Kwanini sherehe za muungano huwa hazifanyiki Zanzibar?

Zamani walishawahi kufanyiaga huko, ila kwa sasa hawawezi tena kupeleka ujinga wao huko. Wapemba hawataki kabisa takataka inayoitwa Muungano.
 
ikifanyikia zenj, rais wa jamhuri ya muungano atadhalilika kwa kuwa ataingia kabla ya rais wa zanzibar halafu mizinga itapigwa mara mbili yaani kwa rais wa zenj na wa muungano vilevile itabidi kuingia gharama ya kubeba watu toka bara wakajaze uwanja sababu wazenj wengi hawatahudhuria!! yaani itakuwa haileweki mkuu wa nchi ni nani.
 
Hivi in reality kabisa by calling a spade a spade, ni kwa nini bara tunaubembelezea muungano wakati sioni tutakachopoteza? Someone plz use simple lingua for my pretty head to understand.
 
Wewe unayejua si uniambie

Usianzisha jambo ambalo hujafanya utafiti wa maana.... ninichojua huwa tunapaokezana kuandaa hizi sherehe, kama mwaka huu zinafanyika Dar, basi mwaka jana sizifanyika zanzibar.... soma hii utajua

[h=2]JK kuongoza sherehe za miaka 47 ya Muungano[/h]

By Mwinyi Sadallah

26th April 2011

Watanzania leo wanaadhimisha miaka 47 ya Muungano wa Tanzanyika na Zanzibar. Sherehe za kilele cha maadhimisho hayo zitafanyika katika uwanja wa Amaan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ataongoza sherehe hizo zinazotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wote wa kitaifa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya maadhimisho hayo, milango ya uwanja wa Amaan itafunguliwa kuanzia saa moja ya asubuhi ili kutoa nafasi ya wananchi kuingia uwanjani na mapema.
Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili uwanjani saa nne asubuhi akiongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, ambapo atakagua gwaride rasmi na kupigiwa mizinga 21 kabla ya kupokea gwaride litakalopita kwa mwendo wa pole na haraka.
Ratiba haikuonyesha kama Rais Kikwete atahutubia katika sherehe hizo.
Muungano wa Tanzania uliundwa April 26, 1964 kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar chini ya waasisi wa taifa Marehemu Mwalimu Julius Nyerere na Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
Sherehe hizo zinafanyika huku makundi ya wanzanzibari wakitoa maoni yao kwamba Muungano unahitaji ukarabati mkubwa ili kwenda na wakati. Juzi, Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, aliwataka wazanzibari kutovunja Muungano wa Tanzania kwa visingizio vya mawazo ya Katiba mpya na kuwataka wananchi kuepuka mijadala inayotoa ushawishi wa kukataa Muungano kwa kisingizia cha Katiba mpya.
Manispaa ya Zanzibar imepambwa kwa bendera za taifa na mabango yenye ujumbe wa kudumisha Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimesema faida za Muungano haziitaji tochi kuonekana kwa vile umesaidia kujenga misingi ya umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Tanzania.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, alipokuwa akitoa tathmini ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Alisema tangu kufikiwa kwa Muungano huo fursa za uwekezaji katika sekta ya biashara, kilimo na elimu zimekuwa zikiongezeka na kuongeza kipato kwa wananchi wa pande mbili za Muungano.
Hata hivyo, alisema wananchi wengi Zanzibar bado hawajatumia fursa ya kuwekeza katika sekta ya kilimo katika mikoa ya Tanzania Bara kutokana na wengi wao kuwekeza zaidi katika sekta ya biashara ya maduka.

SOURCE: NIPASHE

hamna mtu anataka huu muungano zaidi ya serikali zetu, watanganyika hawautaki wazenj hawautaki, inabidi twende na wakati this is 2012 kila nchi iwe na uhuru wa kufanya inachotaka...tutasemaje sisi ni nchi moja wakati kuna bunge mbili, serikali sijui ziko mbili na kama watanganyika nini faida ya kuungana na zanzibar....what do we really gain from them?
 
ikifanyikia zenj, rais wa jamhuri ya muungano atadhalilika kwa kuwa ataingia kabla ya rais wa zanzibar halafu mizinga itapigwa mara mbili yaani kwa rais wa zenj na wa muungano vilevile itabidi kuingia gharama ya kubeba watu toka bara wakajaze uwanja sababu wazenj wengi hawatahudhuria!! yaani itakuwa haileweki mkuu wa nchi ni nani.

Nimeipenda hii...!
 
muungano ukivunjika tutaishi kama sudan kusini na sudan kasikazini.......acheni muungano ubaki hivi
 
Hivi in reality kabisa by calling a spade a spade, ni kwa nini bara tunaubembelezea muungano wakati sioni tutakachopoteza? Someone plz use simple lingua for my pretty head to understand.

Mkuu Wazenj ndio wanaoubembeleza Muungano, achana na waganga njaa wachache wanaodai kuwawakilisha Wazanzibari wote na kudai kuupinga!
 
Usianzisha jambo ambalo hujafanya utafiti wa maana.... ninichojua huwa tunapaokezana kuandaa hizi sherehe, kama mwaka huu zinafanyika Dar, basi mwaka jana sizifanyika zanzibar.... soma hii utajua

[h=2]JK kuongoza sherehe za miaka 47 ya Muungano[/h]

By Mwinyi Sadallah

26th April 2011

Watanzania leo wanaadhimisha miaka 47 ya Muungano wa Tanzanyika na Zanzibar. Sherehe za kilele cha maadhimisho hayo zitafanyika katika uwanja wa Amaan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ataongoza sherehe hizo zinazotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wote wa kitaifa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya maadhimisho hayo, milango ya uwanja wa Amaan itafunguliwa kuanzia saa moja ya asubuhi ili kutoa nafasi ya wananchi kuingia uwanjani na mapema.
Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili uwanjani saa nne asubuhi akiongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, ambapo atakagua gwaride rasmi na kupigiwa mizinga 21 kabla ya kupokea gwaride litakalopita kwa mwendo wa pole na haraka.
Ratiba haikuonyesha kama Rais Kikwete atahutubia katika sherehe hizo.
Muungano wa Tanzania uliundwa April 26, 1964 kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar chini ya waasisi wa taifa Marehemu Mwalimu Julius Nyerere na Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
Sherehe hizo zinafanyika huku makundi ya wanzanzibari wakitoa maoni yao kwamba Muungano unahitaji ukarabati mkubwa ili kwenda na wakati. Juzi, Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, aliwataka wazanzibari kutovunja Muungano wa Tanzania kwa visingizio vya mawazo ya Katiba mpya na kuwataka wananchi kuepuka mijadala inayotoa ushawishi wa kukataa Muungano kwa kisingizia cha Katiba mpya.
Manispaa ya Zanzibar imepambwa kwa bendera za taifa na mabango yenye ujumbe wa kudumisha Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimesema faida za Muungano haziitaji tochi kuonekana kwa vile umesaidia kujenga misingi ya umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Tanzania.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, alipokuwa akitoa tathmini ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Alisema tangu kufikiwa kwa Muungano huo fursa za uwekezaji katika sekta ya biashara, kilimo na elimu zimekuwa zikiongezeka na kuongeza kipato kwa wananchi wa pande mbili za Muungano.
Hata hivyo, alisema wananchi wengi Zanzibar bado hawajatumia fursa ya kuwekeza katika sekta ya kilimo katika mikoa ya Tanzania Bara kutokana na wengi wao kuwekeza zaidi katika sekta ya biashara ya maduka.

SOURCE: NIPASHE

JF RAHA SANA! Ama kweli HAKUNAGA
 
Tanganyika yetu tunaitarajia soon tumechoka kumezwa twaidai Tanganyika yetu
 
Mwaka huu sherehe zingefanyika Znz, kungekua hamna gwaride labda maandamano ya kupinga.
 
Back
Top Bottom