Plummie
Member
- Aug 22, 2011
- 6
- 1
Ndugu zangu tutunze heshima ya kuitwa "Great Thinkers", kama humjui mtu usitende dhambi ya ushabiki na kuchafua hali ya hewa au kumsafisha asiyesafishika. Kwa wanaomfahamu PR na utumishi wake, Tanzania haina watumishi wengi waadilifu kama mtu huyu. Alipinga vikali IPTL, leo (miaka 17 baadaye) hata mtoto mdogo anajua ubaya wa dili la IPTL. Amefanya mengi mazuri kwa taifa hili, wewe nami hatuwezi. Kwanza ukikaa naye nusu saa unagraduate digrii ya kwanza.
Amesafisha Wizara ya Maji, kasafisha Wizara ya Mambo ya Ndani, na sasa anasafisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi. Akiwa Wizara ya Mambo ya Ndani, alishauri kuwa Mradi wa Vitambulisho ulivyobuniwa na wanaotakiwa kutunza usalama wa watu na mali zao utaiingiza Serikali kwenye kashfa nzito (wakamuhamisha) subiri kidogo uone madudu yajayo.
Huku aliko kakuta UFISADI PAPA WA ARDHI uliokubuhu kwa zaidi ya miongo minne. Huku kuna ka-mchezo ka kuuza viwanja vilivyopangwa kubaki kwa matumizi ya wazi. Kamchezo ako ni kati ya Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na Mafisadi wa Ardhi na ni ka muda mrefu. Kwa mchezo huo, mafisadi huchukua maeneo rasmi ya wazi, wakipigwa stop na mamlaka husika (Kamishna wa Ardhi) hukimbilia Mahakama ya Ardhi kudai "settlement out of court" kwa kuwatisha watumishi wasiojiamini (au wala mlungula) kwamba wakikaidi watafungwa, ili hatimaye, Waheshimiwa wasio waaminifu watumie rungu la Nyumba inayoheshimiwa (Mahakama) kubariki DHULUMA KWA UMMA. Mabadiliko ya matumizi ya viwanja vya wazi hayawezi kufanywa kwa manufaa ya kikundi kidogo au mtu. Huu ni uvunjifu wa Sheria za Ardhi.Safari hii wamegonga mwamba wa kale (PR), hatishwi mtu, hafungwi mtu, na wala halipwi mtu. Wamechimba shimo, wataingia wenyewe. Hata majaji hawako juu ya sheria.
Ndugu zangu, watumishi wa ardhi wala rushwa na MAFISADI PAPA WA ARDHI, PR kawasambaratisha, baadhi yao naona wakichangi thread hii. Aidha, kumbuka anatafutwa KMK baada ya mzee wa sasa kustaafu na KM mtembeza bakuli kunyea kambi. Eti wanaangalia anayeweza kuwa KMK na kudhamiria kumharibia PR safari! Kama JK anataka kufanya usafi wa Serikali na kurejesha heshima amteue PR muone. Hata ule mtaji wa "POSHO" wa kambi fulani utakuwa kwishney! Anayemfahamu vizuri PR ni Padri Privanus Karugendo ambaye aliandika makala yenye mantiki, siku kumi zilizopita. Uliza ujuzwe.
Unamjua PR vizuri sana, umenena vyema