Kwanini Pengo asiende mwenyewe kuhiji Butiama?

Mimi sioni haja ya Rais na Marais wastaafu watatu (Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa) kuwepo pale. Kwani ni national issue? Au kwa lipi jema alilofanya Polycarp Kadinali Pengo? Upuuzii mtupu. Watu wa dini waendelee na mambo yao ya kiroho na wanasiasa waendelee na siasa ...

Umeshasema wastaafu. Hawana kazi wenzio. Sasa kuna ubaya gani wao kwenda kujiachia sehemu mbalimbali na tofauti? Wewe ulitaka wawe wapi?
 
......walipewa mwaliko na wakahudhuria ..hawakulazimishwa .........wangeweza pia kuacha kwenda..sasa wewe shangaa kwa nini wamehudhuria wote...!

ni vigumu kwa mtu mwenye akili kupuuza role ya kanisa katika huduma za jamii....hasa pale unapokuta karibu asilimia 40% ya huduma za jamii zinatolewa na kanisa........watanzania wengi wapo vijijini....na huko ndiko wanakotoa huduma,...hawana haja ya kufungua kwa wingi huduma hasa za afya mijini ambako mnapata private hospitals ,,,,..vijijini watu wengi wana shida na wanapewa huduma nzuri kwa kuchangia kidogo au bila malipo..........sasa kama mtu anataka kuwaona hawa kina pengo hawana maana basi na yeye apeleke huduma huko ...afikiri ni rahisi!!!!

afteral wale unaoshangaa kwa nini wamehudhuria pale ...watoto wao ndio wanaosoma....st.marian,kifungilo,st.joseph....etc.


8D6U8671.JPG



wenyewe wote wako hapo. Picha kwa hisani ya MICHUZI blog
 
Cynic,
Hata hivyo yawezekana alikuwa akimpa somo MKAPA ajirudi. Just imagine MKAPA na madhambi yake dhidi ya watanzania anaenda kutembelea kaburi la Nyeyere?
Hii ndiyo habari nilitegemea kusikia toka kwa mtu mzima huyu lakini nadhani anaona raha tu na utukufu alokuwa nao..Kisha ukisoma hakumtaja Mwinyi ambaye niliwahi kusikia lawama zao sikutaka kuamini kama nilivyokataa kuamini ya Mwalimu na kanisa hilo...
Sasa nikichukulia maelezo yake na habari ambazo zilikuwa zikisambaa kuhusiana na serikali zetu ktk maswala ya dini na hasa kanisa hili inanipa wasiwasi kuwa yawezekana kuwepo Ukweli fulani..Hii initisha hata kama kanisa katoliki wanasaidia sana wananchi.. As a fact kama mimi ningekuwa rais huduma zote za Afya (Hospital) na Elimu ndio NGO pekee ningewapa ruksa na baraka zote kwani hawa jamaa inapofikia ktk maswala haya nawapa salute.. hayo ya kiroho ni jukumu la kila dini kujiendeleza..
 
hapa naona Cardinal alitumia lugha ya kiutu uzima , kwamba Mkapa akaombe radhi huko Butiama na kujutia Dhambi alizo wafanyia wa tanzania
 
MtindiowaUbongo,
Mkuu acha unazi hauna maana sisi watu wote wazima hapa..soma vizuri maelezo ya huyu kiongozi wa dini utaelewa nachozungumza.. Ni Ujinga mtupu... samahani lakini, - kwani kila unaposhukuru kuwezeshwa wewe ina maana kuna wengine hawakuwezeshwa..
Kwa nini wewe unashindwa kuamini upande wa madai ya kutowezeshwa ila unaamini na kukubali upande wa kuwezeshwa kama sii mvua ilikunyeshea!

Hivi unaweza kusema serikali ilimwezesha nini Pengo? Halafu sikujua kuwa ukitoa shukrani kwa mtu ina maana alikupa kitu, tena alikuteua na kukupendelea kutoka ktk umati wa wengine!

Safi sana mzee. Hawa ndo ma-great thinkers wa JF! Pure mashudu!
 
Mimi sioni haja ya Rais na Marais wastaafu watatu (Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa) kuwepo pale. Kwani ni national issue? Au kwa lipi jema alilofanya Polycarp Kadinali Pengo? Upuuzii mtupu. Watu wa dini waendelee na mambo yao ya kiroho na wanasiasa waendelee na siasa ...

Marais kwani hawana maisha binafsi?

Ishu ipi ina-qualify kwako kuwa ishu ya taifa?

Kama humuheshimu Pengo, waheshimu basi wale wafuasi wake anaowaongoza, kama huwezi basi subiri na wewe zamu yako..!
 

......gagnija ..inawezekana wewe sio mkatoliki ..lakini kwa kifupi kanisa katoliki huwa halitegemei wala kukubali kumtegemea muumini mmoja kwa mapato....hata kama unayo pesa ya kujenga na kulisha kanisa lote peke yako hawatakubali zaka yako peke yako...kwani kanisa ni la watu wote,mkapa anajuwa utaratibu huo...hata kama anatoa sadaka atakuwa kama waumini wengine wenye uwezo tu....

nikirudi kwenye mada ...nemebahatika kupata huduma za makadinali RUGAMBWA na PENGO....wote walikuwa na mshango mkubwa kila mmoja kwa wakati wake.

Wakati wa utawa wa cardinal pengo ...ndio wakati serikali iliruhusu kanisa kuendelea na huduma za shule na hospitali,amefanikiwa kiasi kikubwa kujenga mashule mengi .....sasa hivi hapa dar karibu kila parokia inayo shule.....na kila kitongoji kuna kanisa...amefanya juhudi kubwa sana kuunganisha nguvu za waamini,...

amefanikiwa kwa upande wa upashanaji habari kwa kuanzisha magazeti na kuimarisha redio [au uanzisha]....na kuanzisha televisheni .

mahospitali yamefunguliwa kwenye parokia nyingi.....

kwa kushirikiana na maaskofu wengine ...baada ya kuruhusiwa na serikali ndani ya miaka 15 ....wameweza kuimarisha hospitali ya rufaa ya BUGANDO,....pia wameweza kuimarisha hospitali zao zilizoenea kila wilaya nchini[ambazo nyingi ndio zinatumiwa na serikali kutoa huduma ya hospitali za wilaya kwenye maeneo ambayo bado serikali haina hospitali zenye hadhi hiyo.....

katika kipindi hicho wameweza kujenga vyuo vikuu ,iringa,mwanza,moshi,etc...vyote vikijulikana kama st.augustine... pia wameweza kujenga chuo kikuu cha teknelojia dar es salaam [st.joseph college of engineering and technology]...tunawashukuru maaskofu,mapadre,watawa,waumini na wote wenye mapenzi mema kwa mafanikio hayo makubwa...ambayo mengi yametokana na juhudi za ndani na michango ya waumini...hasa katika enzi hizi ambazo misaada kutoka ulaya kuendesha makanisa imeshakoma.....na misaada mingi kutoka rome inaelekea sehemu zenye maafa ya vita,...etc[ie congo,east europe,darfur etc]

mwendeleo hayapiwi tu kwa mashule na universities, kuna vigezo vingi, pengo na wengine wanatakiwa kusimamia ukweli na kuhakikisha kuwa mustakabali wa amani ya taifa hili unakuwa endelevu, wanapaswa kuongea na kukemea bila kumumunya maneno, kukemea wizi, na ujambazi uliosisiwa na mwinyi, ukaendelezwa na mkapa, na sasa unashamiri kwa kikwete. nchi haiwezi kuwa na amani kama hazina ya nchi inakombwa na genge la watu wasiozidi 20, kwa wizi wao huo watatamani madaraka na wakishindwa watahonga wapiga kura, likishindikana hili wanaweza kununua silaha na kuliweka taifa matatani, hayo mashule yaliyojengwa na pengo yatageuka kuwa MAKAMBI YA WAKIMBIZI KAMA PENGO AKIENDELEA KULEWA MADARAKA NA KUWAKUMBATIA MAFISADI, NCHI JIRANI YA RWANDA TUNASIKIA KUWA HATA VIONGOZI WA DINI WALISHIRIKI MAUAJI, RWANDA NI WAKATOKILI 90%

TUWE MACHO NA AKINA PENGO

MWISHONI NATANGAZA MASLAHI YANGU KAMA MKATOLIKI NA TENA MWANAFUNZI WA ZAMANI YA SEMINARI

KWA HILI NAMENGINE PENGO AMEKUWA AKICHEMSHA, HUWA NAJIULIZA NI KWELI ALISTAHILI KUWA KARDINALI? WAKO WNAOSEMA ALIYESTAHILI NI MTUMISHI WA MUNGU MHASHAMU ASKOFU MAYALA, HUYU SIJUI ALIDANDIA NAMNA GANI

HE CAN BORROW A LEAF FROM RT REV.PIUCE NCUBE THE THEN ARCHIBISHOP OF BULAWAYO
 
Mtindiowaubongo,
Hivi unaweza kusema serikali ilimwezesha nini Pengo? Halafu sikujua kuwa ukitoa shukrani kwa mtu ina maana alikupa kitu, tena alikuteua na kukupendelea kutoka ktk umati wa wengine!
Hii swali ndilo ungemuuliza Pengo aliyesema na kusifia, na ndio maana nikasema mzee mzima kachemsha!.. inafanya watu wajiulize maswali mengi!..
 
Mtindiowaubongo,

Hii swali ndilo ungemuuliza Pengo aliyesema na kusifia, na ndio maana nikasema mzee mzima kachemsha!.. inafanya watu wajiulize maswali mengi!..

Tatizo ni uelewa wako na wala si Mzee Pengo! Yeye alichosema ni kuishukuru serikali kwa kuweka mazingira yaliyoliwezesha kanisa lake kufanya kazi vyema. Sasa wewe kwa sababu ya uelewa wako dilated, unadhani labda kanisa la Pengo limepewa special treatment na serikali, ndio maana nikakuuliza unajua unachoongea? and you did not dissapoint with uncorrelated answer.

ungemuuliza Pengo

Yaani unaanzisha dhana halafu unasubiri mwingine ai-substantiate!! It can't get funnier than this, ai?
 
Mtindiowaubongo,
Kiswahili lugha yetu haihitaji tafsiri ili mtu apate kuelewa.. mimi sii mgeni wa lugha hii.. soma tena alichosema kisha nambie kwa hatua umeelewa vipi!..
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, amemtuma Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kwenda kuhiji alipozikwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na kufikisha shukurani zake kwa kazi aliyoifanya kujenga mazingira yaliyoliwezesha Kanisa kupata mafanikio.

Kadinali Pengo pia alimshukuru Mkapa, marais waliomtangulia na mrithi wake, Rais Jakaya Kikwete, kwa kuendeleza mazingira hayo yaliyoliwezesha Kanisa kufanikiwa katika shughuli zake za kiroho na kijamii...

Haya mkuu wangu sii maneno ambayo kila siku waislaam wanapigia kelele na kanisa lake hukataa kata kata kuwa haikuwa hivyo, leo iweje aseme maneno haya ya shukran akiwa na maana tofauti!..
Ni mazingira gani YALIYOJENGWA kuwezesha kanisa lifanikiwe..

Alichotaka kusema ni kumpasha Mkapa indirectly kuwa ameharibikiwa na lazima aende kuhiji kaburi la mwalimu lakini ktk upangaji wa maneno yake amechemsha.. utasifia mvua tu kama imekunyeshea mkuu wangu...
 
Mkandara,

Sasa nimeanza kupata chanzo cha matatizo yako. Na si jingine ni udini ulikukaa rohoni:

maneno ambayo kila siku waislaam wanapigia kelele

Udini na chuki yako dhidi ya watu wa dini nyingine inakupofusha, na hata kushindwa kuona hata unachoandika kuwa kinakupinga.


Ktk nukuu uliyoileta, mzee Pengo anaishukuru serikali kwa kuwezesha uhuru wa kuabudu, na hivyo kuwezesha kanisa la Pengo kupata mafanikio. Thats so straight forward, na hutegemei dini yeyote kuimarika kama hamna uhuru wa kuabudu. Na hili ni jambo la kushukuru kwa sababu kuna maeneo mengi tu duniani ambapo uhuru wa kuabudu unapata dhahma, na hivyo kuzorotesha shughuli za dini mbalimbali.

Hivyo basi, ndio maana sioni unachoking'ang'ania kuwa serikali inaliwezesha kanisa, tena hadi sasa ambapo Mh. raisi ni mwislamu! Haihitaji kuwa na darubini kuona huna hoja! Kama unadhani unahoja, jaribu kujibu hili swali, lililokushinda hapo awali ukukuruke nalo;

Hivi unaweza kusema serikali ilimwezesha nini Pengo?
 
%

TUWE MACHO NA AKINA PENGO

MWISHONI NATANGAZA MASLAHI YANGU KAMA MKATOLIKI NA TENA MWANAFUNZI WA ZAMANI YA SEMINARI

KWA HILI NAMENGINE PENGO AMEKUWA AKICHEMSHA, HUWA NAJIULIZA NI KWELI ALISTAHILI KUWA KARDINALI? WAKO WNAOSEMA ALIYESTAHILI NI MTUMISHI WA MUNGU MHASHAMU ASKOFU MAYALA, HUYU SIJUI ALIDANDIA NAMNA GANI

HE CAN BORROW A LEAF FROM RT REV.PIUCE NCUBE THE THEN ARCHIBISHOP OF BULAWAYO


...ex seminarist hawezi kuandika this low...and shallow..hata kama ukitaka kumshambulia mtu ungekuwa umefundishwa na kufaulu kutumia falsafa...[philosophy]..........

Hasa unaposema kuwa nani alistahili kuwa cardinal....inaonyesha hujuwi kabisa mchakato uliopo ndani ya kanisa ...uonavyo wewe sio waonavyo wengine...na wanaoona kama wewe wanaridhika...!!

uasikofu au ukardinali haogombewi kwa kura .....

Nani huwaita wageni wake karamuni na kuanza kuwatukana..."...kila kitu kina wakati wake...kuna wakati wa kukaa kimya ..na wakati wa kupiga kelele,kuna wakati wa kurusha mawe na wakati wa kukusanya mawe,kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka........"
 
Marais kwani hawana maisha binafsi?

Ishu ipi ina-qualify kwako kuwa ishu ya taifa?

Kama humuheshimu Pengo, waheshimu basi wale wafuasi wake anaowaongoza, kama huwezi basi subiri na wewe zamu yako..!

Namheshimu sana. Issue ni kwamba wanasiasa wamezidi mno ku hang out na watu wa baadhi za dini. Na watu wa dini nao wanatumia nafasi hizo kutoa statements zenye utata. Inakuwa ni kama trend - kumbuka ni wiki hii jana tu naye Kilaini alitoa statements za ajabu ajabu
 
Katika kuichangia maada hii ni bora watu tukaweka UDINI WETU PEMBENI KIDOGO,then tusimamie kwenye ukweli.

Mimi nadhani kuna mambo mazuri pia ambayo hawa viongozi,HASWA KIONGOZI MTAJWA HAPO JUU amewahi kuyafanya katika utawala wake.

Pia kwenda kumkumbusha mkapa KUHIJI kwenye kaburi la mwalimu NI JAMBO JEMA TU.Kuhoji kwamba KWA NINI ASIENDE YEYE PENGO,naona kama ni hoja ambayo haijaenda darasa.
ANYWAYS,NI MTIZAMO TU!
i love you all
 
Katika kuichangia maada hii ni bora watu tukaweka UDINI WETU PEMBENI KIDOGO,then tusimamie kwenye ukweli.

Mimi nadhani kuna mambo mazuri pia ambayo hawa viongozi,HASWA KIONGOZI MTAJWA HAPO JUU amewahi kuyafanya katika utawala wake.

Pia kwenda kumkumbusha mkapa KUHIJI kwenye kaburi la mwalimu NI JAMBO JEMA TU.Kuhoji kwamba KWA NINI ASIENDE YEYE PENGO,naona kama ni hoja ambayo haijaenda darasa.
ANYWAYS,NI MTIZAMO TU!
i love you all


Ni kweli mkuu,

Unajua michango iliyofuata baada ya post # 1, imeniacha hoi sana, na kujiuliza kama watu huwa wanaelewa wanacho-respond au ni kuosha kinywa hadi kitakate.

Kuna mmoja amesema eti kwenda kumuomba 'marehemu' Mwalimu ni kosa, huku akisahau kuwa hata dini za mahoka wanaomba hivyohivyo! Hata kama kwenye dini yake ya kikoloni wanafuata manabii walikufa pia!

Mwingine aka-interpret kuwa serikali inalibeba kanisa la Pengo. Yaani ilimradi tu vurugumechi imekuwa shouting match.

Watu inabidi wajifunze ku-respond accordingly sio mradi tu umechangia..
 
Unajua Cardinal Pengo ni mtu mtata mtata sana mara nyingine. Msomi anayejua kutumia vema jukwaa kujenga hoja zake. Anachojaribu kufanya ni kuwaambia watu kuwa Mkapa ametufanyia makubwa so ni lazima ku appreciate...kumbuka huyu ni kiongozi mkubwa wa kiroho na hivyo sauti yake kwa watu wanaomeza issues bila kutafuna inakuwa na impact kubwa. Nionavyo, ni kuwa anataka kumsafisha Mkapa kiujanja janja. Huyu kiongozi wangu wa kiroho huwa napata shida kujua yuko upande gani mara nyingine.
Mkapa alichofanya kinastahili kuombewa toba. Kama Pengo angekuwa ana maanisha kweli aliyoyasema, angemueleza wazi Mkapa...waombe toba wadanganyika mana hukuwatendea haki.
Chakushangaza anafanya jumla jumla kama anauza mitumba ya masalo...kana kwamba aliyoyafanya Nyerere yanafanana na wengine wote include Mkapa!!! Kulikoni?
Kuna kitu muhimu kukijua kuhusu secret socities. Waumini wake wengi wamo hata active member and leaders wa dini nyingine pia.
Kwa mfano, Freemasons wana namna zao katika kuteteana na kitu kimoja muhimu sana kwao wanakiita collegiality...it means decision yoyote unayotaka kufanya usionyeshe kana kwamba ni ya kwako binafsi..kwa mfano labda askofu ana isssue ambayo haina uhusiano na mafundisho ya kweli ya dini lakini ina interest za freemasons. Wanachofanya wanaita baraza la maaskofu..huyu askofu ambaye ni freemasons anawapa wenzake hoja na kuwapa vigezo vya umuhimu wa hoja yake kuungwa mkono na asilimia kubwa hivyo mwisho wa siku hakuna atakayekuuliza wewe individual maswali maana linakuwa tamko la baraza la maaskofu..hivyo hivyo inawezekana kuwa ndani ya baraza la mawaziri au sehemu nyingine yoyote yenye manufaa kwao.Nimejiuliza sana maswali..is this one of their strategies to clean Mkapa if he is a member?
Pili, Freemasons wana kingine muhimu wanakiita brotherhood wakimaanisha member, lazima wawe na mkakati wa pamoja kwa wazi au kwa siri kuhakikisha wanateteana hata kama ni kwa kueneza uongo, kuua au vinginevyo kuhakikisha yule anayetuhumiwa anakuwa salama...Is this also one of their strategies?
Msinielewe vibaya hapa...sijui kama hawa jamaa ni members..lakini ipo Dar Lodge na ina wakubwa wengi tu. Yaliyofanyika awamu ya tatu mengi yaliwapa favor freemasons kuliko wengine wote. Tazameni vizuri na wenye jicho la kujua members watupe habari. Ila nijuavyo mimi, hawa jamaa wapo mpaka ndani ya kanisa.
Maana haiingii akilini kuona kwanini Kardinali wetu anatumia fimbo yake ya kiuchungaji kuendesha move kama hii ya kumfanya Mr Clean awe clean wakati wote tunajua ametota kwenye kashfa ambazo zinamtaka yeye binafsi atueleze yote yalivyokuwa na sio Kadinali on his behalf. Jamani hapa Kwa kardinali kuna nini?
 
Pengo amtaka Mkapa kwenda kuhiji Butiama
Basil Msongo
Daily News; Saturday,February 21, 2009 @19:00

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, amemtuma Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kwenda kuhiji alipozikwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na kufikisha shukurani zake kwa kazi aliyoifanya kujenga mazingira yaliyoliwezesha Kanisa kupata mafanikio.



Msinielewe vibaya hapa...sijui kama hawa jamaa ni members..lakini ipo Dar Lodge na ina wakubwa wengi tu. Yaliyofanyika awamu ya tatu mengi yaliwapa favor freemasons kuliko wengine wote. Tazameni vizuri na wenye jicho la kujua members watupe habari. Ila nijuavyo mimi, hawa jamaa wapo mpaka ndani ya kanisa.

Maana haiingii akilini kuona kwanini Kardinali wetu anatumia fimbo yake ya kiuchungaji kuendesha move kama hii ya kumfanya Mr Clean awe clean wakati wote tunajua ametota kwenye kashfa ambazo zinamtaka yeye binafsi atueleze yote yalivyokuwa na sio Kadinali on his behalf. Jamani hapa Kwa kardinali kuna nini?


wait wait...nadhani nitakuwa wa kwanza kukuelewa vibaya...

i think you are using the freemason thing as a metaphor and not a testable hypothesis, right?

Even if that is teh case, you are still implying kwamba Card. Pengo ana usihirka na kina Ben na viongozi wengine wa awamu ya tatu,na for that matter anaweza pia kuwa kwenye huo ushirika wao mwingine wa siri wa freemasons

kwangu mimi nadhani tumekwenda mbali mno, ijapokuwa pia siwezi kukataa moja kwa moja kwa sababu haya mambo ni ya siri, lakini ningesita kulichanganya na hoja iliyopo hapa

Hapa hoja ni kwamba Mkapa kaagizwa akahiji kule Butiama afikishe salamu kwa Mwalimu kwa kujenga mazingira mazuri ya kanisa kustawi. Hapo kuna ishu mbili:
  1. Mkapa kwenda kuhiji Butiama
  2. Mkapa kufikisha salamu kwa marehemu Baba wa Taifa


kwa ishu ya kwanza, ungeweza pia kuielezea kwa upande mwingine kuwa Kardinali amemtuma AKATUBU, manake kutubu pia ni lengo mojawapo la kwenda kwenye kaburi, so kwa namna nyingine amemnanga Ben akajiangalie vizuri atubu dhambi zake...ni mtazamo wangu pia.

Ila kama ulivosema kwa usomi wake Pengo akapooza kwa kumwambia afikishe salamu kwa marehemu..kwani uandhani Pengo anashindwa kwenda Butiama? au ameshaenda mara ngapi? Na hapo sidhani kama angemtuma Mwinyi au JK kwa sababu nadhani hilo lingeleta mjadala mkubwa zaidi ya huu hapa.
 
Back
Top Bottom