Kwanini Serikali isiombe kushirikiana na JF badala ya kuiua?

Mr.mzumbe

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,014
957
Mpaka sasa bado najiuliza jinsi swala zima la jf kuchukuliwa kama blog ya hovyo hovyo.
Hili swala linaniumiza kichwa kidogo kitendo cha wabunge kuugua JFRISM uku wabunge wenye tiba wapo.
Sasa hii imaanisha nn?hata hao n active memba wa jf nao wameunga mkono harakati hizi?hii inaonesha wabunge wetu ambao ni memba wa jf hawapend kuambiwa ukweli.
 
Najua rafiki yangu wa Kigoma kaskazini alikuwa anaunga mkono hoja ya jf kufungiwa uli tuhamia kwenye twita na fesibuk
 
Lilikuwa ni swali kwa Waziri, So hakukuwa na muda wa kuanza kuitetea JF
 
Kwa walioangalia Bunge jana ilikuwa hivi...baada ya swali la Rwakatare kuulizwa na Hilda Ngoye kwa niaba yake,Spika aliomba majibu.Na majibu yalipotolewa na wizara kupitia kwa waziri majibu yalikuwa safi na waziri hakuishambulia JF kabisa.Na hapa namtetea waziri vizuri kabisa.Baada ya kujibu swali la msingi,Spika aliruhusu swali la nyongeza.

Na kwa kweli hata Hilda Ngoye wakati anauliza swali la nyongeza akuigusa JF kwa jina lake,isipokuwa aliongea kauli kuwa kuna mitandao inatukana matusi,na vijana wadogo wanatembelea internet cafe wakiwa na umri mdogo kwa hiyo ni sehemu ya kuharibu maadili.Sasa wakati spika anamruhusu Waziri kujibu ndio akaongeza...

na hapa namnukuu "MWESHIMIWA WAZIRI MAJIBU,NA UNAPOJIBU ZINGATIA SWALI LA MSINGI,LINALOULIZA KUHUSU JAMII FORUM MAANA NI TATIZO KUBWA SANA KWASASA..." Lakini nzuri zaidi kwa mara nyingine waziri akuigusa JF zaidi alisema hii mitandao ni sehemu muhimu ya kupeana taarifa.

My take:
Nadhani ifahamike kuwa anayekereka na JF atakuwa na haya yafuatayo;
  1. Ni moja ya mafisadi...
  2. Ni moja wa watu wanaofahidika na mfumo wa sasa wa kifisadi..
  3. Ni watu wasiotaka kuona uchafu wa serikali na wanasiasa wetu unafichuliwa...
 
Swali liliulizwa kwa Waziri, mbunge huwezi kuamka na kujibu badala ya waziri. Na maelezo ya waziri hayakuichafua JF!
 
Swali liliulizwa kwa Waziri, mbunge huwezi kuamka na kujibu badala ya waziri. Na maelezo ya waziri hayakuichafua JF!
Kwa maana nyingine ni kwamba serikali haioni kama JF ni tatizo. Muuliza swali (Lwakatare) pamoja na Naibu Spika (kwa kauli yake) ndio wanadhani JF ni tatizo!
 
Ndugu wana JF, ninapata taabu sana kuelewa mawazo na fikra za baadhi ya wabunge wanaodiriki kuichongea JF bungeni na serikalini eti inatoa taarifa za uongo.

Nina mawili ya kuweka jamvini;
Mosi, kama serikali kupitia baadhi ya wabunge wanaona kwamba JF inatoa taarifa za uongo kwa jamii kwanini wasifunguke na kuweka wazi hizo taarifa hapa jamvini ilikuondoa lawama?
Pili, kwanini wengine wanaotembea JF kwa mfano marehemu Regia Mtema aliona umuhmu wa JF kwa upande wa kujua kero za wananchi?
Tatu, kwa kuwa JF inatembelewa na watu wengi, kwanini serikali na vyombo vyake isione kama ni fursa ya kuwafikia jamii katika kifanya mashausriano (consultation)?
Ni bahati mbaya sana kwamba wamechagua silaha dhaifu ambayo ni kuitishia JF kwa kujaribu kuchimba taarifa za nani mwanzilishi, imesajiliwa wapi na mengine mengi ambayo kimsingi hayana tija kwa jamii ya watanzania ambao wanakerwa na ugumu wa maisha na siasa inayojenga uongozi wa kifalme badala ya kuwahudumia wa Tz kwa paomoja.

Haya ni maoni yangu kwa leo!

Naomba kuwasilisha wangwana!
 
angekuwepo Regia angetetea mpaka kikaeleweka, wengi wao hawapendi siri zao kuvuja ndio maana wanaishikia Bango.

Kabisa mkuu,aiseeee!!comment yako imenigusa sana ni kama kuna maneno fulani kwenye wimbo mmoja wa 20% (...angekuwepo mwalimu nani angeiba hela...)Huwa yananihuzunisha sana pia.RIP Regia
 
Mkuu haya maswali sijui angeulizwa Mh.Pinda (Mb) siku ya alhamis pale bungeni Dodoma!!!!!????
 
Hapa ninapata wasiwasi ususani uwezo wa hawa jamaa kufikiria kwa mapana bila kuangalia kila kitu kwa jicho la kipinzani!
 
Back
Top Bottom