Kwanini television ya taifa (tbc) haiendeshi vipindi juu ya muswada wa katiba mpya?

JOB SEEKER

Senior Member
Aug 1, 2011
145
33
Wana JF,Nimekuwa nikifuatilia vipindi mbalimbali juu ya mswada wa katiba mpya katika television vinavyowakutanisha makundi mbalimbali ya jamii kama vijana,wazee,wanawake ,watoto wenye umri na taaluma tofauti wenye kutoa michango iliyobeba mawazo na mitazamo tofauti yenye nia na lengo la kujenga mswada wa katiba mpya.Lakini sijawahi kuona vipindi kama hivyo juu ya mswada wa katiba mpya vikionyeshwa na television ya taifa (TBC), ni kwanini ? na kwa mamlaka ya nani wana fanya hivyo? Hichi ndicho chombo kinacho wafikia watanzania wengi kwa ujumla na kwa wakati mwafaka, Je ! tujiulize swala la mswada wa katiba mpya halina maslahi kwao kama vipindi vya miaka 50 ya uhuru!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kwanini wenzao kama ITV,STAR TV, wanaweza kukidhi maslahi ya watanzania lakini wao washindwe, Je !! maslahi ya taifa yana maslahi gani na maana ipi kwao??? Job Seeker.
 
mie nilishaacha hata kuitazama hiyo TV so ndo nashangaa, kumbe hata mambo muhimu kama hayo wanayapuuza...? hii ni hatari sanaa mbona safari za kitalii zisizo za msingi zinazofanywa na ****** huwa wana zirusha, tena nasikia wapo tayari hata kukatisha taarifa ya habari ili kumrusha Huyu jamaa, ******, a.k.a mzee wa kuuza sura na misele... IMECHAKACHULIWA tangu alipoondoka Mhando Tido, TBCCM imekuwa ni TV dada na Uhuru magazine
 
Hadhi haina siku hizi imekuwa KASUKU tuu. (Miaka 50 ya uhuru wa tanzania bara)
 
Unataka mkurugenzi mkuu awe tidolized eeeeh! anaupenda ugali wake bwana
 
Wana JF,Nimekuwa nikifuatilia vipindi mbalimbali juu ya mswada wa katiba mpya katika television vinavyowakutanisha makundi mbalimbali ya jamii kama vijana,wazee,wanawake ,watoto wenye umri na taaluma tofauti wenye kutoa michango iliyobeba mawazo na mitazamo tofauti yenye nia na lengo la kujenga mswada wa katiba mpya.Lakini sijawahi kuona vipindi kama hivyo juu ya mswada wa katiba mpya vikionyeshwa na television ya taifa (TBC), ni kwanini ? na kwa mamlaka ya nani wana fanya hivyo? Hichi ndicho chombo kinacho wafikia watanzania wengi kwa ujumla na kwa wakati mwafaka, Je ! tujiulize swala la mswada wa katiba mpya halina maslahi kwao kama vipindi vya miaka 50 ya uhuru!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kwanini wenzao kama ITV,STAR TV, wanaweza kukidhi maslahi ya watanzania lakini wao washindwe, Je !! maslahi ya taifa yana maslahi gani na maana ipi kwao??? Job Seeker.

Ni kwa sababu TBC ni chombo cha propaganda kinachotaka kuwalisha wananchi habari za uelekeo flani kadiri wao watakavyoona inafaa. Vipindi vya Mijadala huamsha na kuchochea fikra kitu ambacho TBC hawako tayari kukifanya.
 
Back
Top Bottom