Kwanini Unatakiwa Kusajili Dot Tz ?

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kwanini Unatakiwa Kusajili Dot Tz ?


Kuna watu wengi wamewahi kulalamika kuhusu anuani za barua zao pepe kuvamiwa na kubadilishwa baadhi ya vitu au kutumiwa kwa huduma zingine ambazo wao hawataki hizi nyingi unakuta zimesajiliwa kwenye mitandao ya yahoo au gmail na hotmail , kama watu hawa wangeamua kusajili Anuani pepe zao kwa njia sahihi ziwe zao moja kwa moja matatizo haya yasingewakuta .


Mimi nina mfano mmoja miaka michache iliyopita mmoja wa rafiki zangu alisajili .com yake na kampuni moja ya Marekani , kampuni ile ilishindwa kutoa huduma alizokuwa anataka mara kadhaa tovuti ilikuwa haifanyi kazi ikawa kupata huduma kwa wale watu ni shida sana hata kufanya nao mawasiliano ni gharama nyingi kipindi hicho .TZ ilikuwa ni bure heri angejua kwamba ukiwa na .TZ unajua pa kwenda kwa njia rahisi zaidi .


Watu wengi wanaposajili Domain zao hupenda kutumia .COM badala ya Tanzania ambayo ni .TZ ya Kenya ambayo ni .KE au Uganda ambayo ni .UG Hata hivyo Usajili ya .COM ndio ulio mrahisi zaidi na Gharama nafuu kuliko hizo zingine kwa sasa lakini kwa kipindi cha miaka 2 iliyopita ilikuwa ni bure kwa Tanzania Kampuni zilizokuwa zinatoa huduma hizo zilikuwa zinasajili .TZ bila gharama yoyote ulichotakiwa kulipia ni Nafasi kwenye mtandao ya kuhifadhi tovuti yako na vingine ulivyosajili kwa jina hilo .


Kwa sasa utaratibu umebadilika kuna pesa kidogo unatakiwa ulipie kwa Hapa Tanzania gharama za usajili wa .TZ ambapo unaweza kupata maelezo zaidi kwa kutembelea www.tznic.or.tz na kisha unalipia tena gharama za kuhifadhi mengine kwenye tovuti yako ila sio kwa kituo cha TZNIC ni kwa kampuni nyingine ambapo taarifa hizo utapeleka TZNIC washugulikie .


Pamoja na utaratibu huu wa gharama na nini kuna baadhi ya watu wamewahi kulalamika kwamba tznic wanachelewesha baadhi ya vitu na hawafanyi kazi kwa wakati kama wateja wengine wanavyotaka inawezekana kwa sababu ya kukosa taarifa sahihi au tatizo lingine la mawasiliano lakini wengine ni kutokujua ni nini haswa wanataka na hata kudanganywa na baadhi ya watu huko mitaani kuhusu usajili huu – usajili wa .TZ una maana sana kwako wewe mfanyabiashara na mtumiaji mwingine wa Mtandao .


Mfano Ukiwa unatafuta kitu Fulani kwenye mtandao kama Nyumba kutumia search engine Fulani , hiyo search engine itakupa majibu makubwa toka mitandao ya nchi uliyopo kwa muda huo una search ina maana kama kuna mtu alikuwa na tovuti yake ya masuala ya nyumba majibu yatakuletea anuani ya mtu huyo yenye .TZ kuliko zile zilizokuwa na .COM lakini pia inategemeana na majina aliyotumia kuita jina lake .


Unapokuwa na .TZ tovuti yako itajumuishwa kwenye huduma zingine nyingi zinazotolewa kwa jamii kwenye nchi hiyo bila shida ya kuhangaika kuliko ile ya .COM au .NET kama wewe ni muuza ndizi ni rahisi kuingiza tovuti yako kwa wauza ndizi wa nchi hiyo .


Kwa wale wanaofanya biashara kwa njia ya mtandao haswa ya kuuza na kununua unapokuwa na .TZ ni rahisi sana kwa watu wa nchi yako kuamini na kujenga kuaminiana kwenye masuala ya biashara kuliko wale wa kimataifa haswa masuala yanayohusu uhamishaji wa hela na vitu vingine vya thamani pia inakuwa rahisi kwa wewe mwenye tovuti kuweza kujua hata wateja wako walipo kwa urahisi zaidi .


Kama mteja anatafuta kitu Fulani anaweza kupelekwa kwenye tovuti yako na kupatiwa bei za bidhaa zako kwa bei za ndani ya nchi hiyo au kubadilisha kwa bei za nchi hiyo hapo hapo pamoja na kuwa na lugha ambayo yeye anaielewa kwa urahisi .


Na Mwisho hizi .COM ni nafuu sana kuna watu wananunua nyingi sana kwa ajili ya kuuzia wengine kwa bei za juu endapo jina lake linakuwa linalipa lakini unapokuwa na .TZ shida hii hautokuwa nayo kwa sababu zote zinasajiliwa toka sehemu moja tu na unaposajili unatoa taarifa zako zote .
Kabla sijafunga ukurasa tunatakiwa tujue kwamba kumekuwa na shida ya Miliki ya baadhi ya vitu kwenye mtandao haswa kwa nchi zinazoendelea Taasisi zinazosimamia mawasiliano ya nchi hizi inabidi kuwa makini na suala hili kwa sababu kuna baadhi ya majina na aina nyingine ya lugha zinaibiwa na kutumika kwenye sehemu zingine bila mataifa hayo kufaidika kwa njia moja au nyingine .


Kwa Kumalizia tu ni vizuri ukafikiria vya nyumbani kwanza kama vitu hivyo vinapatikana nyumbani badala ya kwenda kurukia nje Nunua vyetu imarisha mitandao yetu na huduma zingine za kiuchumi ndani ya nchi Itakuwa faida kwa vizazi vijavyo .


YONA F MARO
WWW.ICTPUB.BLOGSPOT.COM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom