Kwanini sisi Waafrika ni Masikini?

MIUNDOMBINU

JF-Expert Member
Apr 14, 2010
465
96
Ndugu zangu,

Kwanza napenda kumushukuru Mungu wetu anayetuwezesha kuwa hai mimi na wewe. Nimekutana na Hoja binafsi katika Gazeti la Mwananchi la leo 01.08.2010.

Mwandishi wa makala hii ni ndugu SAMMY MAKILLA. Labda ni nukuu baadhi ya maneno yaliyopo katika hoja hiyo binafsi;

"MTANZANIA mmoja aliyewahi kwenda ulaya alinifanya niamini kwamba kuna tofauti kubwa kati ya binadamu wa sasa na wale wa zamani.

Yeye aliniambia kwamba, jambo lililomshangaza huko ni kukuta madaraja makubwa na mzuri, makanisa makubwa, majumba mazuri ya kifalme na kitajiri na majengo mengine yaliyojengwa miaka miatano au zaidi iliyopita. Majumba hayo yapo kuanzia Misri, Italia, Uingereza, Uchina, nk.

Kilichomshangaza nikuwa wakati huo hakukuwa na vifaa vya kisasa vya ujenzi kama ilivyo leo, akawa anajiuliza kwanini watu hao enzi hizo za Tekenelojia duni waliwezaje kutengeneza madaraja mazuri, majumba makubwa na Watanzania wa leo wanashindwa?

Je ni kitu gani walichokuwa nacho hao binadamu wa kale kiasi cha kufanya mambo makubwa lakini sisi tunashindwa?" Mwisho wa kunukuu.

Ndugu zangu, mimi pia nimeguswa sana na hoja hii ndiyo maana nikaamua kuileta hapa JF ili iweze kujadiliwa kwa mapana zaidi, kwani hapa JF ni kisima cha maarifa.

Asanteni.
 
Jibu unalo katika sentensi yako ya kwanza kabisa.

Mungu.

Kuamini mungu ndiko kunatufanya tuwe masikini. Wakati wenzetu wamemtumia mungu kwa sababu zao za kisiasa na ili kutajirika, sisi tunaamini kweli kweli.

Of course ukiamini mungu unaamini katika msaada na kuomba, ukiamini katika msaada na kuomba huwezi kutajirika.
 
Jibu unalo katika sentensi yako ya kwanza kabisa.

Mungu.

Kuamini [M]mungu ndiko kunatufanya tuwe masikini. Wakati wenzetu wamemtumia mungu kwa sababu zao za kisiasa na ili kutajirika, sisi tunaamini kweli kweli.

Of course ukiamini mungu unaamini katika msaada na kuomba, ukiamini katika msaada na kuomba huwezi kutajirika.

WAAAT???????????
rubbish!!!! Nyie ndo watu mnaoturudisha nyuma kimaendeleo!!
 
we are selfish na uvivu

Hapo umesema

Nikiongeza , kwa ujumla muafrika ;
> Hafanyi kitu cha maslahi ya jamii
> Hana ujasiri wa kusafiri akavumbua vitu
> Anaridhika na maisha yake hata yakiwa duni vipi.
> Hana mchango wowote katika sayansi na maendeleo ya binaadamu.
> Fikra zake zina upeo
> Hana ushujaa wa kuondoa viongozi wasioleta maendeleo

Lakini kuna matuamaini hayo hapo juu yanabadilika pole pole ambapo baadhi ya mataifa wameanza mamia au maelfu ya miaka nyuma na sisi tunafaidika kwa kunakili bidii zao zilizowachukua miaka kufanisi.
 
Hahahahahaaa...this topic is right up my alley way....don't get me started y'all....don't get me started
 
WAAAT???????????
rubbish!!!! Nyie ndo watu mnaoturudisha nyuma kimaendeleo!!

Think about it, wenzetu zikitokea ajali wanachunguza zimeanzia wapi na kuweka jinsi za kuzizuia.Sisi rais anasema "kazi ya mungu".

Ukiangalia maendeleo ya Ulaya kisayansi yalianza sna baada ya the 1400's, baada ya the bubonic plague / black death ambapo karibu 1/3 ya population ya europe ilikufa, watu wakakaa na kufikiri mungu gani huyu anaua watu kama hivi, wakaona hamna mungu, wakaanza ku concentrate kwenye uchumi na sayansi, wakaanza kusafiri kwenda mabara mengine. Sie tunaomba mizimu na mungu mpaka kesho.

Ukiamini mungu utaogopa authority, utakuwa mtu wa kukubali maisha yako kwamba "ni mipango ya mungu". Usipoamini katika mungu utajua kwamba una mamlaka ya kubadilisha maisha yako mwenywe, wala mungu hawezi kukusaidia, utafanya juhudi kujisaidia mwenywe.

Unavyozidi kuamini mungu, ndivyo unavyozidi ku suspend reson, unavyozidi ku suspend reason ndivyo unavyozidi kualika umasikini.
 
Toka miaka mingi iliyopita bado waafrika wengi ni masikini na maendeleo yetu yamekuwa ya kusuasua na hii inasababisha tuwe nyuma kwa vitu vingi ukilinganisha na wenzetu wa europe, america na asia!

Labda tunaweza kukasema ni effect za ukoloni zilichangia, hata hivyo mbona zipo nchi nyingi zitizotawaliwa kama baadhi ya nchi za asia na zimeweza piga hatua kubwa kimaendeleo?

Au tatizo ni swala la vita? Ila mbona Israeli ina maadui chungu nzima na bado inafanya vizuri? Au tatizo hasa ni nini? Viongozi? Mbona walikuwepo akina Nyerere, Kwame Nkurumah na wengine ila bado tupo nyuma?

Hata ukijaribu kuchunguza maisha ya ndugu zetu African-American pale kwa Obama utagundua kuwa wengi maisha yao ni ya kawaida tofauti na wenzao ngozi nyeupe?

Au fanya utafiti wako hata hapa nyumbani Tz utagundua kuwa wengi wenye asili ya Asia au Ulaya ndio vibopa,,, tatizo ni nini hasa?
Au hili swala linahusiana na GENETICS? kuwa ndio namna uwezo wetu wa kupenda mabadiliko umekwama?

Ni mawazo tu majameni,, ila ya kwenu yatanisaidia kujua!

Asanteni!
 
Kwanza kabisa si sahihi kusema waafrika ni masikini. There are divides and these divides are extreme in contrast. They are like our "class" systems in the fact that there are rich and poor. The only difference is that their rich are VERY rich and their poor are VERY VERY poor.

The extremely wealthy part of Africa has a good diamond and oil trade going on. The rich part of Africa (and the governing bodies that rule) keep the money they have from this trade, all to their selves. They do not care for the poor part of their own country and choose to seclude it and abuse it to help their trade prosper. Yes, the "west" could easily stop doing trade with them, but why should they? It's not the "wests" fault that Africa's leaders are a bunch of selfish horrible people who don't care about their own people.

The poor majority of Africans suffers because their government leaders are horrible people who care for nothing but their own wealth. Just as most governments are the same I might add, except, African governments are very extreme and harsh in their judgement.
 
Ni, kweli unachokiongea! Kwanza kabisa mwafrika bado hajajitambua kua yeye anauwezo wa kufanya mambo makubwa kama wenzetu,pia sisi waafrika tuna kitu kimoja kiitwacho"most people of africa they have dreams,but they have not planning to do,so utagundua kwamba sisi hatuna unit kama wenzetu pia.

hatuna umoja wa kufanya mambo makubwa,pia bado tunasumbuliwa na neo-colonialism kwa mfano utakuta hawa viongozi wetu wa africa bado ni vibaraka wa viongozi wa mataifa makubwa,utawala wao sio wa kujiamini.Bali wanatawala kwa kufata america inasema nini? sasa labda pengine kwa kuwa siwezi kulaumu kwa MWENYEZI MUNGU KWAMBA rangi yetu kuwa black hatuisamini,mfano wewe kiongozi wa africa unapewa ziara kwenda nje,ukifika kule basi unaingizwa mkenge kwa mikataba fake! Ndani ya mazungumzo kuna mrembo kwa pembeni,kwa kuwa hajawahi kuona nyama ya mzungu papo kwa papo unasaini mikataba ya unyonyaji na ukandamizwaji jamii, pia utakuta viongozi wetu wanapora rasrimari zote wanapereka nje sisi huku tunabaki hewa.

Utakuta wawekezaji wanatoka nje wao watawekeza katika ardhi nzuri wewe mwafrika utamiriki ardhi mbaya! kwa hiyo tujue kwamba"AFRICA IS STILL DARKNESS CONTINENT, Bado tunakazi kubwa viongozi wetu kugubikwa na uroho wa madaraka,kijipendekeza kwa wazungu pengine hayo ndio yatakuwa suluhisho kama tukiachana kwayo.
 
Hivi mnataka kuzungumzia UMASKINI upi hapa?

Umaskini wa AKILI au wa MALI? Kama ni wa akili ni kwa Waafrika wepi, na kama ni wa MALI ni kwa Waafrika wepi!

  • Maana kama SOUTH AFRICA ni Waafrika wenzentu na ni nchi inayoongoza kwa UCHUMI katika Bara Afrika vipi useme Waafrika ni maskini?
  • BOTSWANA nayo ina UCHUMI wa kupigiwa mfano kwa Bara Afrika. Kwa maana ya kuwa hata Wabotswana hali zao kiuchumi ziko poa.Kwa hiyo siyo swala la Uafrika hapa.
  • Tukirudi Bongo hapa tuna akina Reginaldi Mengi,kina Mkono n.k ambao wako vizuri kiuchumi kwa lugha rahisi ni mamilionea. Vipi useme Waafrika maskini???
  • Tanzania tuna rasilimali za mabilioni ya pesa. Tunachokosa ni Uongozi bora tu na hii ni kwasababu viongozi wetu wametanguliza UBINAFSI wa kushibisha matumbo yao.

Kwa upande wa akili Waafrika tuko vizuri mbona. Mtu unakaa darasani na mzungu.mhindi,mrusi au Mwingereza mnachuana na hata unawa piku darasani. Kwa hiyo kiakili napo nakataa kuwa Waafrika si maskini wa akili.

Nakataa kuwa WAAFRIKA TU MASKINI. No!
 
makoye2009

Hujamuelewa mtoa hoja. hela za akina mkono ni mavi tu, tunazungumzia majority. ukitaka kujua nini maana ya umaskini tunaozungumzia kawaulize Tanesco/Dawasco.
 
Last edited by a moderator:
Hii ni hoja nzuri ila mie nadhani chanzo ni sisi wenyewe kwanza wazazi hawamuandai mtoto vitisho na kukatishana tamaa vimekuwa mbele oh! maisha magumu utajiri mpaka uwe mchawi oh! watakuroga nani atathubutu? kulingana na mawazo hayo yanapelekea upoor
 
Hakuna jibu sahihi la umasikini ,mungu alikuwepo na atakuwepo na yupo pia ujumbe mungu wa hapa duniani ni baba yako na mamayako ,ukiwakutamajiri nawe unakuwa tajiri ,ukiwakuta masikini nawe unakulia kwenye umasikini
 
Ukiulizwa swali hili Mara nyingi kwa kulijibu kwa swali hili utapata shida sana. Kwa sababu huwezi kuja na jibu moja ndo ukasema sababu hii ndiyo imesababisha Waafrika wengi kuwa maskini. Kuanzia miaka ya 1960 na kuendelea jibu kwa wengi hasa magwiji wa Historia na Wanaharakati maarufu wa kiafrika na waliokuwa nje ya Afrika walikuwa wanakuja na jibu MOJA TU, nalo ni ukoloni. Ukoloni kwa sababu ulinyonya rasilimali nyingi sana za kiafrika. Pia walifanikiwa kuwahadaa Waafrika na elimu isiyoendana na mazingira yao wakaja kuwa watumwa kifkira. Kuwa watumwa kifkira likatokea tatizo sugu sana ambao nalo ni mwendelezo mwa sababu ya kwanza ya umaskini wa Waafrika ambalo ni UKOLONI MAMBO LEO.

Nakubaliana na sababu ya ukoloni ambao umezaa ukoloni mamboleo kuwa ni msingi wa umaskini mkubwa wa bara la Afrika. Mwalimu Nyerere kabla hajaondoka duniani alisema kuwa,nchi za afrika zilipopata uhuru viongozi wake walikuwa na maono na mikakati madhubuti kabisa ya kupambana na ukoloni mamboleo pamoja na umaskini. Kizazi kilichofuata kilikuja kulegalega na kwa sababu Kilianza kuzidiwa na ukoloni mambo leo, kwa kifupi Nyerere alisema kilianza kukosa dira kabisa. Na akawa na matumaini kwa kusema anaona Afrika mpya, Afrika ambavyo watu wengi watakuwa wanaishi maisha mazuri, Afrika ambayo itaweza kutoa mnyororo wa ukoloni mambo leo. Lakini Mwalimu Hatuko naye kwa sasa, bila shaka angekuwepo angetupa jibu zuri kwa hali iliyopo Afrika.

Tatizo kubwa kwa sasa katika nchi za kiafrika ni Uzalendo. Mfano, katika halimashauri zetu hapa Tanzania au taasisi nyingi tu,utakuta mtu akiajiliwa anakuwa na maono mazuri ya kimaendeleo. Tatizo akifika ofisini anakutana na mifumo miwili. Mfumo halali ndani ya sehemu alipo na mfumo ulioota mizizi na umekuwa kama ndo mfumo halali kabisa,nao ni mfumo wa kutotoa huduma vizuri kwa wateja, kutofanya kazi ipasavyo mpaka mtu a pâté chochote ndiyo afanye au ahudumie watu wake. Na mbaya zaidi viongozi wanaotakiwa kukemea ndiyo wanaofanya hayo. Utakuta maono yako yako kinyume kabisa na watu wengi,hapo ndipo wazalendo wachache wanapozidiwa na majambazi wakubwa wa rasilimali za afrika.

Uzalendo ninavyouchukulia binafsi,kama wewe ni mfanyakazi wa nyumbani na unalipwa fanya kazi ipasanyo,kama wewe ni mkulima fanya kazi, kama wewe ni Mwalimu fanya kazi ipasavyo,kama wewe daktari timiza wajibu wako. Kama wewe raisi wa nchi waonee huruma wananchi wako timiza wajibu wako ipasavyo.

Tatizo kubwa la Afrika ni Waafrika wengi wamepoteza uzalendo kabisa. Kwa niñi limetokea hili?. Tufanye nini kuweza kurudisha uzalendo ili angalau turudi kwenye msingi?

Au tumekuwa tukichagua viongozi hawa hapa wafuatao kama Plato Myunani wa kale alivyonena. Yeye alisema kuwa viongozi wanaofaa kutuongoza ni;

a) Wanafalsafa
-Hawa wana sifa mbili muhimu, sifa ya kwanza; Wanaweza kuongoza, ya pili hawapendi kuongoza. Hawa Plato alisema ni vizuri waongoze maana hata kung'ang'ania uongozi hawataki, maana miaka yao ikiisha waliochaguliwa watafurahi maana watarudi kwenye kazi zao za falsafa. Hawa Nyerere kwenye kitabu chake cha Viongozi wetu na Hatma ya Tanzania aliyesema a nadhani kwa Tanzania hawa hawapo kwa sasa.

b) Wanaopenda kuongoza na hawana uwezo wa kuongoza.
-Hawa watu nao Wana sifa zao; kwanza, wanapenda kuingia kwenye madaraka kwa njia zozote chafu maana njia halali ni vigumu kuchaguliwa na watu. Wanaingia kwa kutumia rushwa, vitisho, kuua,udanganyifu mwingi. Hawa watu wakishaingia madarani maana hawajui Hatma Yao Mara nyingi utawala wao wanaulinda wa njia yoyote ile chafu. Wanna fanya hivi maana hata wakitoka huwa hawajui watafanya kazi gani?.Wakitoka nani atawatetea kwa dhuruma walizofanya?. Hawa ndo wako wengi katika bara la Afrika. Na wameota mizizi Afrika maana wamezagaa kila koan ya Afrika na jeshi Lao ni kubwa mno. Na hawa viongozi wengi tulio nao kuanzia ngazi za chini mpaka juu. Ukiwasikiliza matamshinyao utafhani Wanauchungu na bara la Afrika. Na hawa ndo wanachangia bara la Afrika kuwa maskini.

c) Viongozi wanaojua uongozi ni WAJIBU.
-Hawa ukiwapa uongozi wanajua kabisa uongozi ni wajibu na wajibu ni kufanya kazi tu. Hawa binafsi nawachukulia kuwa wanaamini katika kufanya kazi ili mtu upate haki yako. Hawa ukiwachagua nao wanasifa zao, sifa Yao kubwa ni kwa sababu anajua uongozi ni wajibu, atafanya kazi sana ili aweze kutimiza wajibu wake. Na asipouyimiza huwa anaumia sana moyoni na Mara nyingi atawaambieni kwa niñi ameshindwa kutimiza wajibu aliokuwa amejiwekea. Hawa tunao wachache sana Afrika na Mara nyingi wanazidiwa na kundi la pili maana kundi la pili Lina jeshi kuwa sana. Na hili kundi huwa haling'ang'anii katika madaraka kama kundi la pili, maana wanaingia kwenye uongozi kwa njia halali na wanapenda kutoka kwa njia hizohizo. Hili ndo kundi ambalo linatakiwa kwa nchi zetu za Afrika ili liweze kupunguzankwa kasi kuwa umaskini.

HITIMISHO
-Wanajamii forum wenzangu hayo ndo mawazo yangu ya msingi kwa niñi bara la Afrika ni maskini. Kama umesoma vizuri, mawazo yangu yamejikita katika nyanja mbili tu; kwanza bara la Afrika ni maskini kwa sababu za kihistoria, pili, za kiuongozi na nikatoa mifano ya ni aina gani ya viongozi na sifa zao kuu. Haya ndo nawazo yangu huru. Wewe una mawazo gani kuhusu koi haw cha habari hapo juu? Naomba tuwe wadadisi sana kama tunataka kujifunza vizuri na tutumie jukwaa hili kwa kujigunza,kuelimishana mambo ya msingi ya bara letu na Taifa letu la Tanzania. Kwa maoni mazuri kuhusu kwa niñi bara letu la Afrika ni maskini na tufanye niñi kama kizazi cha leo kuweza kutatua jambo hili; changia vizuri hapa chini ili tujifunze vizuri au kama waweza nishauri vizuri kuhusu hili waweza niandikia 8319jilala@gmail.com. Karibuni kwa michango yenu.[MENTION][/MENTION]
 
Ninachosikitika zaidi maliasili zetu zinazosimamiwa na hao viongozi unaowataja zimeshindwa kutupatia elimu bora,technology,huduma bora za jamii ,Ajira na Amani
Hii ni ishara ya kutawaliwa na kukosa uzalendo
 
Back
Top Bottom