Kwanini waislam wa tanzania wanawachukia ndugu zao wakristo?

Tamko la Askofu mkuu wa TAG kuhusu makanisa yaliyochomwa!




Oktoba 12 mwaka huu, matukio mabaya na yenye kutia doa sifa ya amani umoja na Utengemano wa Taifa la Tanzania, yalijitokeza huko Mbagala Jijini Dar es Salaam, wakati watu wenye jazba wanaoaminika kuwa ni Waislamu wenye msimamo mkali walipovamia makanisa saba …na kuyachoma moto eti kwa kulipiza kisasi cha mtoto aliyekojolea kuran katika utani wa kitoto.Katika mkasa huo ambao ni kama muendelezo wa

ghasia zingine zilizotokea kule Zanzibar miezi michache iliyopita na kuteketeza makanisa mbalimbali mbali na kuharibu mali za kanisa na zile za watu binafsi.


Tukio la Mbagala limesababisha makanisa saba kuharibiwa vibaya, mali kuibiwa na hata kuhatarisha maisha ya watanzania na kuwafanya waishi kwa hofu na kupoteza matumaini.


CHANZO CHA TUKIO


Kwa mujibu wa walioshuhudia, Polisi na wahusika (Waislamu) chanzo cha ghasia hizo na mabishano ya kitoto baina ya watoto wa dini ya

Kiislamu na kikristo, waliobishana kuwa ikiwa mtu atakojolea kuran na kuitemea mate atageuka mbuzi au nyoka.


Lakini baada ya tukio hilo la kitoto watu walilikuza na kulipeleka kwenye misikiti na hivyo kuchocheza ghasia. Kimsingi tukio lenyewe ni jepesi

sana ukilinganisha na matokeo yake. Ukweli kwamba waliofanya utani huo ni watoto na chanzo chake ni mabishano ya kitoto, unatia shaka kuwa

huenda kuna hoja nyuma ya pazia ambayo isipotazamwa kwa makini inaweza kulete matokeo mabaya sana.


Jambo linalonitia shaka ni kufanana kwa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa ya Zanziabar na ya Mbagala ambapo hakukuwa na uhusiano wa vyanzo vya ghasia na makanisa husika.


Mfano; Ghasia za Zanzibar zilizopelekea kuangamizwa kwa makanisa zinaelezwa kuwa zilitokana na kikundi cha Kiislamu cha Uamsho wa

Mihadhara, kilichokuwa kikiandamana kudai mjadala wa Muungano, lakini zikaishia kwenye uchomaji wa makanisa, hapa hauonekani uhusiano wa kanisa na Muungano; nalazimika kujiuliza kulikoni?


Vivyo hivyo tukio la Mbagala halina uhusiano wa moja kwa moja na kanisa kwa kuwa hakuna ushahidi wala hata tetesi kuwa mtoto huyo alitumwa

na kanisa lolote. Wahusika wa dini ya Kiislamu akiwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, analielezea tukio la kitoto kama lisilostahili

hata mtu kufunguliwa mashtaka bali kuelekezwa tu. Ni vipi lisababishe uchomaji wa makanisa?


MAKANISA YALIYOCHOMWA MOTO


Katika ghasia hizo za aina yake, makanisa saba yamethibitishwa kuharibiwa kwa kuchomwa moto, kupasuliwa vioo, viti na kuibiwa vyombo vya

muziki na jenereta. Makanisa hayo ni TAG Kizuiani, Agape, Kibonde maji, SDA Sabato, Mbagala Kizuiani, Katoliki Kristo Mfalme Mbagala

Rangi Tatu, Anglican Mbagala Kizuiani, KKKT, Mbagala Zakhem na TAG, Shimo la Mchanga.


Pamoja na majengo hayo kubomolewa kwa viwango tofauti mengine yakichomwa moto, pia wahusika waliiba Genereta, na vyombo vya muziki vya makanisa hayo na kuvunja magari na baadhi yao kuchomwa moto.

Choko choko zilizinazoweza kuwa chanzo cha matukio hayo ni:

Januari sita mwaka huu, kikundi kimoja kinachoitwa JUAKITA, kiliitisha kongamano la kujadili katiba mpya Tanzania, kwa upande wa Waislamu.

Katika kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kulitolewas kauli za kichozi kama:

1. Lazima Rais ajaye atoke Zanzibar
2. Kukabiliana na ukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo
3. Kupinga Muungano ili kuupa nguvu Uislamu
4. Kupigana kufa na kupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa katiba mpya.

Kauli hizo zilitolewa na Sheikh Nasoro Mohamed, kutoka Zanzibar, ambaye alikuwa mgeni rasmi. Baadaye zikaandaliwa kanda za CD zilizosambaza ujumbe huo.
Uchunguzi unaonesha kuwa uchochezi huu umekuwa ukiwaandaa watu kusubiri vijitukio vidogo tu ili kulipua ghasi. Tuliona jinsi makanisa yalivyochomwa kule Zanzibar. Kwa kuwakumbusha tu, Makanisa yaliyoangamizwa katika tukio hilo ni: EAGT, Elimu Pentecost na TAG, Anglikana, Katoliki na FPCT.
Ni jambo la kusikitisha kuwa matukio haya yanatokea siku mbili tu kabla ya maadhimisho ya miaka 13, ya kifo cha Rais wa Kwanza, Mwl. Julius kambarege Nyerere. Leo hotuba na midahalo inarindima kila mahali kumuenzi Nyerere, lakini wengi wetu tukiwa tumejaa majozi baada ya nyumba zetu za ibada kuharibiwa katika matukio yanayoashiri hatari kubwa.
Hofu yangu ni kuwa, roho hii ya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliifananisha na dhambi ya kula nyama ya mtu, imekuwa ikiyatafuna mataifa ya Afrika kama ifuatavyo:

  1. Mwaka 2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu (Sharia), lilianza kwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka michache baadaye majimbo kadhaa yakajitangazia sheria hizo na tangu wakati huo kumekuwa na mapambano yasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo 500 wameuawa kikatili na makanisa kuchomwa moto.
  2. Roho hii imekuwa ikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya Afrika ambapo imelikumba taifa la Mali, majimbo ya kaskazini tayari yametangaza kujitenga na kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya silaha.
  3. Itakumbukwa kuwa miezi michache tu ilizopita vuguvugu hili la kudai utawala wa kidini liliibuka nchini Kenya ambapo watu wanaojiita wanaharakati walianzisha madai ya kutaka eneo la Pwani kujitenga na Jamhuri ya Kenya na kujitangazia taifa la Kiislamu.
  4. Katika tukio hilo inasemekana mtoto huyo alitengenezewa mabishano ya kitoto kuwa akichoma kurani atakuwa chizi naye akabisha kisha akapewa kiberiti na kurani akachoma tena walioandaa mzaha huo wakamkamata na kumpeleka mahakamani.

Tukio linalofanana na hilo lilitokea tena Bagamoyo mkoani Pwani ambapo mtoto wa kike alishtakiwa na hata kuhukumiwa kifungo kwa madai ya kuchoma kuran lakini tukio lilikuwa katika mabishano ya midhaha ya kitoto.WITO WANGU


Natoa wito kwa Wakristo wote nchini kujiepusha na mizaha inayoweza kutengeneza sababu za kulipuka kwa ghasi na kutengeneza mwanya wa watu wenye nia mbaya kutekeleza agenda zao zaria Ili kulinda amani umoja na utengemano wetu, nawasihi viongozi wa makanisa kuonya na

kukemea waumini na watoto wetu wasishiriki kwa namna yoyote ile mizaha inayopelekea kuchoma au kuharibu vitabu au nyaraka za kidini.


Nawasihi watanzania wote kwa ujula kujiepusha na mizaha ya kidini inayoweza kuchafua amani yetu, na pale jambo lolote lenye kukera

linapotokea tujiepushe kuwa mawakala wa shetani wa kueneza chuki badala ya amani na upendo.


USHAURI WANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI


Nawashauri viongozi wa Serikali ambao leo wanatoa matamko na kushiriki midahalo ya kumuenzi Mwl. Nyerere kukumbuka kuwa huyo alikuwa

na mapenzi makubwa na amani na umoja wa taifa. Kwa hiyo kumuenzi kwa vitendo ni kudumisha utawala bora, unaofuata sheria usio na chembe ya ubaguzi wa aina yoyote.


Kulipuka majukwaani kumuenzi Nyerere bila kuilinda na kuitetea amani ya nchi ni kujidanganya.


Ni wajibu wa kila Mtanzania kutii sheria na mamlaka kwa kuwa zimewekwa/kuruhusiwa na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi. Hivyo kila Mtanzania anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii mamlaka.


Viongozi wenzangu wa dini wakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika jamii, na jamii inawasikiliza hivyo ni vyema wakawa makini katika

matamshi na maelekezo yao ili wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu za kidini na uvunjaji wa amani.

Pia ningependa kuwashauri viongozi wa serikali kusimama imara katika kusimamia sheria na haki, na kuepuka kauli au vitendo vitakavyofanya baadhi ya watanzania kudhani kuwa hawatendewi haki.

Ni vema ieleweke kuwa matukio kama haya ya uvunjaji wa amani yasipodhibitiwa na kukomeshwa haraka yanaweza kuumba chuki ambayo

inaweza kuibua mlipuko mkubwa na machungu kwa wananchi na matokeo yake yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na busara inatufundisha kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta.


Ni vyema wenye dhamana ya kuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele ya Mungu aliyewaweka au kuwaruhusu kuingia madarakani na siku moja watatoa hesabu mbele zake.


Ni vyema viongozi wa Serikali wakajizuia kufanya maamuzi yanayoashiria upendeleo kwa baadhi ya makundi ya kidini na kukiuka utawala wa sheria, mfano; kutii waandamanaji na kuwaachia bila mashrti watu waliokamatwa kwa mujibu wa sheria kuna jenga kiburi kwa makundi yenye kiu ya matumizi ya nguvu na kujenga hofu kwa pande zingine.


Ni vyema mamlaka zikasiamama katika sheria na kufanya hukumu kulingana sheria badala ya kuamua mambo ya kisheria kisiasa.


WITO MAALUMU KWA VIONGOZI WA DINI


Nitumie nafasi hii kuwasihi vingozi wenzangu wa dini, kusimama imara katika kuombea taifa na kuhubiri kwa nguvu ili kukabiliana na giza la kiroho ambalo linatishia kuifunika nchi.


Takwimu za karibuni kabisa za utafiti uliofanywa na taasisi ya Washnton DC iitwayo, Pew Research Centre, na kurushwa na Televisheni ya CNN,

Katika kipindi chake cha Inside Africa, zilionesha kuwa watanzania asilimia 93, wanaamini mambo ya ushirikina na uchawi wakati Uganda ni

asilimia 29 na Kenya ni asilimia 27 Tu. Mahali ambapo giza la kiroho limezingira kiasi hiki ni lazima matukio ya kishetani yashamiri tuchukue hatua.


Mwisho, natoa wito kwa watanzania wenzangu tuulinde umoja, amani na utengamano wa taifa letu, tuikimbie dhambi ya ubaguzi kwa kuwa

tukiiruhusu itatuangamiza sote. Tuliombee taifa letu na kukiwa na mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya majadiliano na vikao vya pamoja vinavyohusisha viongozi wa dini zote na serikali pia.



Imetolewa leo 14/10/2012
Na Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu Mkuu wa TAG

–Sam Sasali blog
 
Jamani mimi ni mkristo, ila katika makuzi yangu, shuleni, kazini na sasa nina famila asilimia kubwa ya watu waliopata kuwa marafiki zangu wa karibu ni waislamu. Hata sasa tunavijiwe vyetu vya kupumzika baada ya kazi, hapo tunachanganyikana wailslamu na wakristo. stori kwa kwenda mbele na utani kemkem huku tukisukuma drafti. Mara huyu kaitwa shekh, mara ustaadh, mwingine kaitwa mwinjiristi au baba paroko, sometime pastor. wengine wataitwa mama, pokoro au mchumba. Alimradi mzaa na utani wa kila aina, WOTE TUNAPENDANA.

Kwa hiyo sikubaliani kuhitimisha kwamba wakristo na waislam TZ hatupendani, lahasha. Kuna watu wachache wanalazimisha ijulikane hivyo kwa manufaa yao.

Hata hivyo Kikwete na utawala wako mnachangia sana haya mambo kuwa kama yalivyo. Kwa sababu Kikwete ni mwisilamu pia basi watu tunadhani kuwa unashabikia 7bu wewe pia ni sehemu yao wakati si kweli.

Rais gani unaendekeza mambo hatari kama haya katika taifa lako? Ndio maana watu wanakuita dhaifu bila kupenda. Karipia kwa kukaza uso na si kutabasamu wakati wote
 
Wapendeni adui zenu waombeeni wanaowaudhi kama mkiwapenda wale wanaowapendeni ninyi mnafanya kitu gani cha ziada.? Hata mbwa anampenda yule anayemtunza dini ya kweli uhubiri upendo, kusamehehana na kuvumiliana dini inayohubiri chuki,kulipa visasi na vurugu nina mashaka nayo kheri yangu mimi mpagani.
 
MziziMkavu Ningefurahi kama watu wangefahamu kuwa waislam wote sio bin laden, boko haram au al shabab. Waliochoma moto kanisa hawafiki hata 0.001% ya waislamu wote, kwanini wote tunaonekana ni magaidi na wenye roho mbaya.

Au ndo ule usemi wa samaki mmoja akioza..... unaaply hapa?
 
Nimeinukuu kua hakuna undugu baina ya Muislam na Mkiristo katika Surat Tawba aya ya 23.....kama hujui nitafute nikufahamishe au tafuta Mshahafu unaotafsiri kiswahili
 
MziziMkavu Ningefurahi kama watu wangefahamu kuwa waislam wote sio bin laden, boko haram au al shabab. Waliochoma moto kanisa hawafiki hata 0.001% ya waislamu wote, kwanini wote tunaonekana ni magaidi na wenye roho mbaya.
Au ndo ule usemi wa samaki mmoja akioza..... unaaply hapa?

Ni kweli kwamba si Waislamu wote wana roho mbaya, kama ilivyo kwamba si Wakristo wote wenye roho nzuri. Lakini kuna maswali kadhaa sijajibiwa hapa JF, naomba MadameX na wengine kama mna majibu sahihi basi mnijibu
1. Waislamu wako Tanzania nzima, kwa nini vurugu na maandamano mengi yapo Dar Es Salaam pekee? Kwamba Waislamu wa Dar ni 'Waislamu' zaidi kuliko wa mikoani?
2. Maandamano mengi ya Dar ni ya 'Uswahilini' sijasikia maandamano kutokea Masaki, Mbezi Beach na Oysterbay, kwanini? Waislamu hawaishi maeneo hayo?

By the way siungi mkono kitendo cha kunajisi kitabu kitukufu cha Waislamu.

 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kwamba si Waislamu wote wana roho mbaya, kama ilivyo kwamba si Wakristo wote wenye roho nzuri. Lakini kuna maswali kadhaa sijajibiwa hapa JF, naomba MadameX na wengine kama mna majibu sahihi basi mnijibu
1. Waislamu wako Tanzania nzima, kwa nini vurugu na maandamano mengi yapo Dar Es Salaam pekee? Kwamba Waislamu wa Dar ni 'Waislamu' zaidi kuliko wa mikoani?
2. Maandamano mengi ya Dar ni ya 'Uswahilini' sijasikia maandamano kutokea Masaki, Mbezi Beach na Oysterbay, kwanini? Waislamu hawaishi maeneo hayo?

By the way siungi mkono kitendo cha kunajisi kitabu kitukufu cha Waislamu.

Mkuu Idimi Waislam wa huko Uswahilini ndio wanaoleta fujo kutokana wengi wao hao Waislam

hawakuenda shule watoto wa Masikini walala hoi Umasikini ndio chanzo kikubwa cha hao watoto wa Kiislam

wa Uswahilini kufanya fujo zisizokuwa na msingi wowote si unajuwa Matatizo ya ajira nchi mwetu. Tofauti na

Waislam wa kutokea Sehemu Masaki,mbezi beach,Oysterbay ni Sehemu za watu Matajiri kuna waislam Matajiri

na watoto waliosoma Kielimu ya Dini na Dunia sio rahisi kufanya mambo hayo ya fujo Mkuu.Usifananishe Sehjemu za

uzunguni na sehemu za Uswahilini hapo Dar ni Tofauti kabisa mji mmoja lakini kila sehemu ina daraja yake.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna undugu uliokuwepo kati ya Muislam na Mkiristo
Mkuu mtwana una uhakika unachokisema lakini? Udugu ninaozungumzia sio udugu wakuzaliwa Baba mmoja mama mmoja . Udugu uliopo ni kuwa urafiki wa karibu baina ya Waislam na Wakristo upo tangu Tupate Uhuru wetu toka kwamkoloni ndio udugu ninaozungumzia simanishi udugu wa baba mmoja na mama mmoja jaribu kunielewa vizuri.

Nimeinukuu kua hakuna undugu baina ya Muislam na Mkiristo katika Surat Tawba aya ya 23.....kama hujui nitafute nikufahamishe au tafuta Mshahafu unaotafsiri kiswahili
Mkuu mtwana umetoaaya Suratil Tawba Aya Ya 23 haiuhusiani na Udugu baina ya waKristo na Waislam. Mbona unatoa aya na maelezo yako yapo tofauti na maelezo ya Aya uliyotoa?

Suratil Tawba Sura 9.23 23. Enyi mlio amini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi vyenu ikiwa wanastahabu ukafiri kuliko Imani. Na katika nyinyi atakaye wafanya hao ndio vipenzi vyake, basi hao ndio madhaalimu.

Aya hiyo uliyyo toa ina uhusiano gani na Udugu wa Waislam na Wakristo? Mbona unazungumza maneno

ya uongo?Aya haiusiani na Mambo ya Udugu wa Waislam na WaKristo? Aya hiyo inawaonya Waislam

wasiwafanye Baba zao na ndugu zenu (wa kuzaliwa baba mmoja na mama mmoja) kuwa vipenzi vyenu

Aya haikusema Waislam wasiwafanye Wakristo kuwa ni

ndugu zao mbona unachanganya mambo mkuu mtwana?kama hujuwi jaribu kuuliza utafahamishwa usiweke aya tu kichwa mchungwa hapo tupo wataalam tutakusaidia.
 
Last edited by a moderator:
Wengi wao wanatokea Uswahilini....utaniamini kwa hili wanaofanya fujo ni Temeke, Mbagala sana sana na Magome... huwezi sikia Waislam toka Msikiti wa Mikocheni au Mbezi Beach wanaanzisha vurugu za kijinga kama hizi.... Tatizo ni elimu ndogo na ukosefu wa ajira....kwa wanaofanya fujo...maana wapo vijiweni
 
409299_467902959920519_1020008608_n.jpg
 
MziziMkavu Ningefurahi kama watu wangefahamu kuwa waislam wote sio bin laden, boko haram au al shabab. Waliochoma moto kanisa hawafiki hata 0.001% ya waislamu wote, kwanini wote tunaonekana ni magaidi na wenye roho mbaya.

Au ndo ule usemi wa samaki mmoja akioza..... unaaply hapa?
Mkuu MadameX Waislam wote sio Magaidi ila kuna kundi moja ndani ya Waislam ndilo linaloharibu jina la dini ya Kiislam. Nahilo neno la Ugaidi kwa waislam limekuja wakati wa Utwala wa Rais Bush ndio uliowapa neno hilo la gaidi lakini kulikuwa hakuna neno la Ugaidi kwa Waislam.
 
Last edited by a moderator:
148800_467830643261084_1641924713_n.jpg


From Atheism to Islam: The Light
of Al-Fatihah
I Knew I Found the Religion I Had
Been Searching For::
I was asked about why I
converted and I'm sure that a lot
of my old high school pals who
have searched me and found me
on Facebook were like "What?"
because this Hijab that you see
now is not definitely what they
saw back then.
And it is not just the covering. It's
the all that I have faith because I
was a very outspoken atheist
back in the day (I'm so old now, I
can't believe how old I'm getting!).
Let's see it would be in high
school, and I had my boyfriend at
the time who was really great for
me, wasn't he?!
Anyways, it wasn't the best
relationship. He was kind of a
dungy! But it is what it is.
Anyways, then I got pregnant and
dropped out. And I gave my baby
up for adoption and blamed God
for how horrible my life was. So I
turned my back on Him, and what
can you say?
So then I healed a little bit I guess
in myself and I started searching.
Searching for the Truth
I was raised as a Lutheran. I was
baptized as a Lutheran. I
remember watching Laura and
Grint Welder at the little house
and I was excited because they
went to church and I wanted to
go to church and I asked my Mum
why we don't go to church and
she said – I'm sorry mum!-
"Because we are Lutherans, we
only go to the church for
weddings and funerals" I know
that that's a lie! But I believed her
and looking back at it now, that is
really kind of funny. But anyway
that's what we went to church
for: weddings and funerals, and
that was it.
So I found a Lutheran church and
I went to it and it was OK and got
the bible and read into it and I
didn't feel it. I didn't feel what I
saw these people around me
feeling and so I looked elsewhere.
I went into all the ‘isms'. I went
into Taoism, Buddhism, and
Judaism. I searched everything I
thought, everything. I searched all
kinds of faiths and all religions of
the world that I could find and
nothing hit home for me. And so I
gave up and I was like OK that's it,
if these things aren't right and I
can't find anything that's right
then that's it. There's nothing for
me, there is no God.
So I went back to that sort of
Atheism, but still searching. I
guess that is not really atheist if
you are searching for God, but
whatever. Then one day I was
working with a born-again
Christian girl, and this is nothing
against born-again Christians but
she was one of those born-again
Christians that was like ‘woho, off-
world cookie!'- and she was
talking about it. And I was very
good at doing "Aha, Aha, Aha!"
when people are talking to me
because I really half the time don't
care.
Anyways, she was talking to me
and then she said "When I make
love to my husband, I'm making
love to Jesus Christ!" And I was
like "What?!!" I'll let you digest
that for a little bit because it took
me a moment. And I was like "You
are off your rocker! You got to be
kidding me! How psycho are you.
You are nuts" and I went to say
that because I somehow
formulated in my mind probably
back when I was 10 or 11 years
old that I could not believe that
Jesus was the son of God. I just
thought "He is God. Why does He
need a son? He is God. Is He going
to die that He needs a son? And
Jesus walking around on earth
and eating and pooping?! That's
very ungodly to me."
So formerly I had this kind of
basis in my mind I guess to begin
with and so I had said that to her.
And she didn't like that and we
kind of had a spat, nothing
violent, but just verbal clashes
back and forth with my
somewhat atheist views against
her very strong born-again
Christian views.
And then along came my boss
who happened to be Muslim. He
set me aside and said "You have
some interesting ideas. I'm going
to bring you some literature." So
the next day he came back, I don't
know if he went to the mosque or
whatever, and he brought some
pamphlets about Islam and I
gobbled them up, I could not read
them fast enough.
And then he brought me back a
Quran and I read it. I didn't read
the whole Quran! I read the very
first chapter. It's called the
opening Surat Al-Fatihah, which is
very similar to some of the things
I guess in Christianity, but when
you are faced with the truth it's
absolutely undeniable and that
was undeniable to me. I knew it.
It's literally six or seven verses,
doesn't even take up a quarter of
a page, but I knew that I had
found the religion that I have
been searching for.
And then I was scared because
even back then, almost 13 years
ago, Islam was pretty much
synonymous with terrorism. And I
thought how can I know that this
is the right faith for me when you
are hearing about suicide
bombers and hijackers and all
these things?
But the more I studied and the
more I read into it, and I certainly
didn't just take the information
from my boss, I have a brain. I
used my brain and I studied. The
truth is the truth, no matter how
many ways you try and turn it and
spin it and wrap it, it's what it is.
And I knew that that's what I
needed to do… and I became a
Muslim… and then I married my
boss!
That's my story so I hope you all
found it interesting, or it
answered some questions

-
 
hivi tumekosa mambo ya kuandika humu mkuu? Mada za uislam na ukristu zinatusaidia nini? Mods please, be careful! Remove all of these posts and take them to Religious Issues.
 
Hata hivyo ningetegemea waislam wasio na ukorofi watoe tamko la kukaripia hao wanaofanya fujo. Nadhani shekh wa Dar amekuwa mfano kwenye hili. Speak out!
Mkuu MadameX Waislam wote sio Magaidi ila kuna kundi moja ndani ya Waislam ndilo linaloharibu jina la dini ya Kiislam. Nahilo neno la Ugaidi kwa waislam limekuja wakati wa Utwala wa Rais Bush ndio uliowapa neno hilo la gaidi lakini kulikuwa hakuna neno la Ugaidi kwa Waislam.
 
hivi tumekosa mambo ya kuandika humu mkuu? Mada za uislam na ukristu zinatusaidia nini? Mods please, be careful! Remove all of these posts and take them to Religious Issues.
Mkuu Paul Kijoka tunazungmzia kuhusu matukio yaliyotokea juzi ya Vijana wa Kiislam kuchoma moto Makanisa hatuna nia mbaya mkuu acha hasira hasira hasara.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom