Kwanini sherehe za muungano huwa hazifanyiki Zanzibar?

Hizi sherehe za upande mmoja zinakera sana! Tanganyika isemwe kama Zanzibar inavyosemwa
 
Jamani hili ni swali ambalo mimi binafsi huwa najiuliza! Miaka karibu yote sherehe za Muungano huwa zinafanyikia uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam kama sikosei ila kama nimekosea mwenye ukweli wa jambo hili atujuze.

Hii nayo inaweza kuwa ni kero mojawapo ya Muungano?
 
Mleta mada, uko sahihi kabisa wala hukukosea. Hata sherehe za uzinduzi wenyewe wa muungano zilifanyika D'Salaam.

Na hata picha ya Rais kwenye noti ya Tanzania imekuwa na sura ya Nyerere hadi juzi tu kero hiyo ilipopigiwa kelele na nadhani miaka ya 2000 ndipo ikaingizwa picha ya Karume.

Unajua muungano una vikero vingi ambavyo havionekani lakini vikiibuliwa hoja zake hazijibiki.

Sijui ni lini mtu ataleta hoja kwamba Karume aitwe Baba Mdogo wa Taifa, nayo ikawa kero na hutaweza kuipinga maana ina ukweli.
 
Jamani hili ni swali ambalo mimi binafsi huwa najiuliza! Miaka karibu yote sherehe za Muungano huwa zinafanyikia uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam kama sikosei ila kama nimekosea mwenye ukweli wa jambo hili atujuze.

Hii nayo inaweza kuwa ni kero mojawapo ya Muungano?


Kwanini wapeleke ZANZIBAR wakati hawautaki huo MUUNGANO? Muungano umebaki kwa CCM Bara na Baadhi ya Viongozi wa CCM Zanzibar; Kwasababu Sidhani Makamu wa kwanza wa Rais atahudhuria na pia Rais wa Zanzibar ni Chameleon

Ni BORA kuuvunja na kama wataamua kuwa na DUAL citizenship btn Zanzibar na Tanganyika ili kuokoa kina MWINYI na BAHRESA na ARDHI zao Bara...
 
... Ndugu wadau inabidi tutazame suala la Muungano kwa mapana zaidi bila kupendelea au kuegamia upande mmoja wa muungano...
-Labda niwaulize makao makuu ya taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yako wapi?
- Pili kwanini Znz(Unguja, Pemba) hajiwakilishi kama Taifa.
- Na kwa nini pale zilipofanyika sherehe za Muungano paitwe Uwanja wa Taifa(taifa la Tanzania)
- Na kwanini Mkao Makuu ya taasisi za Serikali yote yako Tanzania Bara.
- Kwanini Wabunge wa Znz washiriki bungeni Dodoma,
- n.k.
Ukifikiria kwaundani utaona kuna sababu sherehe za Muungano kufanyika pale Uwanja wa Taifa, na ndiyo maana ukaitwa uwanja wa taifa.
 
Jamani hili ni swali ambalo mimi binafsi huwa najiuliza! Miaka karibu yote sherehe za Muungano huwa zinafanyikia uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam kama sikosei ila kama nimekosea mwenye ukweli wa jambo hili atujuze.

Hii nayo inaweza kuwa ni kero mojawapo ya Muungano?

... Hili suala la makubuliano ktk kati mambo ya muungano. Yawezekana kuna mambo mengi tusiyoyajua kuhusu muungano, na labda hayako wazi kwa raia. Lakini kuna usemi usemao kuwa "mwenye macho haambiwi tazama"
: kwa mfano huu utaratibu wa ccm wa kutawala nchi kwa kufuata itikadi za zamu (kidini); tangia awamu ya kwanza hadi ya sasa (Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete,..) kwa mtindo huu nina hisi kuna mambo fulani ya muungano ambayo hayako wasi kwa raia wa kawaidi.
 
How Zanzibar lost her groove in a record 4 month jan to april 64 ,its time we are told the truth about the worlds greatest untold story.
 
Na kwanini haya makampuni ya umma yanayoanzia na T hapa Tanzania bara na kule Zenji yapo mengine yanayoanzia na Z? Mfano TBC, Tanesco na TRA. Hiyo T ni Tanganyika au Tanzania?
 
Jamani hili ni swali ambalo mimi binafsi huwa najiuliza! Miaka karibu yote sherehe za Muungano huwa zinafanyikia uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam kama sikosei ila kama nimekosea mwenye ukweli wa jambo hili atujuze.

Hii nayo inaweza kuwa ni kero mojawapo ya Muungano?

Nawewe kuwa makini basi mbona unaona visiwani tu je sisi wa Ntwara na Lindi hatutaki hizo sherehe?
 
one.jpg

Mwaka 2011 "Sherehe za Muungano mara hii nihapa
April 7, 2011"

Makamu wa pili wa rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akitoa taarifa kwa kamati ya sherehe na mapambano kuhusu sherehe za Muungano kufanyika hapa Zanzibar.

Sherehe za kuadhimisha miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinatarajiwa kufanyika rasmi hapa Zanzibar tarehe 26 April, 2011 katika Kiwanja cha Aman Mjini Unguja.Taarifa hiyo rasmi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Zanzibar, ambaye niMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi katika kikao cha Halmashauri hio kilichofanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi wa Mnazi Mmoja.
Alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshatoa uwamuzi huo ambao umepokelewa kwa furaha na tayari umesharidhiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dr Ali Mohd Shein.
Kikao cha leo kilikuwa na Madhumuni ya kupokea taarifa hiyo na mapendekezo ya Kamati Tendaji ya Maandalizi ya Sherehe hizo, yaliyotokana na mikutano miwili ya Kamati Tendaji zilizokua na wajumbe wa Bara na Visiwani iliyofanyika Zanzibar na Dar es Salaam katika miezi ya Februari na March mwaka huu.
Wakati huo huo Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameliagiza Baraza la Manispaa la Mji wa Zanzibar kuweka taratibu nzuri za utupaji wa taka katika Mji huo na kuwaelimisha wananchi wasitupe taka ovyo.
Agizo hilo alilitoa katika ziara fupi aliyoifanya katika pwani ya Kilimanina Bustani ya miti mashuhuri ya Kilimani juu, kuangalia hali ya usafi katika maeneo hayo kwa wakati huu wa mvua za masika.
Aidha, alikubali ushauri wa Mwanachi mmoja Ndugu Issa Mohammed wa kuzuwia mmongunyuko wa ardhi kwa vigogovya minazi katika eneo la pwani ya Kilimani ili maji yasipande juu mitaani.

CHANZO: ZNZ YETU
 
Jamani hili ni swali ambalo mimi binafsi huwa najiuliza! Miaka karibu yote sherehe za Muungano huwa zinafanyikia uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam kama sikosei ila kama nimekosea mwenye ukweli wa jambo hili atujuze.

Hii nayo inaweza kuwa ni kero mojawapo ya Muungano?

"SHEREHE ZA MUUNGANO MWAKA 2011"

Mvua yasitisha sherehe za Muungano
April 26, 2011

MVUA kubwa iliyoanza ghafla jana ilisitisha sherehe za maadhimisho yamiaka 47 ya muungano waTanganyikanaZanzibarkatika uwanja wa Amaan mjiniZanzibar.Sherehe hizo zilizoanza majira ya saa 3;00 asubuhi ziliingia dosari hiyo huku tayari mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshakagua gwaride na kujumuika na viongozi wenzake katika jukwaa kuu.
Viongozi wengine waliokuwepo katika sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Dk Ally Mohammed Shein, Makamu wake wa kwanza Seif Sharrif Hamad na makamamu wake wa pili Balozi Seid Idd.
Wengine waliokuwepo ni pamoja naMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anna Makinda, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange, Mkuu wa jeshi la Polisi Said Mwema, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Rais mstaafu wa awamuya sita wa SMZ Dk Salim Amour.
Vilevile walikuwepo viongozi wa vyama vya siasakamavile mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Katibvu mkuu mstaafu wa CCM Philip Mangula, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia na wanadiplomasia wanaoziwakisha nchi zao nchini.
Rais Kikwete aliingia uwanjani hapo majira ya saa nne asubuhi akiwa kwenye gari la wazi na kuwapungua mamia ya wananchi waliokuwepo uwanjani hapo na baadaye kukagua gwaride.
Baada ya hapo gwaride lilipita mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa kasi na mwendo wa pole.
Ulipowadia wakati wa halaiki iliyoshirikisha wanafunzi 500, ndipo mvua ilianza kunyesha na baadaye kuivuruga kabisa sherehe hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo kipindi kilichokuwa kikifuata ni ngoma za asilia. Lakini mvua ilipozidi washereheshaji walitangaza kukatisha sherehe hiyo na viongozi wakaanza kuondoka.
Kauli mbiu ya sherehe hiyo ilikuwa ni “Miaka 47, tuwaenzi waasisi wetu, Tudumishe muungano, matunda ya miaka 47 ya mapinduzi na miaka 50 ya Uhuru, amani, utulivuna maendeleo ni matokeo ya muungano wetu, zilionekana kudorora hasa kutokana na mahudhurio hafifu ya wananchi. Sehemu mbalimbali za uwanja huo zilionekana kuwa wazi huku wafuasi wa CCM waliokuwa wamevaa sare nao wakiwa wachache.
Hata hivyo sherehe hizo zilionekana kudorora hasa kutokana na mahudhurio hafifu ya wananchi. Licha ya wanafunzi waliokuwa wamevaa sare nyeupe na wale waliovaa sawa na rangi za bendera ya Taifa na wafuasi wa CCM. Maeneomengine ya uwanja huo yalikuwa wazi.
Taarifa zaidi zinasema kuwa Serikaliilituma mabasi zaidi ya 20 vijijini ili kukusanya watu kwaajili ya kuhudhuria sherehe hizo, lakini hawakufika.
Hali hiyo imejitokeza huku kukiwa na manung’uniko mengi kutoka kwawananchi visiwani humo wakitaka muungano huo ufanyiwe tathimini upya.
Wakati huo huo, Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar umetoa tamko kuhusu hali ya muungano.
Huku wakitoa ushahidi wa tume kadhaa zilizoundwa ili kutafuta maoni ya wananchi kama vile Tume ya Jaji Nyalali na ile ya Jaji Kisanga, jumuiya hizo zimesema kuwa muungano kati yaTanganyikanaZanzibarumekosa kukubalika ba Wazanzibari tangu siku yake ya kwanza hadi leo.
Huku wakikilaumu CCM kwa kuhodhimuungano, wamesema kuwa nguvu zaZanzibarkatika kama mshirika mmoja kamili wa muungano huo hazipio kwa kuongezewa mambo yamuungano nay ale yasiyo ya muungano yamekuwa yakiilemeaZanzibar.
“Kwa karibu miaka yote 47 muungano huu umekuwa ni miliki ya chama kimoja cha siasa cha CCM, ukitoa miaka michache ya 1964-1977”.
Jumuiya hizo zimetaka kuwepo kwa majadiliano ya muungano ambapo wametaka pia nafasi ya Rais waZanzibarkatika muunganokamamakamu wa kwanza wa Rais.
“Mjadala wowote wa muungano ule urudishe nafasi ya rais waZanzibarkatika muungano na sio ilivyovyo hivi sasa ambapo Rais waZanzibarya maana wala amri yoyote ile katika muungano” imesema taarifa hiyo.
bi-samia.jpg

CHANZO: ZNZ KWETU
 
Huu Si Muungano ni mashaka tu maana tokea siku ulioasisiwa Mpaka Leo mashaka matupu na hauna ridhaa ya Wananchi wa pande mbili za Muungano
 
Back
Top Bottom