Kwanini unibadilishie mfumo wangu wa maisha??!!

me nchojua wawili mnapoamua kuanzisha mahusiano amabayo ni focused,
basi lazima hua kuna "submission of self mandate" kwa mwenzako.yaani maamuzi yako unakua huyamiliki kwa asilimia 100.
inamaana kuana vitu ambavyo inakubidi uache kama ulikua unafanya au ufanye kama ulikua hufanyi,
ili kuweza kudumisha mapenzi,na hii hua paletu kunapokua na mapenzi ya kweli.
bila kufanya hivi penzi kudumu ni kazi ngumu.
so kumbadilisha mtu ni sawatu ila cha msingi ni nia inayotumia.

ni kweli tasia, maamuzi yako huwezi kuyamiliki 100% kuna vitu ambavyo lazima mjadili mfikie muafaka. Ina maana huwezi kujiamulia.
Ila suala la interests za mtu sio suala la mtu mwingine kulifanyia maamuzi.
Unaweza kujifunza kukikubali kile anachopenda mwenzio. Au waonaje?
 
mleta thread sijui ulikuwa umeandika huku una gadhabu?
Nafikiri ungepunguza ukali wa maneno ili kuleta uhuru kwa wachangiaji..lakini binafsi nadhani nimekuelewa ujumbe uliokuwa unataka kutufikishia.

Ukweli ni kwamba kweli mtu anaweza akawa amekupenda, na kwa kiasi kikubwa unategemea akuheshimu kama alivyokukuta.

Lakini kama unafikiri hauwezi kubadilika ni vyema ukamueleza yule anayekupenda kwamba wewe huwezi kubadilika na akuchukulie kama ulivyo, hilo litakuwa ni kama angalizo kwa mpendaji,ili ajue kama anasuka ama ananyoa.

Kwa upande mwingine kukataa kubadilisha lifestyle ni dalili ya ubinafsi..Kwenye mapenzi lazima ku-compromise.

mpendwa maneno gani yana ukali nikayaedit? Wala sina ghadhabu. Lisred lenyewe tu limekaa kighadhabu ghadhabu.
B2T: huyo binti ameshamwambia rafiki yangu kuwa hawezi kubadilika. Rafiki yangu ndio hajui kama aendelee nae tu hivyo hvyo au achape lapa.
 
Hayo angemwambia kabla hawajawa pamoja kama ni muhimu sana kwake.Angeambiwa kama inawezekana au la ili nae aamue kama anaweza kumvumilia mnywaji au la!Kutaka kumbadilisha mtu kwa lazima unakua humtendei haki...shawishi..shauri alafu mwache mtu aamue mwenyewe!

well said. Mpasome hapo juu.
 
Kwa Hiyo wewe Upo tayari kumpoteza mtu unayempenda kwa sbb hautaki kuacha tabia za kinyonge eg Pombe,Vimini,Clubbing,etc,I doubt ur love for him!!

Kwa sbb tu nimekukuta na tabia fulani hiyo sio sababu ya ww kutokubadilika,CHANGE! Angekuwa anakwambia uache kufanya ibada au usafi hapo ningekuelewa,Pombe Vimini na Disco ni vitu vya muda mfupi,angalia Maisha in the next 20 years,ukipiga darubini ya kipindi hicho bado unajiona upo kwenye min?

Besides,sio lazima uvae mini ndiyo uonekane mrembo,yapo mavazi ya staha na mwanamke anapendeza not necessarily Hijab!
Sidhani kama kuna mwanaume mwenye akili timamu anayetaka Mkewe awe anavaa nguo juu ya magoti,kama yupo hatakuwa mwanaume asiye na Fahari!!

The bottomline hz,kwenye uhusiano kila mtu hakubari kupukutisha mambo fulani ili timu iwe Imara!!

Kama ningekuwa mm ndiyo mwanaume wako,ningekwambia taratibu halafu nikupe muda ubadilike,nikiona haubadiliki,nakuuliza swali kibabe: CHAGUA KATI YA MIMI AU POMBE,UKICHAGUA POMBE NASEPA NA HAUTOSIKIA KUTOKA KWANGU KATIKA MAISHA HAYA NA HAKUNA SECOND CHANCE!!!

Nakubaliana na we 100%, mi sidhan kama MAMBO ya club,vimini,pombe kwa mwanamke ni jambo la kawaida kwa jamii ye2 hasa ya kitanzania, hebu angalien skendo za wasanii wa kike kama irene uwoya, ambavy alikuw nazo,ameolew halaf mambo ambayo alikuw anafany akayaendeleza! Hii haileti picha kabisa ktk mahusiano, HUYO mwanaume alikuvumilia hapo mwanzo na anapotaka ubadilike anakuepusha na mengi ambayo we hutayaona! Kwahyo msikiliz na ubadilike! Lakini yote tisa, kumi ni kwamb inawezekan Mwanamke anapesa, na elimu ambayo inampa kibur cha kutotaka kubadilika anaona hata kama huyu mwanaume atamwacha atapata tu mwingine! Kwahyo hana shida sitarehe kama kawa.. Usemi ni ule ule ''PATA PESA TUJUE TABIA YAKO''.. Na ki2 kingine kama hutak kuacha hiyo tabia ambao mi siipend kabisa, unaonaje utakapo pata watoto, na 2najua tabia ya mtoto inatoka kwa mzazi hasa Mama. Je huoni utawafundisha watoto wako tabia mbaya ambayo itapelekea kuwa na wenz wengi, mimba, na tabia chafu ambazo haziitajiki katika jamii.. Kuwa na akili ya kuangalia mbele si ulipo sa hvi.
 
BAK & WISELADY.
Mmeongea kitu kuombana au kuelekezana kwa utaratibu. Kweli ni vizuri hata kama unataka kumbadilisha mtu ufanye kumuomba.
Habari za kumwambia usipoacha kufanya hivyo mimi na wewe basi inakuwa kama unamlazimisha kinguvu.
Wakuu AFRODENZI, KING'AST, NEWDAWN na JUMALESO nimewasoma. Mmeongea vyema sijaona pa kuwachallenge.
 
To RG &TUMAINI:
hiyo pombe, club & min nimechukulia kama mifano tu. Halafu hobi ya mtu mi najua haibadiliki kutokana na umri bali mazingira tu.
Kwa mfano binafsi, mimi napenda kwenda ufukweni ila mazingira niliyopo hakuna bahari, ziwa wala mto. Mazingira hayaniruhusu kufanya nikipendacho.
Sasa, kama umemkuta na hobi zake tangu mwanzo na ukaridhika nazo, kwanini umbadilikie sahv? Kwanini usiruhusu mazingira ndio yambadilishe taratibu?
Kwa mfano baada ya hiyo miaka uliyosema 20 kama atakuwa kwenye ndoa na watoto kashazaa kuna possibility kubwa ya yeye kubadilika. Ila kwa mazingira ya sahv kama yanaruhusu kwanini asifanye kinachompendeza?
Ukiacha hiyo mifano, kuna wengine unakuta ni mtu wa kuinteract na watu, anapata mpenzi ila huyo mpenz unakuta jamaa akisalimiana tu na watu yeye ananuna.
Hapo napo utasemaje?
Kwanini utengeneze mgogoro sasa kwa jambo ambalo ulishalijua tangu awali?

kwa vi2 vizur mi sipingi kabisa, kama ni kuongea na wa2,kwenda beach halaf jamaa anakukataza hapo atakuw anakosea, lakin si kwa mambo mabaya na ya aibu HUSNINYO.. Kwa mfano mi napenda kuangalia Movies, mpira wa basket, lakin ikitokea mpenz wangu akasema niache, inabidi nimuulize kwanin anataka niache ,na kuna madhara gan kwenye hvyo vi2.. Na kama atatak niache 2 kisa amependa kwel cdhan kama kunaleta mantik.
 
ni kweli tasia, maamuzi yako huwezi kuyamiliki 100% kuna vitu ambavyo lazima mjadili mfikie muafaka. Ina maana huwezi kujiamulia.
Ila suala la interests za mtu sio suala la mtu mwingine kulifanyia maamuzi.
Unaweza kujifunza kukikubali kile anachopenda mwenzio. Au waonaje?

Kwa mfano ulitongozwa na huyo mwanaume club tena usiku wa manane, mkakubaliana, mkapendana na mkaanza kuwa wapenzi. Lakini kila weekend huyu mpenzio anapenda kwenda club (peke yake) hadi majogoo. Tabia hiyo haikupendezi, unapomuuliza anasema ulinikuta napenda kwenda club kwa hiyo naomba uniache nifanye ninachopenda. hapa sasa itakuwaje, utamwacha aendelee kufanya anachokipenda hadi yeye mwenyewe aamue kuacha?
 
BAK & WISELADY.
Mmeongea kitu kuombana au kuelekezana kwa utaratibu. Kweli ni vizuri hata kama unataka kumbadilisha mtu ufanye kumuomba.
Habari za kumwambia usipoacha kufanya hivyo mimi na wewe basi inakuwa kama unamlazimisha kinguvu.
Wakuu AFRODENZI, KING'AST, NEWDAWN na JUMALESO nimewasoma. Mmeongea vyema sijaona pa kuwachallenge.

The sentence I hate most in a marrital relationship.

Huwa najiuliza, kwani wewe mwanaume ndio unaamua ndoa iendelee au isiendelee, kwa kuwa tu mapendekezo yako hayajatimizwa? Tena wakati mwingine unakuta vitu vingine ni so trivial.

Je nami nikaanza kuitumia hiyo sentensi kwenye mambo ambayo siyapendi, hiyo nyumba inasonga kweli?

Nadhani hao wanaume wanaopenda kutumia hiyo sentensi wajiulize, je mimi mpenzi wangu anapenda kila kitu kutoka kwangu? Hebu tukae tuongee tuone nini tunaweza fanya kuyamanage mapungufu yetu bila kutishiana kuachana.
 
Kwa mfano ulitongozwa na huyo mwanaume club tena usiku wa manane, mkakubaliana, mkapendana na mkaanza kuwa wapenzi. Lakini kila weekend huyu mpenzio anapenda kwenda club (peke yake) hadi majogoo. Tabia hiyo haikupendezi, unapomuuliza anasema ulinikuta napenda kwenda club kwa hiyo naomba uniache nifanye ninachopenda. hapa sasa itakuwaje, utamwacha aendelee kufanya anachokipenda hadi yeye mwenyewe aamue kuacha?

kwa kesi hii kama anapenda kwenda club mwambie muende wote ila sio umkataze kabisa. Unaweza ukamkataza akaacha huku moyo wake unasononeka matokeo yake siku haupo anatoroka. Kwanini umjengee mazingira ya kujiiba iba? Au unakuta mtu anakuwa kwenye uhusiano ila hafurahii kutokana na kushindwa kufanya vitu ulivyomkataza.
Kwanin umnyime mtu uhuru wa nafsi?
 
The sentence I hate most in a marrital relationship.
Hebu tukae tuongee tuone nini tunaweza fanya kuyamanage mapungufu yetu bila kutishiana kuachana.

umeongea vyema. Kuna watu wanajua kutoa vitisho kwa wapenzi wao.
Sasa mtu mzima mwenzio unamtisha tisha kama mtoto sijui ili iweje.!
 
WATU WAZIMA HAWATISHIANI BALI WANAELEWESHANA JUU YA JAMBO LOLOTE LINALOONEKANA SI ZURI KWAO.
MPENZI/MKE/MUMEO KUKUSHAURI JAMBO UNALOFANYA KAMA ANAONA SIYO ZURI SI VIBAYA,
NA HAPO UNA HIARI YA KUKATAA AU KUKUBALI MOJAMOJA, AU KWA KUPEWA MUDA MFUPI WA KUJIREKEBISHA.
KUSIKILIZANA NA KUELEWESHANA NI SEHEMU YA MAPENZI.

HAUPASWI KUMWAMBIA MWENZI WAKO KWA SAUTI KALI NA USO MKAVU kwa mfano ETI USIPOACHA POMBE NAKUACHA.....
HATA KAMA HAUPENDI KIWANGO CHA POMBE ANACHOKUNYWA BASI KUNA JINSI YA KUMWAMBIA NA KUMPA MUDA
PIA WA KUBADILIKA,USITEGEMEE LEO LEO UMEMWOMBA JAMBO FULANI AACHE BASI LEOLEO AACHE KWELI mmh! huyo mtoto au mtuzima??

Binadamu tunaweza kubadilika kutoka wema kwa ubaya au ubaya kwa wema.
Lililo muhimu ni kuelimishana na subira, pamoja na matumizi sahihi ya njia ya kumbadilisha mtu.
 
kwa kesi hii kama anapenda kwenda club mwambie muende wote ila sio umkataze kabisa. Unaweza ukamkataza akaacha huku moyo wake unasononeka matokeo yake siku haupo anatoroka. Kwanini umjengee mazingira ya kujiiba iba? Au unakuta mtu anakuwa kwenye uhusiano ila hafurahii kutokana na kushindwa kufanya vitu ulivyomkataza.
Kwanin umnyime mtu uhuru wa nafsi?

Anakwambia hapendi mwende wote, yeye ana enjoy kwenda club peke yake. Ukizingatia kuwa hata siku mlipokutana alikuwa peke yake..
 
NN ngumu sana banaa hiyo mtu mzima kubadilishwa tabia labda aamue mwenyewe tu

Ewaaaa.....hapo bolded ndo umegonga Ikuli mazee. Na ninaamini mtu afanyaye mabadiliko mwenyewe hayo mabadiliko yatakuwa ya dhati. Lakini hii ya kusema sijui nimbadilishe fulani tabia yake....sijawahi mimi kuiona. Huenda wapo wanaobadilishwa tabia na wenzao lakini mimi sijawahi kuwaona.

Halafu mara nyingi wanawake ndo huwaga na mawazo ya kuwa wanaweza kuwabadili wenza wao.
 
Kweli kabisa nilishawahi kushuhudia mwanamke anamkataza mwanaume wake asiwe anafanya mambo aliyokuwa anafanya zamani ambayo kimsingi sio kwamba yangebadili mfumo wa maisha waliyonayo matokeo yake jamaa akawa worse zaidi kuliko ambavyo alivyokuwa mwanzoni
 
Halafu mara nyingi wanawake ndo huwaga na mawazo ya kuwa wanaweza kuwabadili wenza wao.[/QUOTE]

Hata wanaume pia huwa na mawazo hayo. mf anatongoza mwanamke ambae hajatulia kabisa lakini anajiambia mie huyu mwanamke nikifanikiwa kumpata, ntamtuliza tu.. sasa sijui kama huwa wanafanikiwa kuwatuliza!
 
Muanzisha thread hana hekima la sivyo iko chini ya kiwango cha kawaida.

Pole zako bibie asiyefunzwa na ***** atafunzwa na dunia. You will learn through you mistakes.

Mungu akutie nguvu, uone mbali!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom