Elections 2010 Kwanini Nyerere hakutishia "kumwagika damu" mwaka 1995?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Mwaka 1994 mauaji ya kimbari yametoka Rwanda na maelfu ya Wakimbiza walikuwa wamevuka kuja magharibi mwa nchi yetu. Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa Rais na Wabunge ndani ya mfumo wa vyama vingi ukafanyika Oktoba 29, 1995. Wakati ule Nyerere alishiriki kumpigia debe Mkapa karibu sehemu mbalimbali nchini ili achaguliwe.

Nakumbuka kampeni ile vizuri zaidi kwani nilikuwepo mmoja wa waangalizi wa Uchaguzi ule. Na nilikuwepo Nyerere alipokuja na kupiga kampeni pale Nyamagana kumnadi Mkapa. Hata hivyo nakumbuka mambo fulani:

a. Hoja yake ilikuwa ni usafi wa kiongozi anayekuja
b. Upinzani ulikuwa bado haujakomaa kuongoza labda wakipewa muda.
c. Sikumbuki hata mara moja kuwa alitumia yaliyotokea Rwanda kuwa ni mfano wa kile kinachoweza kutokea Tanzania ati wakichagua upinzani na nitakuwa tayari kusahihishwa na wengine waliomsikia mahali pengine kwani kama ingekuwepo CCM wangeweza hata kutumia hotuba hiyo kwenye kampeni zao leo hii kwa mafanikio makubwa.

Nabakia najiuliza:

Kama Nyerere ambaye alijua mambo ya Rwanda vizuri sana na alikuwa karibu zaidi kihistoria na matukio hayo hakuweza kutumia hoja ya umwagikaji damu kuwatisha Watanzania wasichague upinzani kwanini hawa watawala wetu wanapata u jasiri huo sasa? What is wrong with this picture?
 
mm huyu jk Hana cha kuwaambia watz nod maana anaongea mambo ya hovyo hovyo
 
Hali mbaya muoneeni huruma makamba chama kumfia yeye aibu
 
Ukiona watu wanakuja na visingizio vya 'watu wanataka kumwaga damu' ujue maji yamewafika shingoni wanatapatapa.
 
Elimu ndogo ya uraia na ujinga wa wapiga kura wa vijijini ndio mtaji wao (JK, Makamba, AK,RA,etc) mkubwa kwani hawana hoja tofauti inayozidi zile za kambi ya upinzani.
Na kutokana na ukweli kuwa wapiga kura wengi wako vijijini na wengi wao kuwa hawana ufahamu wa mambo yanayotokea tofauti na yale yanayotolewa na viongozi (kwa sababu haya ndiyo yanayoripotiwa na vyombo vya kitaifa) wanabaki kuwa shamba la rutuba kupanda ujinga na propaganda za maji taka kama umwagikaji wa damu na machafuko. Huu ndio mtaji wao pekee uliobaki kushinda uchaguzi wa mwaka huu kwa kura.
 
Kama Nyerere ambaye alijua mambo ya Rwanda vizuri sana na alikuwa karibu zaidi kihistoria na matukio hayo hakuweza kutumia hoja ya umwagikaji damu kuwatisha Watanzania wasichague upinzani kwanini hawa watawala wetu wanapata u jasiri huo sasa? What is wrong with this picture?

Kwa ninavyofahamu mimi hili la damu lilianza kutamkwa na mgombea unayempigia chapuo, sasa ili kubalance swali ungeuliza na kwa nini wakati ule Agustine Mrema(pamoja na kuonekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda wakati ule kuliko huyo wako) hakuwahi kutoa kauli za kumwaga damu 'ikbidi'.
 
Panya alietaitiwa kwenye kona atatafuta kila mbinu ya kujiokoa, hata ikibidi "kupaa" ilhali hana mbawa.

Rungu tunalo

Nia tunayo

Sababu kibao tunazo

Na uwezo tunao!!!!!!!

Piga piga kanyaga!!!!!!!!!!
 
Sijui ni nani unaedhani MM anampigia chapuo. Hata hivyo kama wewe ni muungwana na great thinker (kama wewe sio kama Kinana), naomba unukuu usemi wa kiongozi au mgombea yeyote unaoashiria, au kuhamasisha umwagikaji damu...
 
Nadhani mkuu hii ya siasa za kuwatisha wadanganyika ni kwa sababu ya kuona sera zao hazikubaliki ndo wameamua kuwachafua wenzao kwa kusema kuwa ni wenye malengo ya kumwaga damu!
 
Sijui ni nani unaedhani MM anampigia chapuo. Hata hivyo kama wewe ni muungwana na great thinker (kama wewe sio kama Kinana), naomba unukuu usemi wa kiongozi au mgombea yeyote unaoashiria, au kuhamasisha umwagikaji damu...

Na mwaka huu tuemekwisha waagiza vijana, tupige kura zetu kisha tuzilinde ikibidi tutazilinda hata kwa damu...nimesahau jina la huyo mgombea na chama chake.
 
mm huyu jk Hana cha kuwaambia watz nod maana anaongea mambo ya hovyo hovyo

hakuna mgombea wa ccm mwenye uwezo wa kunadi ccm kwa zaidi ya dk 15 labda magufuli tu. kikwete mwenyewe hasidi dk 7 siku hizi. they have nothing to offer
 
Mtu mmoja mahali fulani aliwahi kusema..."Wining through intimidation is the means used by all corrupted leaders" . Huwezi kuamini kabisa CCM yenye mfumo na mjengo mzuri kuliko chama chote afrika ... Today is totaly compromised, consumed and corrupted than any evil system you dare to imagine! Inanisikitisha, Inatia majonzi kuona vihoja vya kichizi, vimkakati vya hovyo hovyo, vijimsamiati vya kiruada, vipropaganda vya kihuni vikibebeshwa kwa chama kama CCM ambacho tumekitolea jasho na kila senti ya mlala hoi kukijenga... Ujinga wa Uongozi unaopania kuua SPIRIT ya kweli ya UTANZANIA... ni ujinga kweli, Maana the spirit will never die ..if you know what am talking...Choice has to be made... UONGOZI HUO UANGAMIE NATURALY AU HIYO SPRIT! Na jibu liko wazi!!!! Lakini tuna imani kwa uongozi usio na ukaidi na wenye usikivu kama wa Kikwete una nafasi ya kujirudi...na nafasi bado ipo! Kama Hautafanya hivyo unategemea umma wa WATANZANIA WENYE UCHUNGU NA UTANZANIA WAO UFANYE NINI?
 
Na mwaka huu tuemekwisha waagiza vijana, tupige kura zetu kisha tuzilinde ikibidi tutazilinda hata kwa damu...nimesahau jina la huyo mgombea na chama chake.

Burn, it is unfortunate kwamba umesahau jina la huyo mgombea na chama chake. Lakini nadhani unatakiwa ku - consider ujumbe wa hiyo statement. Amesema walinde kura zao ikibidi hata kwa kumwaga damu (kama ndivyo alivyosema). Mbona ni wengi tu wamemwaga damu kwa kulinda mali zao zilizotaka kuporwa na majambazi.

kwa jinsi nilivyoielewa statement ya huyo uliyemnukuu ni kuwa yeye (wao) siyo watakaoanzisha umwagaji damu ila ni wale wezi wataotaka kuiba / kupora kura zake (zao)
 
Ni kweli ila hapo mwisho ndio kuna utata unaposemakuwa wao hawataanzisha kumwaga damu maana hatukusikia kauli yao wanaotaka kuiba kura wakisema kuwa mwaka huu wataiba kura hata kwa kumwaga damu, hivyo nilidhani mwakijiji alipoleta suala la kumwaga damu angewatendea haki wanaojibu suala hilo kwa kuwataja kama wanajibu damu baada kutishiwa damu. Naamanisha kuwa mwaka 1995 nyerere hakujibu damu kwa sababu hata Mrema hakutoa vitisho hivyo vya kumwaga damu 'kulinda kura'
 
Vilitumika vituo vya television za DTV na ITV kuonyesha mauaji ya Rwanda wiki nzima kuelekea uchaguzi. Acheni kutudanganya! :hand:

Isitoshe hao wanayezungumzia kumwaga damu na pipoz pawa ni hao hao unaowapigia debe.

Hatudanganyiki lakini kudanganya rukhsa!
 
...
kwa jinsi nilivyoielewa statement ya huyo uliyemnukuu ni kuwa yeye (wao) siyo watakaoanzisha umwagaji damu ila ni wale wezi wataotaka kuiba / kupora kura zake (zao)

JB ... Huo ndio Ujumbe wa kutafakari!!

Na Mimi Nina hakika wataepusha hali hiyo isitokee Kwani bado wana nafasi ya kutosha kabisa...au wantaka kusema nini?
 
Wana JF kama tutaacha ushabiki tunaweza kutoa hoja za kuchambua kauli hizi kwa uhalisia wake.

Kwa maoni yangu kauli za CCM zinazosema wapinzani wamepania kumwaga damu ni moja ya propaganda katika kipindi hiki cha kampeni. Suala la damu kumwagika siyo tu ni baya bali ni balaa. Hivyo kulifanya hoja katika kampeni ni uchuro usiokubalika. Hivyo CCM wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kuacha kutoa kauli za namna hiyo.

Kwa upande mwingine jeuri hii ya CCM kusema kauli hizi imetokana na wapinzani wenyewe. Ni mara ngapi tumeshuhudia wagombea tena wengine wa urais wakidai kuwa CCM imejiandaa kuiba kura. Kwao wao wanaamini kuwa CCM lazima itashindwa kinyume chake CCM itakuwa imeiba. Kauli hizi pia zimejaa humu JF. Kusema kwa kurudia rudia kuwa CCM ITAIBA kura hata kama hicho kitu ni hisia tu hiyo ni hatari zaidi.

Kwa watu wanaofahamu maana ya matangazo katika biashara, mbinu muhimu ni kurudiarudia sifa ya bidhaa zako. Unaporudia mara nyingi inaingia katika ubongo wa binadamu na kuwa sehemu ya maisha yake. Ndio maana mwiko mmoja wa matangazo ni kutoa sifa za uongo.

Hivyo basi vyama kuendelea kusema CCM itaiba kura kwa kurudiarudia athari yake ni kwamba mawazo haya yatazama katika vichwa vya watu hivyo kama matokeo yatakuwa ushindi kwa CCM basi watu wengi wataamini kuwa CCM imeiba kura hata kama si kweli na hapa ndiyo tatizo litakapoanza.

Hivyo wakati tunaikemea CCM, vyama vingine navyo vinapaswa kukemewa mara dufu kwa kauli hizi unless watuonyeshe jinsi kura zinavyoibiwa. Kinyume chake CCM ina haki kusema vyama hivi vinataka kumwaga damu kwa sababau ni kweli kwa mantiki niloieleza hapo juu.
 
Elimu ndogo ya uraia na ujinga wa wapiga kura wa vijijini ndio mtaji wao (JK, Makamba, AK,RA,etc) mkubwa kwani hawana hoja tofauti inayozidi zile za kambi ya upinzani.
Na kutokana na ukweli kuwa wapiga kura wengi wako vijijini na wengi wao kuwa hawana ufahamu wa mambo yanayotokea tofauti na yale yanayotolewa na viongozi (kwa sababu haya ndiyo yanayoripotiwa na vyombo vya kitaifa) wanabaki kuwa shamba la rutuba kupanda ujinga na propaganda za maji taka kama umwagikaji wa damu na machafuko. Huu ndio mtaji wao pekee uliobaki kushinda uchaguzi wa mwaka huu kwa kura.

Elimu kubwa ya uraia (read Mwongozo wa Kanisa Katoliki) ndiyo mtaji mkubwa wa Slaa?

I thought kuparamia bandwagon ndiyo ushamba zaidi!
 
Panya alietaitiwa kwenye kona atatafuta kila mbinu ya kujiokoa, hata ikibidi "kupaa" ilhali hana mbawa.

Rungu tunalo

Nia tunayo

Sababu kibao tunazo

Na uwezo tunao!!!!!!!

Piga piga kanyaga!!!!!!!!!!

Uwezo wa kujaza kura za online poll za JF ndiyo mnao! Teh teh teh! :tonguez:

Lakini uwezo wa kuzitoa tigo zenu mbele ya screen na keyboard kwenda vijijini kufanya grassroot movements hamna! Teh teh teh :tonguez:
 
Back
Top Bottom