Kwanini spika anazima hoja ya kujadili mgogoro wa Madaktari?

kinachonitatiza ni kimoja tu!kwa nini serikali haifanyi maamuzi?kama kuwahukumu madaktari kifo basi ifanye hivyo sasa au kama ni kutekeleza mahitaji yao na iwe hivyo sasa na sio na kuendelea na danadana wakati watu wanateseka.

Wahukumiwe mara ngapi, au hujamsikia Pinda?
 
labda nikuulize wewe Black Rose kama mwanamke

wakati anateuliwa u spika wengi tuliona hafai na ni makosa kumzuia Sitta kugombea

lakini wanawake weengi mliona 'anafaa' ni sahihi kuteuliwa kuwa spika.....

je wewe hukuliona hilo toka mwanzo?

Sasa wewe Boss, unataka kusema watu wangepinga na kusema hafai kwa vile tu ni wanawake?
Watu wangesema hafai,kama angekuwa hakuwahi kushika wadhifa wowote mkubwa. Huyu amekuwa waziri kwa vipindi virefu toka enzi za Nyerere hadi Mkapa,kisha akawa naibu spika.
 
Kumbuka kuwa Tanzania inaendeshwa kisheria na wabunge ndio watunga sheria. Sheria haziruhusu daktari kugoma, Daktari anaegoma ni kama mwanajeshi anaesaliti wenzake (traitor), hukumu yake ni kifo tu.
hicho ndicho walichokuwa wanawaza serikali ya ccm kwa miaka mingi huku wenyewe wakijilimbikizia posho kwa kushinda na kutoa udenda tu bungeni...!
 
Ishu ya madokta ina usiri gani?
Mh Erasto ZAMBI akataka swala hili nyeti lijadiliwe.Spika kakataa na kawa mkali kama Mbogo

The true colour ya huyu mama ndiyo hiyo
aliyoonyesha jana! Binafsi sikuona haja ya kuzuia hoja kuzungumzia mgomo wa madaktari wetu na kutoa solution kupitia chombo muhimu kama Bunge!
 
Back
Top Bottom