kwanini polisi?

Baiskeli

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
336
61
Jamani wengi wetu hatupendi udini wala ukabila. leo hii ukiulizia jamani igp ni dini gani, utaitwa mdini, sasa kwanini polisi lazima uandike dini na kabila lako? huo si udini?
 
"Wanataka kujua kuwa u jamii ya 'magaidi' au ya 'mashoga"
 
Kuhusu swala kwa nini Polisi uandike dini yako na kabila hilo si tatizo labda tatizo tujiulize kwa nini siku hizi mfumo wa kuchukua takwimu kwa kuangalia dini kabila nk umeacha...Maana kwa kifupi unapofanya hivyo mathalani...Katika Polisi inawezesha serikali kujua uwiano uliopo katika jamii ili kila jamii ipate haki stahiki...Kwa hiyo wadau tusiwe na shaka na hile. Shaka iwe tu ni kwa nini hili halifanyiki kwa nyanja nyingine?
 
Hiviitakuwaje kama ukiulizwa swali hilo na ukasema sina DINI au Mpagani watasemaje? Maana pia sio lazima kuwa na Dini au ukawa muumini wa dini za Asili ya Pagani.
 
Nafikiri mambo ya kuulizana dini makazini, hapo zamani, yalikuwa na Mantiki ya kudhibiti utoro au ukwepaji majukumu. Ina maana kuwa, isije ukawa umeandika wewe ni mkristo, halafu Ijumaa unakwepa kwenda doria kwa kudai unaenda Masjid, au labda wewe ni Muislam, ukatae lindo Jumapili kwa kudai unaenda Kanisani. Kwa kuandikisha dini ndani ya jeshi la polisi, inawezekana kiubinadamu, kwa Mkuu kutoa ruhusa spesho kwa mtu kuhudhuria shughuli au tafrija za kidini bila kudanganyana.

Haya ni mawayo yangu tu, hayawakilishi mtazamo wa watendaji wa utumishi walioanzisha taratibu hizi.
 
Kaseme kuwa wewe ni mpagani utapgwa virungu mpaka ukome.
Utasikia wakisema, mura hebu riongeze virungu vitano vya jichoni na vinne vya kwenye meno hadi ritaje kabira rake.
Kuna mfanyakazi wetu wa ndani alikamatwa kwa kufaminiwa, alikuwa anaitwa polisi, akapelekwa polisi, mapiolisi wakampiga hadi akapoteza fahamu wakisema kuwa anawadhihaki.
Tanzania na polisi wake ni mazuzuz magic, ndio maana maswali ya kipumbavu ni mengi mno.
hiviitakuwaje kama ukiulizwa swali hilo na ukasema sina dini au mpagani watasemaje? Maana pia sio lazima kuwa na dini au ukawa muumini wa dini za asili ya pagani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom