Kwanini unabaki kuwa masikini mpaka leo?

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,699
9,455
Habari zenu wapendwa wangu

Leo nimekuja na SOMO JIPYA sana mwaweza kunishangaa mkadhani ladyf kadata la hasha sijawa hivyo bali
wakati mwingine lazima uwape somo wenzao sio kila wakati wewe unakuwa MFUNDAJI tu wa mambo ya MAHUSIANO wakati mwingine unawapa somo maridhawa jinsi ya kuondokana na dhana ya kuwa masikini miaka nenda rudi unakuwa vileville wala hubadiliki

Nimekuja na swali hapo juu lisemalo: Kwanini ubaki kuwa maskini mpaka leo huoni mbele wa la nyuma upoupo unaishi tu bora liende kwanini mpendwa rafiki yangu.? Basi tutaangalia sababu zifuatazo za wewe kuwa mskini mpaka leo.

1. Kushindwa kuamua haraka fursa zinapojitokeza kwao

2. Fursa kali Zikitokea wanaziona kama ni uongo na utapeli wa mjini.

3. Kung'ang'ania kuajiriwa hata kama ajira hiyo hailipi.

4. Kudhania unajua sana hivyo huoni jipya la kujifunza.

5. Kukosa ujasiri wa kuanza. Unapanga mwezi huu au mwaka huu ntafanya hili au lile. Lakini mwaka unaisha hujaanza

6. Kutokuwa na ndoto ya kiasi cha pesa unazotaka kwa siku, kwa wiki mwezi au mwaka. Unataka shs ngapi kwa siku? Wiki? Mwezi? Mwaka? Kwa nini unataka kiasi hicho? Matumizi yako ya lazima ni yapi? Ya starehe zako ni yapi?

7. Kununua vitu vya bei kubwa sana na visivyo na tija yoyote katika kuongeza kipato chako.

8. Kuwaza kwamba maendeleo yanapatikana uzeeni na siyo ujanani? Eti kumiliki mamilioni ya pesa mpaka uwe mzee kama Bakhresa na wengineo

9. Kufikiri eti huwezi kufanikiwa kuwa na fedha kuubwa mpaka uwe freemason au fisadi. Ujinga.

10. Kuwa na wategemezi kibao nyumbani kwako wakati kipato chenyewe kinatosha kula watu 2 tu kwa mwezi.

11. Kusubiri siku utakayopata pesa nyingi sana eti ndipo utafanya biashara hii au ile! Utasubiri sana mpaka utachoka.

12. Kutokuweka akiba yoyote kwa malengo ya maendeleo ya watoto na wajukuu zao.


13. Kufikiria kuwa kuna siku utapata msaada kutoka kwa wafadhili, serikali au wazungu au washikaji zako.

14. Kubadilisha mshahara wako au kipato chako kuwa mali ya ukoo mzima. Kila mtu kwenye ukoo wenu anakuomba pesa na wewe unampatia. Usimpe mtu samaki mfundishe kuvua samaki naye hatakuomba tena samaki. Usimpatie maziwa ndugu yako mfundishe kufuga ng'ombe wa maziwa.

Je wewe umeguswa na sababu ipi ktk hizo? na umepanga kufanya nini?

Zindukeni kutoka katika usingizi mzito wa kutegemea kuajiriwa hebu jiwekee malengo ya kujiajiri ndipo utakaopoona mlango wa mafanikio yako ukaribu

Anza sasa hujachelewa bestito kwani MAFANIKIO UNAYALETA WEWE HAKULETEI MWENZIO USIWE TEGEMEZI

Wasalaam

Ladyf (Mwallimu na mfundaji wa ukwelii)





Comments





 
Dah izi mada zinatia hasira sana. Nisipokuwa na hela mipango miiingi nikipata vihisenti mmipangi yote inayetuka
 
Dah izi mada zinatia hasira sana. Nisipokuwa na hela mipango miiingi nikipata vihisenti mmipangi yote inayetuka
usijisikie vibaya mkuu mawazo yako yaweza kuhamishia kwenye diary ili hiyo mipango yako usisahau jifunze kuweka kumbukumbu kwenye diary yako siku ukiwa na fedha utaweza kuchukua na kuanza kujiandaa kwa hiyo mipango uliyojiwekea
 
hasa hiyo namba 5...., unaweza kujikuta unajiwasha kibao mwenyewe
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom