Mzizimkavu!umenigusa sana kwa ujumbe wako.Mimi ni mkristo lakini mchango wako hapa,wa uwazi na mwingine nikuombao kupitia Private Messages)PM) umekuwa kamwe hauna chembe ya ubaguzi.Mungu akubariki sana!
 
HADHI YA YESU
Je wale Waislamu waliokuwa kwenye jopo la wazungumzaji, walikuwa wakijaribu kukonga nyoyo za watazamaji wa Televisheni kinyume na

sera au kwa kutumiya uwongo au kwa kutumiya diplomasiya? La hasha! Hapakuwa na kitu cha namna hiyo. Waislamu hao walikuwa

wakiyasema yale ambayo MwenyeziMungu, katika Qur'an, amewaamrisha kuyasema. Haikuwa hiyari yao bali walilazimika kusema kwa

kutumiya maneno mengi tu kuwa- "Sisi Waislamu tunaamini kuwa Yesu alikuwa mmoja wa Mitume wakubwa wa MwenyeziMungu,

kwamba yeye ndiye Masihi, kwamba alizaliwa kimiujiza-bila maingiliyano ya jinsiya ya kiume na ya kike ( jambo ambalo Wakristo wengi

wa leo hawaliamini), kwamba aliwafufuwa wafu kwa idhini ya Mungu, na kwamba aliwaponya vipofu na wakoma kwa idhini ya Mungu.

Kwa kweli Muislamu hawi Muislamu kama hamuwamini Yesu!"Mkuu mayanga


 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu Waislam hichi kitu hawakijuwi hata kidogo hebu Someni hapa chini Waislam Wenzangu.

UADUI WA MAYAHUDI NA URAFIKI WAWAKRISTO
Aya 82 - 86
Maelezo yanaanzia na Aya 82 iliyokuwa mwisho wa juzuu ya sita, kwa vile inaungana hapa.

MAANA
Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu wengine kwa walioamini ni mayahudi na washirikina. Yaani mayahudi na washirikina ndio waliokuwa maadui zaidi kwa Waislamu. Mara nyingi watu wameitolea ushahidi Aya hii, kuwa dini ya kikristo iko karibu zaidi na Uislam kuliko dini ya kiyahudi. Hilo ni kosa ikiwa inakusudiwa dini ya kiyahudi na ya kikristo kabla ya kugeuzwa. Kwa sababu dini kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake ni moja tu kwa upande wa itikadi na msingi yake. Na kama ikikusudia baada ya kubadilishwa, basi zote mbili ni sawa (Ukristo na Uyahudi) hakuna yenye afadhali.


Usahihi ni kuwa uhasama wa mayahudi na washirikina katika Uislam unatokana na mgongano baina ya mwito wa kiislam na tabia iliyokuwa imeshika kasi katika Bara arabu mwanzo wa utume. Tabia hiyo ilikua ni mashindano ya kupora mali na watumwa. Vilevile riba, ghushi na mengineyo ya kutumia nguvu na utapeli. Tabia hii iliambukiza wafanyibiashara wa kigeni, kama walivyoambukizwa viongozi wa kiyahudi waliokuwa wakimiliki viwanda na biashara ya ndani.


Ukaja mwito wa Muhammad (saw) unaohimiza uadilifu na kukataa dhuluma na unyonyaji wa aina zote, na kuzuia unyonyaji wa mayahudi na washirikina. Kutokana na hali hiyo ndipo pande zote mbili zikakutana na kukubaliana kwa pamoja kujiepusha na dini na itikadi na kuungana mkono kupigana na Muhammad (saw), adui wa wote wawili.


Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa uadui wa mayahudi na washirikina kwa waislam, ulikuwa ni kwa msukumo wa kidunia na wala sio wa kidini, lakini mayahudi walijificha nyuma ya pazia la dini kwa kujionyesha na unafiki; sawa na wafanyavyo leo watu wanaotafuta chumo la haramu. Zaidi ya hayo ni kuwa mayahudi na washirikina wanashirikiana katika ubaguzi. Lakini washirikina pamoja na ujahili wao walikuwa na moyo usiokuwa mgumu, wakarimu na wenye fikra huru zaidi ya mayahudi. Ndio maana wengi wao wakamwamini Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na ni mayahudi wachache tu ndio waliomwamini Muhammad.


NI NANI WALIO KARIBU NA WAISLAMU KIMAPENZI.
Na utawakuta walio karibu zaidi kwa mapenzi na waumini ni wale waliosema sisi ni Wanaswara (WaKristo). Baadhi wanaichukulia Aya hii na iliyo baada yake ni chombo cha kukoroga mambo, kwamba Uislamu unaelemea mojawapo ya majeshi mawili hivi sasa. Jambo hili ndilo lililotufanya tufafanue Aya hizi nne kwa namna ambayo haitaacha nafasi kwa wale wanaobadilisha mambo.


Hakika mwenye kuziangalia vizuri Aya hizi, hawezi kuwa na hata chembe ya shaka kuwa zinakamilishana na kwamba haifai kabisa kuifasiri moja pekee yake bila ya kuichanganya na wenzake. Nazo ziko wazi kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakuwafanya bora manaswara, kwa ujumla, kuliko makundi mengine katika kuwa karibu kiurafiki, si kwa umbali wala karibu. Isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) alikusudia kikundi maalum kutoka manaswara (wakristo) kwa dalili ya kuwa yeye hakuishia hapo tu bali aliendelea kusema: "Hayo ni kwa sababu wako miongoni mwao makasisi na watawa, na kwamba wao hawafanyi kiburi." Tena akaendelea kusema: Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa mtume, utaona macho yao yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua; wanasema: "Mola wetu! Tumeamini basi tuandikie pamoja na wanaoshuhudia."


Maana yake ni kuwa miongoni mwa manaswara (wakristo) wako walioujua Uislamu,wakaukubali kwa kutii, kukinai na kwa imani.


Historia inathibitisha hivyo; kama ambavyo inathibitisha chuki ya manaswara kwa Uislam na Waislam. Kwa mfano: Fedheha ya Wataliano huko Tripoli ya Magharibi, na Wafaransa katika Algeria, Tunisia, Morocco na Syria. Vile vile fedheha ya Waingereza katika Misr, Iraq, Sudan n.k. Na leo hii1 Marekani wanaaungana na mayahudi katika kulingamiza taifa la Palestina. Wanawapa silaha za kisasa maharamia hawa, kisha wanafanya uchokozi na kudai kuwa wao ndio waliochokozwa na kuungwa mkono na Marekani katika Baraza la Usalama na Umoja wa mataifa. Hapo Marekani husema: Huu ndio ukweli uadilifu na demokrasia.


"Na kutoa Bishara ya Mjumbe atakayekuja baada yangu aitwaye Ahmad" (61:6) Hayo, bila shaka, yanatiliwa mkazo na kukanushwa na kauli yake Mwenyezi Mungu aliyoifuatilia bila ya upambanuzi wowote isemayo: Basi Mwenyezi Mungu atawalipa, kwa yale waliyosema, Bustani zipitazo chini yake mito, humo watakaa milele na hayo ndiyo malipo ya wafanyao mema. Ushahidi wa wema na kulipwa pepo kwa kundi hili la wakristo ni dalili ya mkato ya kusilimu, na kwamba ndilo pekee lililokusudiwa baada ya kusifiwa wema na thawabu.


Ama wakristo ambao wameikana haki baada ya kuijua au wakaipinga bila ya kuangalia dalili zake na ubadhirifu wake, hawa wamekemewa na Mwenyezi Mungu na kuwapa kiaga kwa kusema: Na wale waliokufuru na kuzikadhibisha Aya zetu hao ndio watu wa Motoni. Unaweza kuuliza kuwa kauli ya waliokufuru na kuzikadhibisha Aya zetu, inamhusu kila mwenye kukufuru na kukadhibisha. Sasa je, kuna wajihi gani wa kuhusisha wakristo?


Jibu: Mfumo wa maneno unafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) baada ya kuahidi pepo wenye kuamini katika wakristo, amewaahidi moto wenye kung'ang'ania ukafiri miongoni mwao. Ameleta neno la jumla, ili kujumuisha kemeo kwa kila mwenye kuihalifu haki na kuipinga, jambo ambao halipingani na yale tuliyoyasema.


Kwa ufupi ni kuwa Aya hii iko wazi kuwa makusduio ni kundi mahsusi katika wakristo - wale waliojua haki na kuiamini. Na kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawaingiza peponi kwa sababu ya imani yao na amali yao njema. Tukikadiria kuwa kauli yake Mwenyezi

Mungu: "Na utawakuta walio karibu kwa mapenzi na waumin ni wale waliosema sisi ni manaswara," inawakusanya wakristo wote, basi itawajibika tuiache dhahiri ya Aya na tuihusishe na wale walioamini katika wao kwa sababu mbili: Kwanza, kwamba Mwenyezi Mungu

(s.w.t) ametaja katika Aya kadhaa kuwa manswara wamemfanyia Mungu washirika, wakaficha jina la Muhammad (saw) na

wakawafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akakataza

kuwafanya mayahudi na manswara kuwa marafiki. Na akasema: "Enyi Mlioamini msiwafanye marafiki mayahudi na manswara." (5:51)

Tukiunganisha Aya hii, na zilizo mfano wa Aya hii, juu ya kauli yake Mwenyezi Mungu na utawakuta walio karibu zaidi kwa mapenzi na

waumin ni wale waliosema sisi ni manswara," maana yanakuwa: "Miongoni mwao wako watu washikao njia ya wastani, na wengi wao wanayoyafanya ni mambo mbaya" (5 : 66)



Pili, ni kuwa wafasiri wanasema, Aya hii tunayoizungumzia ilishuka kwa sababu ya Najashi, mfalme wa Uhabeshi2 aliyekuwa mnaswara (Mkiristo). Kwani Mtume (saw) alipoona adhabu inayowapata sahaba zake kutoka kwa washirikina, mwanzo mwanzo wa mwito wa Uislam, aliwaamuru kuhamia Uhabeshi na kuwaambia: "Huko kuna mfalme ambaye hadhulumiwi mbele yake yeyote." Wakaenda huko, miongoni mwao akiwemo Jafar bin Abu Talib. Wakapata amani kwa Najashi na ujirani mwema. Hilo lilikuwa mnamo mwaka wa tano wa kutangazwa Utume.


Zimekuja Hadith Mutawatir kuwa Najashi na Baraza lake, la Mambo ya dini na mambo ya kidunia, walisilimu mikononi mwa Jafar bin Abu Talib baada ya kuwasomea Aya za Qur'an Tukufu na kutaja mazuri ya Uislam. Na kwamba walibubujikwa na machozi waliposikia Aya za Mwenyezi Mungu.


Baada ya hayo tunasema kwamba yule anayetolea ushahidi kauli ya Mwenyezi Mungu (Na utawakuta walio karibu zaidi kwa mapenzi na waumin ni wale waliosema sisi ni manswara) kwamba ukristo na wakristo kwa ujumla wote wako karibu zaidi na Uislamu na waislamu kuliko wengine, na kunyamazia Aya zinazokamilisha Aya hii, anayefanya hivyo huyo hakijui Kitabu cha Mwenyezi Mungu au ni mwenye kujionyesha tu kwa kutaka kuongeza chumvi kwa kuutumia Uislamu na Qur'an au anaweza kuwa ni mhaini anayezitia sumu fikra dhaifu katika Uislamu ili zikubali madai ya maadui wa dini, wanaowasaidia Israil na kuwapongeza kwa uchokozi wao kwa Waarabu na Waislam. 2 Sasa ni Ethipia
 
Mkuu MziziMkavu, kwa hao wa Mbagala na Temeke tuchukulie hawajasoma, sawa, wasiosoma wapo mpaka mikoani pia. Iwapo kitabu kilichonajisiwa kinamhusu kila Muislamu, mbona wale wa mikoani hawaja andamana? Hili nalo linataka jibu! Au hawa wa Mbagala ni Waislamu zaidi kuliko wale wa mikoani. Tofauti iko wapi hapa?
Mkuu Idimi Nimeshakuambia wale Waislam waliochoma Makanisa ni watoto wa mitaani Wahuni na walala hoi wazazi

wao hawakuwasomesha shule masikini hawana kazi, kazi yao uwatume wakafanye fujo. Muislam wa ukweli hawezi

kwenda kuchoma moto makanisa eti kwa sababu watoto wawili walioshindana kuhusu dini Mmoja wapo akakojelea msahafu? Hicho

kitu kwa Waislam wenye elimu zao haitawezekana kwenda kuchoma Moto Makanisa. Kosa la mtu mmoja ukawahukumu

watu wote kwanini? Samaki mmoja akioza basi wote watakuwa wameoza? Watu siku hizi wanachanganya Dini na Siasa

pamoja sijuwi kwanini? Kama una chuki na mtu jaribu kuzizuia chuki zako moyoni mwako usizitowe nje. WaKristo

wameumbwa na Mwenyeezi Mungu na wanamuamini Mungu na Waislam pia wameumbwa na Mwenyeezi Mungu na wana muamini Mwenyeezi Mungu kila mtu na imani yake

Mkristo muache aende kanisani na Muislam Mwache aende Msikitini tungoje siku ya mwisho nani atakuwa ni mkweli

tuwe na uhuru wa kuheshimiana katika Masuala ya Dini tuache tofauti zetu jamani tunakwenda wapi? Boko Haram au

Wapi jamani Palestina na Wa Israil? Tuache mambo ya ujinga kila mtu amuheshimu mwenzake anaye anzisha

uchokozi kwa mwenzake tumpeleke Serikalini ndio itakayo muadhibu kwani huko kwetu hakuna Serikali? Serikali

inafanya kazi gani? Tuache mambo ya chuki zetu jamani tuwe kitu kimoja kujenga nchi yetu asanteni.
 
Last edited by a moderator:
Sasa wewe unaejua zaidi ni nani aliekusudiwa????????? Na nikuulize hivi wewe kweli ni Muislamu au ndio Muislamu kama mashehe wa BAKWATA?

Unataka kutuambia wewe ndo mteule wa Allah ambae umepewa mamlaka au uwezo wa kupima uislam wa mtu!!? wewe uislam wako aupime nani?
 
Nimelipenda hilo bango la kanisa hakika Wakristo wa hapa JF wangekuwa kama hao hata mimi ningeamia chadema
 
HADHI YA YESU
Je wale Waislamu waliokuwa kwenye jopo la wazungumzaji, walikuwa wakijaribu kukonga nyoyo za watazamaji wa Televisheni kinyume na

sera au kwa kutumiya uwongo au kwa kutumiya diplomasiya? La hasha! Hapakuwa na kitu cha namna hiyo. Waislamu hao walikuwa

wakiyasema yale ambayo MwenyeziMungu, katika Qur'an, amewaamrisha kuyasema. Haikuwa hiyari yao bali walilazimika kusema kwa

kutumiya maneno mengi tu kuwa- "Sisi Waislamu tunaamini kuwa Yesu alikuwa mmoja wa Mitume wakubwa wa MwenyeziMungu,

kwamba yeye ndiye Masihi, kwamba alizaliwa kimiujiza-bila maingiliyano ya jinsiya ya kiume na ya kike ( jambo ambalo Wakristo wengi

wa leo hawaliamini), kwamba aliwafufuwa wafu kwa idhini ya Mungu, na kwamba aliwaponya vipofu na wakoma kwa idhini ya Mungu.

Kwa kweli Muislamu hawi Muislamu kama hamuwamini Yesu!"Mkuu mayanga



Ndugu mzizi mkavu nakuomba usome biblia ili upate jibu kuhusu bikra maria alipataje ujauzito mpaka Yesu akazaliwa uone kama kuna tofauti na maelezo yako!! naona kama umechemka kuhusu wakristo wanavyoamini jinsi ujauzito huo ulivyopatikana!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom