FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,392
- 4,468
Afrika kuwa moja hata Nyerere alishasema haiwezekani sababu ya tofauti nyingi Nyerere alitoa hoja kuwa afrika inaweza kuungana kwa makundi yanayofanana mfano Tanzania Kenya na Uganda zikawa nchi moja, Malawi, Zambia na Zimbabwe zikawa nchi moja, Congo Kinshasa, Congo Brazaville na Gabon zikawa nchi moja, Ethiopia, Somalia, Djibout na Eriteria zikawa nchi moja, Misri, Algeria, Tunisia, Libya na Morocco zikawa nchi moja. South Africa, Lethoto, Swaziland na Namibia zikawa nchi moja. Orodha ni ndefu kiini cha kusema haya Nyerere alinena kuwa kuna tofauti kubwa tano ya Kwanza weupe wa kaskazini yaani waarabu dhidi ya weusi wa kusini weupe wale watataka wao ndio wawe watawala, sababu ya pili kuna nchi za kuzungumza kiingereza na nchi za kuzungumza kifaransa kila kundi litataka kushika madaraka, sababu ya tatu kuna wa kaskazini wengi ni waislamu na wa kusini wengi ni wakristo, sababu ya nne wakati huo kulikuwa na nchi za kibepari na kijamaa na sababu ya tano kulikuwa na nchi zinazotawaliwa kijeshi na zile zinatawaliwa na serikali za kiraia hizi sababu mbili kwa sasa si tatizo ila zile tatu za mwanzo bado zinasimama na ni kikwazo kikubwa tunachoweza kufanya ni kuungana kwa makundi na kuwa na nchi saba au nane Afrika zenye sauti badala ya 51 za sasa
Hata ukifanya utafiti, wanainchi wa Morocco, Libya, Tunisia, Algeria..hawako proud sana kujiita waafrica (labda kidoogo Misri)