Kwanini Tanzania wanauza kwa 'dollar' sio 'shillings'?

Tunatumia dola za kimarekani kwa vile hatuna fedha zetu wenyewe, au tumeshindwa kutunza fedha zetu.

Ni kama ambavyo Zimbabwe walivyoshindwa kutunza fedha zao na wakaamua kutumia dola za kimarekani hata katika kulipa mishahara ya wafanyakazi wa serikali. Huu ni ujinga kweli kweli kwa taifa lililo huru kwa miaka 50!

Mwaka 1999, China ilifikisha miaka 50 ya uhuru wake, na mwaka 1997 India nayo ilifikisha miaka 50 ya uhuru wake. Je Tanzania ya leo inalingana na China ya mwaka 1999 au India ya mwaka 1997?
 
Tumepiga kelele humu sana kuhusu hili,pale mlimani city kuna mpaka maduka ya simu,tv and music system wanatoza kwa dola! Nani awajibike,BOT,MOEF?
 
nafikiri waziri wetu kivuli wa fedha mh Zitto Kabwe anaweza kulisemea hili serikali itoe tamko rasmi.matumizi ya dola yanatuzidishia machungu wakuu!
 
Bunge linafanya nini kwa swala hili na wizara ya fedha inasemaje? Na wanamchi wana mpango gani na swala hili?
<br />
<br />
Huo ni mchongo wa watu mkuu! We unafikiri Beno Ndulu halioni hilo? We unadhani JK halioni hilo? TISS wana department ya economic intelligence, unadhani hawalioni hilo??? We cheki utitiri wa maduka ya forex ndo uelewe and most of them owned by asians! Hapa mpaka yafanyike mapinduzi ya kweli ndo nchi itabadilika!
 
uchumi umepewa uhuru wa hatari sana kwa nchi kama hii ambayo bado haijawa stable, tunaenda tuuuuuu bila breki na kutafakuri!
 
Bunge linafanya nini kwa swala hili na wizara ya fedha inasemaje? Na wanamchi wana mpango gani na swala hili?
Sio Tanzania tu, hata Kenya hususani Nairobi wanapenda kutumia dollar. Nenda kwenye hotel kubwa na maduka makubwa utaona dola pia zikitumika. Ila Tanzania tumezidi. Labda kwa sababu pesa zetu hazipo stable. Basi tuache shillingi uwe mwendo wa dollar tu.
 
Hili suala nakumbuka serikali iliingilia kati wakati Mama Meghji akiwa waziri wa fedha, lakini cha kuchekesha na kwa sababu maagizo ya serikali siku zote ni sanaa hakuna kilichoendelea in fact serikali yetu siku zote " They never do what they say and never say what they do"

Mifano.

1. Sheria mpya ya kazi inakataza ubaguzi wa aina yeyote ile katika tangazo la kzi, lakini unakuta matangazo ya serikali hiyo hiyo kwa kazi za serikali hiyo hiyo ndani ya magazeti ya serikali wanaweka say umri - usizidi miaka 35.

2. TRA ambayo ni taasisi ya serikali inachaji import duties zote kwa dola, pamoja na kwamba unalipia Tshs, wao utakuta wanapigia hesabu bei ya dola ya siku hiyo.

3. Kukodi ndege za serikali malipo ni kwa dola!!!!!!!!!

Kusema kwamba kufanya hivyo ni kucope na economic terms nadhani ni kitu kinachohitaji kuelemishana otherwise true independence ni pamoja na kumiliki your own currency!!!!! Kinachoendelea bongo is just greed na as usual " no utekelezaji wa regulations"
 
wengine wanasema ni soko huria.........kumbe ni holela........kutumia dola nayo ni sababu inayoifanya thamani ya shilingi kushuka.....

Nakubaliana kabisa nawe, uko sahihi. Moja ya sababu kuu ya kushuka kwa shilingi yetu kila mara ni kuruhusu matumizi ya dola. Hakuna nchi duniani ambayo inataka kuimarisha thamani ya fedha yake, inayoweza kuruhusu matumizi ya fedha za kigeni. Inabidi manunuzi yote kila sehemu yafanywe kwa shs. ya tz, hapo tutaweza kuipandisha thamani hela yetu, pili kuongeza uaalishaji na mauzo katika soko la nje na ndani. Sasa hawa mawaziri wetu na wachumi wetu, wanayajua haya saaaaaaaaaaana, ila wanachozingatia ni uchumi matumbo yao!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa kweli hata mie nashindwa kuelewa jinsi ambavyo hata ada za shule zinadaiwa kwa dola! Kweli hii ndio maana ya soko huria jamani?
 
Tanzania tuna pesa moja tu nayo ni shillingi, lini imeruhusiwa kutumia dollar

Kwa mtu yeyote anayefahamu maana ya thamani ya pesa au thamani ya jasho lake, kutumia hard currency ni bora zaidi kuliko kutumia shilingi. Sababu ni kuwa thamani ya shilingi inaendelea kuporomoka
 
Tatizo la Watanzania wakiona Kipara cha Mkulo wanadhani ni Kuna Kitu Mle ndani!! Kumbe full Masaburi Thinking!!!
 
Back
Top Bottom