payuka
JF-Expert Member
- Jun 17, 2010
- 829
- 127
Kuna wadada ving'ang'anizi sana! Unakutana nae hata wiki haijaisha anaanza kuleta habari za ndoa. Hata hamjasomana vizuri kujuana tabia yeye anaweka ndoa mbele kuliko kukufahamu wewe mwoaji.
Katika ka-research kangu kadogo nimegundua mambo yafuatayo:
Katika ka-research kangu kadogo nimegundua mambo yafuatayo:
- wadada wa aina hiyo mara nyingi huwa wanataka kuosha kwa wenzie na jamii kwa ujumla kwamba nao waliolewa kwa ndoa, potelea mbali hata kama itadumu kwa wiki moja.
- pressure kutoka kwa wenzie walioolewa.
- frequency ya kuachana na maboy-friend na yenyewe inachangia binti kutafuta permanent residence!