Kwanini vyama vya upinzani Tanzania vinashutumiana?

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Tangu umeanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa uanzishwe hapa tanzania, kitu kikubwa cha kujifunza ni uadui,chuki na kushutumiana baina ya vyama vya siasa hususan upinzani. Katika sikum za hivi karibuni,cdm imekuwa ikiibua tuhuma nzito dhidi ya cuf kuwa ni ccm B.cdm haohao wanawatuhumu TLP,NCCR na UDP kuwa sio wapinzani wa kweli.

Vyama hivyo navyo kwa nyakati tofauti huibua tuhuma dhidi ya cdm kuwa ni chama chenye ubinafsi,umimi,na kisichopenda ushirikiano.mfano mzuri ni huko bungeni ambapo upinzani umegawanyika katika suala la posho kwa wabunge, kuunda kambi ya upinzani na katika suala la katiba mpya...........

Swali-Je,nini mustakabali wa vyama vya upinzani tanzania, kwa nini chadema ina ugomvi na vyama vya upinzani.
Je,chadema itadumu chama gani kingine kitakachoweza kuibuka kama kilivyowahi kuibuka NCCR,CUF na sasa CHADEMA?
 
Kwakuwa kila chama kilianziswa kwa sera zake huwezi kulazimisha kwamba ni lazima wakubaliane.Kama chama kinapinga ufisadi nakingine kinaukumbatia sasa utalazimishaje kwamba waungane, kwakuwa ni wapinzani.Nadhani chamaana ni watanzania kuona na kutambua nichambagani chenye mlengo unaoutaka wewe,la sivyo kama vikiungana hakuna hata maana ya vyama vingi kwani cvitakuwa chama kimoja.
 
Ni lazima vishutumiane kwasababu licha ya kwamba vyote vina malengo ya kuongoza,kila kimoja kina malengo ya tofauti inapokuja kwenye namna ya kuongoza,so hapo lazima uwepo utofauti ambao unaweza kupelekea "kushutumiana"
 
vitofautiane kwa Sera but visiwe vinatukanana mf kusema chama kimefunga ndoa na kingine
 
Mimi huwa ninawashangaa nyie mnaotaka visituhumiane. Hivyo vyma ni tofauti, kwamba vinataka
kuchukua dola hata chama tawala nia yake ni kuendelea kuchukua dola katika kila uchaguzi, sasa
visishutumihane kwa misingi gani. hii hoja imejificha nyuma ya kichaka cha kutaka viungane hii, ni hii
hoja ni mfu sana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom