Kwanini Safari Bia imepungua umaarufu?

Tuliambiza wenyewe humuhumu kwenye jukwaa kwamba safari bia inapunguza nguvu za kiume sasa yaelekea hayo ndio matokeo yake.
 
Safari Lager ni msamiati wa bia,ingawa TBL hawataki kujua kuwa wameiua Safari Lager na haiuziki mjini wao hawaamini,soko la Safari lager limebaki vijijini tu ambako kabia kamoja kanachanganywa na kangala debe ,huko vijijini hakuna hela sasa TBL kama wanategemea soko la wakulima vijijini huo ndio mwanzo wa kusema hapo zamani kulikuwa na bia inayoitwa Safari lager na sasa ukitaka kuiona nenda Jumba la Makumbusho
 
inaumiza kichwa-wanaokunya kwa sasa wanazid kupungua-watu wengine hawatak kulewa haraka,wanataka kukaa bar muda mrefu
 
Mimi nilikuwa mnywaji mzuri wa Safari lager. Lakini mwaka jana nilikuta kuwa imekwishachakachuliwa na TBL. Safari bia ya sasa siyo ile tuliyokuwa tunakunywa enzi zile kabla ya Breweries kukabidhiwa Makaburu. Nimehamia Serengeti nikiwa Bongo na ile nyingine inaitwa malt. Au hata Guiness. Safari kwishney.
 
Tatizo safari inatengenezwa kwa kutumia teknologia ya zamani ya kuongeza sukari ambayo inamadhara makubwa kiafya na sehemu nyingi duniani wameacha kuongeza sukari kwenye bia,bia kama Castle(TBL) na bia zote za SBL hawaweki sukari kwahiyo madhara yake sio mabaya kama Safari na bia zingine zinazoongezwa sukari.
 
Eeee brew master wasamehe hawa, kwa maana hawajui walinenalo.
Nadhani ndimi zenu zimepata sugu kwa kunywa viroba ndiyo maana mnaona ladha ya safari lager imebadilika, nikwambieni kitu formula ni ile ile.mmehongwa nyie.
 
Wapasua mawe wamepungua. Ndo bia yao. Akitoka kwenye gongo anapitia baa kusuuza na moja wakati anasubiri baa maid afunge kazi wakajiburudishe.
 
safari inakufanya ujione we ndo mbabe kuliko kiumbe chochote.
Wanywaji wa safari ndio wanaongoza kwa kuzua fujo bar na kuwapiga wake zao nyumbani.
 
Imepungua umaarufu labda mijini. Maana ukiwa vijijini ukisema bia unamaanisha Safari lager
<br />
<br />

Nakuunga mkono mkuu, waache hao wanadarisalama wazee wa chips mayai chips kuku, mzigo huu wa ukweli hawauwezi. Wazee wa kujiekti wakiwa na mademu pub zao ooh leta hei*k*n, leta m*ll*r, leta wind**k, sijui cas*le lite na nini huko. Huku mawilayani mwendo ni safari na balimi tu kudadadeki
 
Breweries fanyeni utafiti muone kama mauzo ya Safari jumlisha mauzo ya Castle yamebaki pale zamani na sasa. Kama ni hivyo basi tatizo itakuwa hakuna. Faida yenu iko palepale. Kama havilingani basi kubalini kuwa kuna tatizo kwenye Safari na muifanyie ama sivyo Serengeti itawapiku.
 
Back
Top Bottom