Kwanini sisi tukuite wewe mtanzania?

firstcollina

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
349
21
Mtu usiye hata na chembe ya uzalendo katika kope za macho yako. Mwenye kuthubutu hata kuidanganya hadhira na jamii tena kwa HONGO ili apate kibali na haki ya kuwaibia wanyonge. Mpumbavu usiyejali hata utu na asili ya utu wa baba na babu zako. Muongo, Mnafiki, Mwoga hata kwa wageni wasio na hadhi ya daraja ulilonalo, Why should we call u our fellow Mtazania?

Nijuavyo mimi thamani ya mtu hutokana na matendo atendayo kwa haki ya walio wengi, sasa iko wapi thamani yako wewe unayejali tumbo lako na la watoto wako pekee?

Inauma sana kuwaona hawa walio na madaraka huku hawana hata chembe ya uzalendo na Taifa lao wala juu ya rasilimali za taifa. Walio tayari kuwapa wageni thamani ya utaifa kwa kupokea Senti a ubuyu.

Go to hell.....!
Huu si upuuzi? Mtu unashabikia tena unakuwa tayari hata kuuza nchi nzima eti kwa kisingizio cha Uwekezaji, ni uwekezaji wa namna gani huu usiyo na mipaka, wala sheria ya ku-counter check the viability and monitoring of the agreements. Uwekezaji usio kupa fursa ya kuuliza muendendo chanya ama Hasi ni uwekezaji huu au ukoloni? Uwekezaji usiokupa fura ya maamuzi wewe mwenye mali bali yule mgeni....! Eheeeeh!! Who are you now, I will be very very wrong to call you Mtanzania.

Help me to stop these.......!!!! Fu*.../$#K!!
 
There is such a thing as flaming.UTanzania ni haki ya uraia, regardless ya tabia ya mtu. Hata kama mtu fisadi wa kutupwa lakini kama kazaliwa Tanzania na/ au ana uraia basi ni Mtanzania tu.

Ni kama ndugu katika familia, huwezi kumkataa ndugu yako kwa sababu kafanya vibaya, utakuwa katika denial tu.

Utanzania si sifa ya kitawa wala kiwalii.
 
Tatizo taifa halina muongozo, na kama upo kwenye makaratasi viongozi wa kuuweka kwenye matendo hawapo. Kwani tulio nao wanahitaji na wao kusimamiwa.
 
Mzee huyu mtu atakuwa amekukera sana, lakini hizo ndio tabia za viongozi wetu wengi tulionao hapa nchini, Tutumie nafasi zetu kuleta mabadiliko ikiwa ni pamoja na kubadilisha viongozi waliokuwepo....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom