Kwanini tunatimkia Loliondo?

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Picha hii inaelezea mojawapo tu ya sababu lukuki za kwa nini watu wanaamua kuacha matibabu na kuamua kukimbilia Loliondo kwa matumaini ya kuwa watapona na kuondokana na adha za magonjwa waliyonayo.

Nyinginezo ya sababu, wachilia hii ya dawa feki ambazo zimekuwa zikipigwa vita, ni pamoja na:-
"kadhia" na "usumbufu" wa mazingira ya hospitalini
Huduma zisizoridhisha mahospitalini
Huduma hafifu, duni au zilizokosekana kabisa mahospitalini
Kukata tamaa baada ya matibabu ya muda mrefu
Kutaka tiba ya haraka bila gharama kubwa (matibabu mkato)
Kutokuwa na elimu wala ufahamu wa tiba za mahospitalini
Jamii kukua katika mazingira ya kuamini 'uganga' zaidi
Kutaka kupata ahueni kwa gharama yoyote ile
na sababu kadha wa kadha unazoweza pia ukawa unazifahamu au umezisikia. Si vibaya ukiziorodhesha hapa pia, pengine wako wanaochukua 'notes' watasoma na kujua namna ya kurekebisha mfumo wa afya nchini na hivyo kurudisha imani ya Watanzania katika huduma wanazopewa na Wasomi/Wataalamu wetu.

1099576.jpg
 
Back
Top Bottom