Mzalendo80
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 2,508
- 1,338
Hivi karibuni kumeibuka wimbi la viongozi wa serikalini kulia na kuonyesha machungu ya wananchi kana kwamba hawajui matatizo yetu, wanalia bila ya aibu au ninaweza kusema wanaigiza bila ya aibu na kuyashangaa maisha au matatizo yetu kuwa ni mageni kwao na kuwafanya waanze kulia mbele ya waandishi wa habari ili watokee kwenye ukurasa wa mbele kuwa alia na kuashangaa watanzania wamelala bila ya kunywa maji au umeme kutuonyesha kuwa wanatujali. Jana tulikuwa tunayaona maigizo ya yule Mama Jeuri wa Bunge Makimba wengine mnamwita Makinda kuwa aliona uchungu na kuanza kulia wakati Bungeni alikataa suala hilo lisungumziwe Bungeni sio la dharura. Sasa hawa viongozi wana uchungu na sisi au wanafanya maigizo ya kwenye Maisha yetu Naomba muongozo wa JF